Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kagera,BUKOBAUko mkoa gani?
Daaah nyie watu nyie....Nitakupa story yangu Kwa ufupi
Nilimaliza chuo 2015
Baada ya kupambana kusaka nikawa na laki 1 tu
Nikaamua nichukue zile t-shirt manga plain, nianze kuuza kimachinga mtaani
Zile t-shirt zilipendwa na watu sana
Nilikuwa nanunua sh 6000 nauza 15000
Hadi nikawa maarufu chinga matishet
Nikipata order nyingi sana
Huu mtaji ndo umenipa kila kitu baada ya miaka 9 saiv Nina maduka mawili ya nguo yenye kila kitu
Naendaga kariakoo naifunga mzigo kuanzia million 10 Kwa mtaji wa laki 1
Hii story ni ya kwangu binafsi na Iko ivo
Usidharau mtaji wowote
Biashara ni timing tu mkuu na ubunifu wako tu
Laki 4 anakomaa na anatoka vizur
Hamna u seriously paleKwahiyo wanaofanya hizo biashara hawako seriously
Jaribu kilimo cha matikiti utanikumbukaWakuu nimefukuzwa kazi
Niko na mtaji wa Laki nne na nusu (450,000/-) naombeni ushauri nifaye nini na hiyo hela
Milioni 2 au 1.5Kwahiyo biashara serious inatakiwa aanze na milioni ngapi? 😁
Mi sijaja kutania hapa mkuut
Una wazo mkuu, usikilizwe
Nimecheka sana eti wanaviita vibolo😂😂😂😂 vitakuwa vya BataHii nasema mimi kwa experience yangu.....
View attachment 3167914
Hivi vidude unavijua?? Vinaitwa visheti watoto wanaviita vibolo.
Ukivipika kilo tano ni vya elf 50, kilo moja inatoa vibolo 100.
Mahitaji ya kilo tano ni ngano kg 5, amira tatu ni 300, nazi 1, mafuta lita 1.5-2 sukari kilo 1 na robo.
Mtaji hauzidi hata elf 30, na ukitaka kufaidi pesa yake nunua ngano ya mfuko, mfuko wa ngano ni elf 40.
Wasema laki nne haitoshi 🤸🤸🤸 naomba laki mie nkanywe bia, nakuinbox my yas namba
Nilikuwa MwanzaDaaah nyie watu nyie....
Kipindi unaanza biashara ulikua unakaa wapi mkuu..?
Mbona hesabu zinagomanunua kabati la aluminium la chips 200000
Mafuta lita tano 30000
Viazi kilo 20 ni 20000
meza na viti 100000
Karai la kukaanfa chips na sahani na tomato na chil sauce 50000
Yai trey 10000
Anza kazi
Karibu mkuuNikitulia naweka kisa changu hapa hiyo laki nne na nusu ni hela kubwa sana.
Kuna kipindi nilipata kazi ya mkataba wa miezi 6 nikawa nalipwa vizuri kama elfu 45 kwa siku pamoja na hela ya usafiri basi nikajisahau nikidhani kazi itadumu aisee nilikuwa mtu wa kujipongeza na hela za posho kuja kushituka mkataba unaelekea kuisha na sina savings yoyote ya maana na madeni juu. 😂😂
Nilisota kama mwezi mmoja hivi sina kazi akiba yangu ilikuwa haizidi laki 3🤣🤣 kwakuwa nilikuwa na mke na mtoto nikampa laki 2 ya matumizi mimi nikabaki na laki 1 tu huyo nikatokomea kujitafuta upya! 😁
Haya maisha yaacheni tu!
Wauza mifuko masokoni wana mtaji gani wale?? Wauza maji , wauza matunda , wauza alkasusu mitaani humo wana mtaji kiasi gani??Anashangaza walah laki nne na nusu daaah atakua wa kishua sana huyu hi dad hi mom
Ingekua rahis hivyo walimu si wangeshatoboa maisha mana ndo biashara yaoHii nasema mimi kwa experience yangu.....
View attachment 3167914
Hivi vidude unavijua?? Vinaitwa visheti watoto wanaviita vibolo.
