Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Huu uzi una Madini mengi sana ila pia unaonesha kabisa uelewa wa watu kuhusu biashara ukoje kwa maana ya uelewa chanya au hasi!

Siwezi kufanya QUOTE yeyote ila kwa ujumla ina aminika kuwa :
Msingi wa kwanza kabisa wa Biashara sio hata mtaji bali ni wazo lako ukijumlisha na Utayari wako ndio vitu vyamsingi kabisa.

Hii haimanishi kuwa mtaji si muhimu No...

Mtaji ni Muhimu ila ukiwa na wazo madhubuti kwanza unaweza kupata mtaji tu bila shaka kabisa kwani kuna watu wanazo pesa ila hawajui wawekeze sehemu gani kwahiyo utapata tu wakupatner nao.
Pia kama hutaki kushirikiana na mtu utaomba tu watu wakushike mkono na wakiona unachokifanya kina mantiki watakusapoti tu kwahiyo Don't dig deeper kupata mtaji kabla ya kwenda deep kwenye Nini unataka kufanya na Mtaji huo na pia ZINGATIA Biashara ina kawaida ya kwenda opposite na unavyopanga at first... Je utakuwa tayari ku persevere!???
Wee jamaa una akili sana
 
Hongera mkuu.ila duniani nimegundua tunatofautiana Sana..kwangu laki nne na nusu ni hela nyingi Sana tena kwa.kijana mwenye nguvu na miguu
Miss Natafuta nilichokuja kugundua kumbe mavitu ya wadada yanalipa sio mchezo... Kuna bidhaa nilikuwa nachukua kwa jero nikifika kule machimbo nawapiga kwa elfu 5 hadi 6 wenyewe wanafurahia tu...😂😂

Sasa hivi naishi kweny ujuzi nilionao maana huko kuishiwa hela za kila siku sio rahisi!
 
Ukiwa unataka kufungua Biashara huku kichwani kwako una mentality ya kwamba nina 450k nifanye biashara gani ili nisipoteze hii pesa Au ili nipate Faida kubwa pengine ndani ya mda fulani (mfupi) hapo umeshafeli hata kabla hujaanza chochote!!!
 
Kiongozi kwanza pole.

mimi nakushauri kwamba cha kwanza kamwe usitumie hela yako yote kwenye kufungua biashara.

Anzisha biashara yenye kutumia mtaji mdogo kabisa na ambayo haitakusumbua hata kidogo ili kuweza kuhifadhi kiasi kingine cha pesa.

Tumia hela kidogo sana kiasi kisichozidi elfu 35,000 fungua biashara ya kukaanga chapati.

Mtaji Mkuu:
Huu ni mtaji usiorudisha faida. Ni msingi wa biashara yako.

Hotpot-10,000
Kaangio ya chapati-4,000
Sukumio la chapati-7,000
Jiko la mkaa-4,000
Baking Powder-1,000
Chumvi-1,000
Tafuta stuli hapo nyimbani.
Jumla kuu-27,000

Mtaji endeshi:
Huu ni mtaji unaokurudishia faida. Hii itaendesha biashara yako kila siku na ndio wenye kukupa faida.

Ngano kilo 1-2,000
Mkaa-500
Mafuta-1000
Jumla kuu-3500/=


Maelekezo:

a. Katika kilo moja ya chapati toa chapati 20 za chapati na kishauza chapati 2 kwa sh. 500(20÷2×500)=5,000 ambayo ni mauzo yote kwa kilo moja.

b. Chukua 5,000 ya mauzo -3,500 ya mtaji = utabakiwa na 1,500 kama faida.

c. Amka asubuhi na mapema sana saa 12 hakikisha unakaanga chapati zako mbele ya unapoishi hapo barabaran wanapopita watu.

d. Hakikisha chapati zako ni nzuri, tamu na yenye kuvutia.

e. Hii biashara inafanywa na jinsia zote. So usiome Soo kuwa wewe ni mwanaume.

Matokeo:
a. Ukifanya vema kwa siku nakuhakikishia kilo 2 za chapati kuisha ni uhakika in which utapata faida ya 3,000 kwa siku.

b. Ukifanya hivo kwa 26 katika mwezi utakuwa na faida ya Tsh. 78,000/=

e. Endelea hivyo hivyo mpka uweze kuuza kilo 4 per day. Hii itategemea ubora wa bidhaa yako, location ya biashara na customer service yako kwa mtaji.

Asante.
Hii biashara imenisomesha.
 
Mkulu wawe

Kama huna nia wala passion ni rahisi kuyumbishwa yumbishwa.

