Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Biashara!
Watu wengi humu watakushauri kwa kukuambia fanya hiki ama kile ila mifano yote hiyo ya biashara watakazo kupatia ni kutokana na mafanikio ambayo wamewahi kuyapata au wameyapata kupitia biashara hizo ila walio wengi ni kwamba hizo sio biashara zao za kwanza isipokua ni zile biashara ambazo ziliwafanikisha baada ya msululu wa biashara nyingi ambazo wamewahi kuzifanya na kufeli, na Watu hawa ukiwauliza ni jambo gani la tofauti ambalo wamelifanya hadi kupelekea mafanikio kutoka kwenye hiyo biashara ambalo katika biashara zingine zilizokufa hawakulifanya hawatokua na jibu la uhakika la kukupa.
Na ndio maana huwa sipendi kumshauri mtu kwa mtindo wa moja kwa moja kwa maana haya mambo huwa hayana formula lakini...
Nataka uwe na hakika kwamba kila mtu anao uwezo wa kufanikiwa kibiashara lakini si kila biashara inayo uwezo wa kumfanikisha kila mtu.
Kwani...
Biashara ni neno moja katika jicho la kawaida la walio wengi ila kwa jicho la ndani biashara ni muunganiko wa maneno mawili ambayo ni kusaidia pamoja na fedha na maneno haya huwa hayaendi pamoja kwa hiyo unapoanzisha biashara yoyote lazima uamue neno lipi utaanza nalo na lipi litafuata, uchaguzi wako wa lipi lianze na lipi lifuate ndio ambao utatoa taswira ya muda gani utakaa na hiyo biashara kabla haijawa yakudumu au kukufia mikononi mwako mwenyewe.
Na hii ndio sababu ya kwanini ni ngumu kumpa mtu ushauri wa biashara gani afanye kwa maana haujui ni changamoto za kiasi gani za kifedha zilizomzunguka ambazo zinamuhitaji yeye azitatue na kuanza kwake biashara anategemea kesho aanze kupata faida ili atatue changamoto zake.
Na ndio maana ushauri wa biashara nyingi za kufanya ambao watu wamewahi kupewa walipoamua kuzianzisha biashara hizo zilikufa kwa maana wengi huanzisha biashara huku wakichagua kwenda na neno fedha badala ya kusaidia.
Sasa fedha inakawaida ya kuwazingatia wale watu ambao hawaizingatii, na sababu ya fedha kufanya hivyo ni kwamba watu wengi ambao hawaizingatii fedha huwa sio wabinafsi, na hii inamaanisha kwamba fedha na ubinafsi huwa havikai nyumba moja.
Na kikawaida ni kwamba nyakati nzuri ambazo mtu huwa hawi na mazingatio makubwa kwenye fedha ni zile Nyakati ambazo uhitaji wa fedha kwake ni mdogo au haupo kabisa.
Na nyakati pekee ambazo mtu anakua katika hali hiyo ni zile nyakati ambazo anakua hana cha kupoteza kwa maana ukiachana na yeye mwenyewe hana watu wengine ambao changamoto zao za kifedha zinamtegemea yeye kuzitatua.
Ukishakua na changamoto nyingi za kifedha ambazo unahitaji uzitatue, kwenye biashara utachagua kwenda na neno fedha na utaachana na kusaidia na ukishaachana na kusaidia basi unakua mbinafsi na ukiwa mbinafsi fedha inatengana na wewe na fedha ikishatengana na wewe hautakua na nguvu ya kuendelea na hiyo biashara kwahiyo itafia mikononi mwako mwenyewe.
Ili uweze kupata unafuu kidogo inabidi utumie mbinu ya kujitengenezea kazi mwenyewe badala ya biashara.
Kwa maana biashara na kazi ni mambo ambayo hayana utofauti pindi yanapoanza kwenye lile swala la muda ila kadri siku zinavyokwenda biashara hujitenda kwenye kazi.
Kazi inaweza kuanzishwa na mtu yeyote yule kwa maana huwa wazo lake likimjia mtu kichwani muda huu basi kesho anaweza akalitekeleza na kuingia sokoni moja kwa moja ila biashara ni ngumu kwa maana huwa inahitaji mchakato wa muda mrefu tangu wazo linapomjia mtu kichwani hadi kuingia sokoni kwa maana linahitaji nguvu zote nne za asili ya ulimwengu ziweze kuingia ndani yake.
Kwahiyo sio kila kazi inaweza kuwa biashara ila zipo kazi ambazo zinauwezo wa kuwa biashara kwahiyo kama wewe uko na changamoto nyingi zinazohitaji fedha na unataka uanze kupambana mwenyewe anzia kwenye hiyo hatua ya kazi kabla ya kwenda kwenye biashara.
Biashara huwa tunaipima kwa magnitude and leverage, ila kazi haina hizo sifa ingawa kuna kazi ambazo zinauwezo wakupelekwa kwenye hizo sifa na hizi ndio unatakiwa uanze nazo kwa maana unahitaji uwe mfanya biashara.
Kila la heri.