Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Mimi wazo langu kwako ni simple tu.

Badilisha hii akaunti yako uwe Verified User, tumia majina yako au jina moja na eneo unalotoka mfano. Mkulu wa Kagera alafu sasa anza kuuza senene hapa hapa JF uwe muaminifu tu.

Sajili lipa namba na uwe unatumia iyo lipa namba kwa biashara yako hiyo ikiwezekana fungua na akaunti ya benki.

Hapa kazi yako ni kutafuta senene kuwaweka vizuri na kuuza huku JF.

Kuna wahaya kibao tu huku wanazimis senene watakuungisha Mkuu.

Kila la heri
 
We zombie weee haujui
 
nunua kabati la aluminium la chips 200000

Mafuta lita tano 30000
Viazi kilo 20 ni 20000
meza na viti 100000
Karai la kukaanfa chips na sahani na tomato na chil sauce 50000

Yai trey 10000


Anza kazi
Anaanzia wapi sasa
 
Akienda naye kuuza hapo watamloga.au figisi za ajabu.
 
Kuna mtaji ambao ni muhimu kuliko hata Pesa..., Nao ni wewe (Mtu Binafsi) inategemea unaweza, unapenda na unajua kufanya nini na wapi....

Mengine yatakuwa ni theory za kwenye makaratasi na hizo naweza nikakutengenezea hata Trillioni kadhaa ndani ya muda mfupi sana...
 
Binafsi hili wazo nimelielewa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…