Nina mke ila nimetokea kumpenda mfanyakazi mwenzangu kazini, na-handle vipi hii hali?

Maisha yamenifunza kitu kimoja, anayeweza kukuletea baraka ni wewe, na anayeweza kukuletea mabalaa ni wewe mwenyewe. Ukiisikiliza mind yako umekwenda na maji. Matamanio huja na kuondoka lakini hakikisha hayakupelekeshi kufanya vitu ambavyo vitakuharibia pakubwa. Mahusiano hayajifichi kwa hiyo kama utaanza naye tegemea kuharibu uaminifu na upendo kutoka kwa mke wako. Hata kazi itaharibika in some way.
 
Kwa kweli Nyege ni mbaya sana. Zinaweza kukuongoza vibaya ukahisi kweli.

Naomba nitumie experience yangu kidogo kwenye ishu kama yako.

Nikiwa na Mke na Watoto wawili, nilitokea kumpenda mdada wa ofisini kwetu. Nikajitahidi kumweka karibu, afu baadae nikamwambia ukweli. Alinambia James wewe umeshaoa na mke wa namfahamu, mi jambo hilo siwezi kufanya. Ungekuwa hujaoa sawa, lakini kwa Kuwa una mke siwezi kumfanyia hivo mwanamke mwenzangu.

Jibu hilo, halikunikatisha tamaa, kwa sababu tayari alikuwa ameshachukua nafasi ya mke wangu katika moto wangu. Niliendelea kumwomba na kujitahidi kumjali mwishowe alikubali. Akanipa tunda!

Cha ajabu baada ya kutoka nae mara 2, nikajikuta nimekinai. Na wala hakuwa na dosari yoyote lkn moyo ghafla ukarudi kwa wife yeye akaonekana wa kawaida tu. Hadi saiv namuona wa Kawaida tu. Sihitaji tena!!

Kwa hiyo, hiyo ni tamaa tu. Sikushauri umpige, wewe uambie moyo wako tu hapana!
 
Ikimbieni zinaa biblia inasema. Literally ni kwamba kushinda zinaa ni lazima kukimbia vishawishi vya zinaa. Kaa mbali naye, futa namba yake, mheshimu Mungu na mke wako pia.
 
Hakukupenda alikupa tu ili kukufurahisha moyo wako, aliona wakawaida tu ndiyo maana hakupagawa nawewe
 
Mtaarifu mkeo haraka sana kuhusu hizo hisia.
 
Mkuu kama hujawai chepuka usijaribu tia doa Hilo kwenye ndoa yako, Vipi mkeo nae akianza chepuka na ktk kumuulzapo akasema aliona we humuheshimu ndomana naye kafanya hivyo na anakugey evidence juu.
 
Achana na mawazo juu ya binti huyo, huu uzinzi ni mbaya sana, ndo humo tunapataga mikosi na balaa maishani mwetu.

Unaweza kuta mambo yako yalikuwa yanaenda vizuri tu, Ila baada ya kufanya uzinzi yanaanza kwenda shaghalabaghala, yaani Kama ni kwenye biashara unakuta mpaka wateja wako wamekuhama, Kama ni ofisini heshima inashuka na hiyo siyo kwamba wamesikia habari zako, ni basi tu malipo ya zinaa.
 
Mheshimu mkeo kama anavokuheshimu, tuliza mihemko why uliwahi kuoa ikiwa bado unatoa toa macho kwa mabinti wengine?😬
Nani alikwambia kwamba ukichelewa kuoa unakuwa hutoi macho kwa vibinti wengine?
Kuna mafataki wenye wake zao wamechelewa kuoa na bado wanamendea wake za watu.sisi wanaume ndo tunaelewa hizi situesheni
 
Pole sana, hayanaga muongozo...

Mapenzi ya kazini mwisho wake hua mbaya sana...
 
Mkuu mbona mkeo yupo vizuri tu kwa avatar! Muombee nafasi hata ya kujitolea hapo ofisini hakika upendo wako kwake utarudi akiwa mfanyakazi mwenzio.
 
Kikubwa ni uvumilivu leo utampeda huyu na kesho utadondokea kwa mwingine lakini nikwambie mkuu ukijitahd kuvumilia na kujikaza kisabuni mwezi tu utatosha utakuwa umeanza kumuona wa kawaida na zile tamaa zitaondoka
 

Acha upumbavu! Ukichanganya mapenzi na kazi lazima kimoja utakipoteza.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba familia utaivunja au utapoteza kazi kwa upuuzi tu.

Huyo binti kama hujui, ana malengo ya kuolewa kama walivyo mabinti wengi, sasa ukiingia kichwa kichwa utaishia kurudi hapa jukwaani kuomba ushauri binti kashika ujauzito na amegoma kutoa, masharti nayo kakuwekea lukuki.

Chagua kunyoa au kusuka, aidha ujitokeze kidume umtongoze awe mke wa pili au mchepuko, la sivyo achana naye. Baki na familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…