Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Madam nipo seriously...
Wee biashara ya laki nne kama unashauri afanye sawa alafu alete mrejesho hapa..

Maana nakumbuka nilikua na pesa zaidi ya hiyo kipindi hicho na ni mfatiliaj sana wa nyuzi kule jukwaa la biashara..

Mkuu ipo hvi ukitaka kufanya biashara ili ujue pesa hiyo inatosha au laa ingia mzigoni ndo utajua ujui mkuu...

Naposema jamaa ajichange basi namaanisha kama anataka kufanya afanye alafy ataleta mrejesho hapa..

Usiingie katika biashara kwa ku test et fulani mbona alifanya hivi na mi ngoja nijaribu...
Biashara hata kama unaanza mdogo mdgo sio kwa laki 4..

Wakuu kuweni serious
Acha uoga kijana laki nne na nusu ni nyingi mno .watu tumeanza na mavuzi tu
 
Madam nipo seriously...
Wee biashara ya laki nne kama unashauri afanye sawa alafu alete mrejesho hapa..

Maana nakumbuka nilikua na pesa zaidi ya hiyo kipindi hicho na ni mfatiliaj sana wa nyuzi kule jukwaa la biashara..

Mkuu ipo hvi ukitaka kufanya biashara ili ujue pesa hiyo inatosha au laa ingia mzigoni ndo utajua ujui mkuu...

Naposema jamaa ajichange basi namaanisha kama anataka kufanya afanye alafy ataleta mrejesho hapa..

Usiingie katika biashara kwa ku test et fulani mbona alifanya hivi na mi ngoja nijaribu...
Biashara hata kama unaanza mdogo mdgo sio kwa laki 4..

Wakuu kuweni serious
Kwahiyo ndugu Hawa jamaa wanaochoma mahindi huku mtaani mitaji yao ilianzia milioni ?
 
Hii nasema mimi kwa experience yangu.....

View attachment 3167914
Hivi vidude unavijua?? Vinaitwa visheti watoto wanaviita vibolo.

Ukivipika kilo tano ni vya elf 50, kilo moja inatoa vibolo 100.

Mahitaji ya kilo tano ni ngano kg 5, amira tatu ni 300, nazi 1, mafuta lita 1.5-2 sukari kilo 1 na robo.

Mtaji hauzidi hata elf 30, na ukitaka kufaidi pesa yake nunua ngano ya mfuko, mfuko wa ngano ni elf 40.

Wasema laki nne haitoshi 🤸🤸🤸 naomba laki mie nkanywe bia, nakuinbox my yas namba
Naomba nimfundishe dada yangu jamani
 
Miss kuna kitu nataka tuwekane sawa....
Mimi mwenyewe mfanya biashara kuna mambo yanafanywa na mtu ila ukifatilia deep unajua undani wa kile anachofanya..

Naposema apambane na vibarua apate kama M1 hivi namaanisha na atanishukuru kuna vitu sio vya kusema ukurupuke tu mkuu
Mdogo wangu yaani Achana na laki nne na nusu laki mbili Tu hapo anatoboa
 
Nunua na kuuza nguo za ndani za kinamama, ongeza taiti na sidiria.

Nunua mashine ya kukamulia miwa, uza juisi ya miwa.

Nunua na uuze yeboyebo HASA za watoto.

Fungua mgahawa(baba lishe) na usimamie ww mwnyw, biashara ya chakula inalipa Sana

Au nenda mahali penye soko lililochangamka, tafuta meza na uuze mifuko tu
 
Tengeneza mkokoteni wenye jiko , balance itumie 300,000/= (laki 3 )na kabati lake.
Nunua kg 2 za nyama , tengeneza mshikaki anza kutembeza.
Jifunze jinsi ya kutengeneza mishkaki vizuri.
Kuwa msafi (smart sana).
Unaweza pata 10,000-- 20,000 kila siku.
 
Back
Top Bottom