Biashara inaanzia moyoni, mfano mimi niliwahi kukataa kazi ya laki4 kwa mwezi sababu nilishakua nimeanza biashara kwa mtaji wa chini ya Elfu50 na faida ya elf6 kwa siku x mwezi = 180,000/=


Kwa mwingine atapiga hesabu ya ukitoa matumizi unabaki na nini bora ajira.


Ukweli mchungu: Mwenye passion ya biashara hayumbishwi na chochote kinachohusu ajira, kwanza anajiepusha sababu anakua anajua anaelekea wapi maana biashara hukua, ila mshahara haukui.


NB: Biashara ni kama mapenzi unatakiwa ujitoe na uwe na nia kweli maana Changamoto zake ni ngumu kuliko kwenye ajira Ukiingia kichwa kichwa kwa sababu ya shida tu, au kujishikiza au kukamilisha tu mahitaji itakufanya hivi 👇
tapatalk_1677991808146.jpg

Mwisho utaanza kuzunguka na vyeti kutafuta kazi tena.


Sasa nifanye nini? Kama una nia:

•Narudia tena mtafute Kibenje KK, ukimkosa huku Jf nenda moja kwa moja kwenye page yake youtube "Kelvin kibenje" - utapata Idea zaidi ya 100+ wewe utaangalia ufanye nini, Au nenda kafungue video comment no.139.


•Kama ukipata cha kufanya utajaribu na kukipitia na hicho kitabu hapo.


NASISITIZA NIA, NIA, NIA,,,,,,,,,,,,,!! Otherwise hizi zitabakia kama Story za kwenye kahawa tu..!!


Sitaki uni-Quote, Just act 😎
 

Attachments

Anzisha Biashara ukiwa Firmly committed kwamba nataka nifanye Biashara hii kwa sababu nimefanya research ya kutosha nimeona kuna Fursa hapa kwa kupitia utatuzi wa changamoto flani nitapata Faida. They say Business is all about making profit through solving people's problems.... Usianzishe Biashara tu kwa kufata Mkumbo Fanya research yako ya kina hata kama biashara hiyo kuna mtu amekushirikisha!!
 
Mkuu jamaa ameomba ushauri wa biashara ya laki4 na nusu, sasa mbona wewe unampa wazo la mtaji wa elfu 35.

Huoni kama unamrudisha hatua 15 nyuma.....!!
Mkuu labda kama sijamuelewa vema. Lakini amsesema amefukuzwa kazi na ana sh. Lk 4.5

So, kwa uzoefu wangu katika biashara nimeona nimshauri biashara atakayoweza kutumia hela kidogo na akapata return kubwa ndani ya muda mfupi.
 
Usinichonganishe, Mimi sio kijana wake kwanza hanijui 😆😆

Uzuri huyu jamaa anakusanya Idea tofauti tofauti, Ni rahisi kupata wazo huko la mtaji wowote.
Huyu dogo wazo la biashara linaletwa na sababu. Lazima aangalie mazingira yake yanhitaj nn na aangalie mkakati atakaotumia kupata wateja ili adecide kufanya biashar husika. Biashara ziko nyingi tu za mtaji huo na anaweza kusogeza maisha bila shida. Kelvin ni jamaa yangu sana ila hata mawazo ya wana jf pia anayatumiaga so jamaaa asiohope kabia unless amtafute kelvin ili akahamasishwe
 
Mkuu labda kama sijamuelewa vema. Lakini amsesema amefukuzwa kazi na ana sh. Lk 4.5

So, kwa uzoefu wangu katika biashara nimeona nimshauri biashara atakayoweza kutumia hela kidogo na akapata return kubwa ndani ya muda mfupi.
Sawa mkuu,,,,,!
 
Kijana usiendelee kusoma mawazo mengi ya humu JF yatabaki kukuchanganya tu na utashindwa uanze na lipi.

Cha msingi wewe chukua wazo moja ingia field uhalisia utaukuta hukohuko hata kama utapata hasara lakini changamoto zitakufundisha mengi!
 
Mkuu hi biashara numefanya hapa ofisini kwangu kuna mdDa alileta hvo vitu..

Mkuu hii ishu hii acha tuu... Usichukulie simple aiseee unaweza kusema kuna pesa ila ukianza kupika hv mbona utakubali
Hizo biashara ya visheti kashata ice cream usidhirau. Kuna dingi mmoja na mke wake wanauzia wanafunzi wa primary na secondary pale mavurunza kimara. Jioni wakikutana na mke wake pesa wanayoweka mezani mzee sio masihara.

Kwaiyo kuna baadhi za biashara unaweza zichukulia poa ila zinafaida sana inategemea tu na uthubutu wako na namna utavojitoa.
 
Back
Top Bottom