Ukivipika kilo tano ni vya elf 50, kilo moja inatoa vibolo 100.
Mahitaji ya kilo tano ni ngano kg 5, amira tatu ni 300, nazi 1, mafuta lita 1.5-2 sukari kilo 1 na robo.
Mtaji hauzidi hata elf 30, na ukitaka kufaidi pesa yake nunua ngano ya mfuko, mfuko wa ngano ni elf 40.
Wasema laki nne haitoshi 🤸🤸🤸 naomba laki mie nkanywe bia, nakuinbox my yas namba
Mleta mada soma vizuri ujumbe huu utakusaidia...Biashara!
Watu wengi humu watakushauri kwa kukuambia fanya hiki ama kile ila mifano yote hiyo ya biashara watakazo kupatia ni kutokana na mafanikio ambayo wamewahi kuyapata au wameyapata kupitia biashara hizo ila walio wengi ni kwamba hizo sio biashara zao za kwanza isipokua ni zile biashara ambazo ziliwafanikisha baada ya msululu wa biashara nyingi ambazo wamewahi kuzifanya na kufeli, na Watu hawa ukiwauliza ni jambo gani la tofauti ambalo wamelifanya hadi kupelekea mafanikio kutoka kwenye hiyo biashara ambalo katika biashara zingine zilizokufa hawakulifanya hawatokua na jibu la uhakika la kukupa.
Na ndio maana huwa sipendi kumshauri mtu kwa mtindo wa moja kwa moja kwa maana haya mambo huwa hayana formula lakini...
Nataka uwe na hakika kwamba kila mtu anao uwezo wa kufanikiwa kibiashara lakini si kila biashara inayo uwezo wa kumfanikisha kila mtu.
Kwani...
Biashara ni neno moja katika jicho la kawaida la walio wengi ila kwa jicho la ndani biashara ni muunganiko wa maneno mawili ambayo ni kusaidia pamoja na fedha na maneno haya huwa hayaendi pamoja kwa hiyo unapoanzisha biashara yoyote lazima uamue neno lipi utaanza nalo na lipi litafuata, uchaguzi wako wa lipi lianze na lipi lifuate ndio ambao utatoa taswira ya muda gani utakaa na hiyo biashara kabla haijawa yakudumu au kukufia mikononi mwako mwenyewe.
Na hii ndio sababu ya kwanini ni ngumu kumpa mtu ushauri wa biashara gani afanye kwa maana haujui ni changamoto za kiasi gani za kifedha zilizomzunguka ambazo zinamuhitaji yeye azitatue na kuanza kwake biashara anategemea kesho aanze kupata faida ili atatue changamoto zake.
Na ndio maana ushauri wa biashara nyingi za kufanya ambao watu wamewahi kupewa walipoamua kuzianzisha biashara hizo zilikufa kwa maana wengi huanzisha biashara huku wakichagua kwenda na neno fedha badala ya kusaidia.
Sasa fedha inakawaida ya kuwazingatia wale watu ambao hawaizingatii, na sababu ya fedha kufanya hivyo ni kwamba watu wengi ambao hawaizingatii fedha huwa sio wabinafsi, na hii inamaanisha kwamba fedha na ubinafsi huwa havikai nyumba moja.
Na kikawaida ni kwamba nyakati nzuri ambazo mtu huwa hawi na mazingatio makubwa kwenye fedha ni zile Nyakati ambazo uhitaji wa fedha kwake ni mdogo au haupo kabisa.
Na nyakati pekee ambazo mtu anakua katika hali hiyo ni zile nyakati ambazo anakua hana cha kupoteza kwa maana ukiachana na yeye mwenyewe hana watu wengine ambao changamoto zao za kifedha zinamtegemea yeye kuzitatua.
Ukishakua na changamoto nyingi za kifedha ambazo unahitaji uzitatue, kwenye biashara utachagua kwenda na neno fedha na utaachana na kusaidia na ukishaachana na kusaidia basi unakua mbinafsi na ukiwa mbinafsi fedha inatengana na wewe na fedha ikishatengana na wewe hautakua na nguvu ya kuendelea na hiyo biashara kwahiyo itafia mikononi mwako mwenyewe.
Ili uweze kupata unafuu kidogo inabidi utumie mbinu ya kujitengenezea kazi mwenyewe badala ya biashara.
Kwa maana biashara na kazi ni mambo ambayo hayana utofauti pindi yanapoanza kwenye lile swala la muda ila kadri siku zinavyokwenda biashara hujitenda kwenye kazi.
Kazi inaweza kuanzishwa na mtu yeyote yule kwa maana huwa wazo lake likimjia mtu kichwani muda huu basi kesho anaweza akalitekeleza na kuingia sokoni moja kwa moja ila biashara ni ngumu kwa maana huwa inahitaji mchakato wa muda mrefu tangu wazo linapomjia mtu kichwani hadi kuingia sokoni kwa maana linahitaji nguvu zote nne za asili ya ulimwengu ziweze kuingia ndani yake.
Kwahiyo sio kila kazi inaweza kuwa biashara ila zipo kazi ambazo zinauwezo wa kuwa biashara kwahiyo kama wewe uko na changamoto nyingi zinazohitaji fedha na unataka uanze kupambana mwenyewe anzia kwenye hiyo hatua ya kazi kabla ya kwenda kwenye biashara.
Biashara huwa tunaipima kwa magnitude and leverage, ila kazi haina hizo sifa ingawa kuna kazi ambazo zinauwezo wakupelekwa kwenye hizo sifa na hizi ndio unatakiwa uanze nazo kwa maana unahitaji uwe mfanya biashara.
Kila la heri.
Tatizo wanadhani kila biashara lazima uanze na mamilioni.Karibu mkuu
Wapewe hawa watoto uzoefu
Mtu anadharau laki 4
Ile mashine milioni mkuuUza juice ya miwa
Hongera mkuu.ila duniani nimegundua tunatofautiana Sana..kwangu laki nne na nusu ni hela nyingi Sana tena kwa.kijana mwenye nguvu na miguuTatizo wanadhani kila biashara lazima uanze na mamilioni.
Nakumbuka nilikuwa na laki hapo sijajua cha kufanya nilimfata rafiki yangu niliyesomaga nae yeye alikuwa ana ofisi kubwa katika kupiga nae story alinipa wazo konki ambalo mpaka leo limenipa hela nyingi.
Iko hivi hakuweza kunikopesha hela ila alinijua kuwa nina bidii ya kujituma kwenye kazi, basi akinielekeza kwa boss wake(anayemuuzia bidhaa kwa jumla). Nikaenda na laki 1 yangu lakini nilipewa jumla mzigo wa laki 3 yeye ndo akawa mdhamini wangu.
Nilichukua hizo bidhaa za Urembo nikaingia nazo maeneo ya machimbo huko mkoa x.. Niliuza bidhaa zote ndani ya siku 5 zikaisha nikawa na kama laki 5 na elfu 60 nikarudi town kufunga mzigo mwingne, waliowahi kuuza urembo wamenielewa hiyo faida ni kawaida maeneo ya mgodini...
Nilizidi kukomaa hivyohivyo mpaka kuwa na goli la 5m+,akaniongezea na ujuzi ambao mpaka sasa hvi ndo unaniweka mjini kama nikihitaji pesa za kula napata vizuri nimefungua ofisi 2 zinazotoa hizo huduma na wateja nawapangisha tu foleni.
Wanaosema mtaji hautoshi ni watu ambao hawajawahi kuishiwa au kuanzia chini kabisa.
Nawasilisha! 🙏
Hebu acha kuandika vitu visivyo na uhalisia wewe motivation speakerWewe binafsi huna idea yoyote nini cha kufanya? Tuache uvivu wa kufikiri. Tazama fursa za kiuchumi ulipo kisha urudi hapa ukitaja wewe ni nani,una ujuzi gani,upo sehemu yenye fursa zipi,commitment yako ikoje kwa maana ya muda usimamizi na ufuatiliaji kisha urudi jukwaani upate ushauri.