Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Umenikumbusha mbali sana hii biashara ione kwa mwenzako nilimuweka Dogo muha mara kuku na mishkak inabaki hadi ina chacha, gas inaisha kila wiki faida inakuwa ya kununulia gas, mara kodi.
Nikakuta jiko na kabati nmerudisha geto nikaja kuyauza kwa hasara.
Ila ajaribu aone
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna mtu nilimfungulia hiyo biadhara, kweli isikie tu kwa mtu, sasa hana chochote na kodi anadaiwa ananitegemea mimi wakati na mimi sina kitu
 
Tafuta sehemu nzuri centre
Anza kuwekea watu macover ya simu na protector
Protector za kawaida jumla ni sh mia.tano
Mteja mmoja bei chini Sana utamuwekea kwa elfu 5.
Cover nazo unatafuta za Mia nane jumla .utawauzia elfu 5
Kwa ushauri zaidi nicheki saa 5 usiku nikiwa free.hapa Niko busy
Kagera afanye biashara ya Macover ya simu na protector
Ushaur mwingine tuangaliage
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna mtu nilimfungulia hiyo biadhara, kweli isikie tu kwa mtu, sasa hana chochote na kodi anadaiwa ananitegemea mimi wakati na mimi sina kitu
Kabisa Na mind you mimi niliifungua pale Mabibo mwisho kuna population lakini ilinishinda.
Ila wengine wanauza tu
 
Attachments

  • IMG_20241203_121715.jpg
    IMG_20241203_121715.jpg
    311.6 KB · Views: 1
Kabisa Na mind you mimi niliifungua pale Mabibo mwisho kuna population lakini ilinishinda.
Ila wengine wanauza tu
Biashara ina mambo mengi sana, mimi nilimfungulia mbele kidogo ya kibozone, dadeki mwanzoni alianza vizuri na faida alikuwa anaiona ila baada ya muda kashindwa na kafunga anasubiri nimpe mtaji tena wakati sina kitu kwa sasa
 
Kiongozi kwanza pole.

mimi nakushauri kwamba cha kwanza kamwe usitumie hela yako yote kwenye kufungua biashara.

Anzisha biashara yenye kutumia mtaji mdogo kabisa na ambayo haitakusumbua hata kidogo ili kuweza kuhifadhi kiasi kingine cha pesa.

Tumia hela kidogo sana kiasi kisichozidi elfu 35,000 fungua biashara ya kukaanga chapati.

Mtaji Mkuu:
Huu ni mtaji usiorudisha faida. Ni msingi wa biashara yako.

Hotpot-10,000
Kaangio ya chapati-4,000
Sukumio la chapati-7,000
Jiko la mkaa-4,000
Baking Powder-1,000
Chumvi-1,000
Tafuta stuli hapo nyimbani.
Jumla kuu-27,000

Mtaji endeshi:
Huu ni mtaji unaokurudishia faida. Hii itaendesha biashara yako kila siku na ndio wenye kukupa faida.

Ngano kilo 1-2,000
Mkaa-500
Mafuta-1000
Jumla kuu-3500/=

Maelekezo:

a. Katika kilo moja ya chapati toa chapati 20 za chapati na kishauza chapati 2 kwa sh. 500(20Γ·2Γ—500)=5,000 ambayo ni mauzo yote kwa kilo moja.

b. Chukua 5,000 ya mauzo -3,500 ya mtaji = utabakiwa na 1,500 kama faida.

c. Amka asubuhi na mapema sana saa 12 hakikisha unakaanga chapati zako mbele ya unapoishi hapo barabaran wanapopita watu.

d. Hakikisha chapati zako ni nzuri, tamu na yenye kuvutia.

e. Hii biashara inafanywa na jinsia zote. So usiome Soo kuwa wewe ni mwanaume.

Matokeo:
a. Ukifanya vema kwa siku nakuhakikishia kilo 2 za chapati kuisha ni uhakika in which utapata faida ya 3,000 kwa siku.

b. Ukifanya hivo kwa 26 katika mwezi utakuwa na faida ya Tsh. 78,000/=

e. Endelea hivyo hivyo mpka uweze kuuza kilo 4 per day. Hii itategemea ubora wa bidhaa yako, location ya biashara na customer service yako kwa mtaji.

Asante.
 
Blaza mi nina idea kinoma NOMA..
Na nachosema nina uhakika nacho..

Unaweza ukachukulia poa ila mi sina mengi mpeni hilo wazo afanye mi nipo hapa...
Laki 4 inatosha sana, ubaya tu ni kua yeye hana idea yoyote ndo tabu inaanzia hapo...

Watu wa hivi mara nyingi wanataka kuanza kwa ukubwa chochote atachoshauriwa , ila angekua na kitu anakitaka tayar angeanzia hapohapo kwa hizo jiwe nne
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kudaaadeki.....
Ndo nakupanga hvo..
Ukiwa na malengo ya kitu unachotaka kufanya uwezi pata kielea kidgo ukakurupukia biashara utazingua tuu...

Au utatumia mda mrefu ku pambana mpaka kufikia hatua fulani.

Wengi wanaelezea biashara in simple way na kwa bahati bahati tu...
Nyie mnataka mwenzenu aingie loss et laki nne biashara daaah
 
Daaah bro tuendelee tu kutafuta mishangazi na mimjomba 😹
 
Kiongozi kwanza pole.

mimi nakushauri kwamba cha kwanza kamwe usitumie hela yako yote kwenye kufungua biashara.

Anzisha biashara yenye kutumia mtaji mdogo kabisa na ambayo haitakusumbua hata kidogo ili kuweza kuhifadhi kiasi kingine cha pesa.

Tumia hela kidogo sana kiasi kisichozidi elfu 35,000 fungua biashara ya kukaanga chapati.

Mtaji Mkuu:
Huu ni mtaji usiorudisha faida. Ni msingi wa biashara yako.

Hotpot-10,000
Kaangio ya chapati-4,000
Sukumio la chapati-7,000
Jiko la mkaa-4,000
Baking Powder-1,000
Chumvi-1,000
Tafuta stuli hapo nyimbani.
Jumla kuu-27,000

Mtaji endeshi:
Huu ni mtaji unaokurudishia faida. Hii itaendesha biashara yako kila siku na ndio wenye kukupa faida.

Ngano kilo 1-2,000
Mkaa-500
Mafuta-1000
Jumla kuu-3500/=

Maelekezo:

a. Katika kilo moja ya chapati toa chapati 20 za chapati na kishauza chapati 2 kwa sh. 500(20Γ·2Γ—500)=5,000 ambayo ni mauzo yote kwa kilo moja.

b. Chukua 5,000 ya mauzo -3,500 ya mtaji = utabakiwa na 1,500 kama faida.

c. Amka asubuhi na mapema sana saa 12 hakikisha unakaanga chapati zako mbele ya unapoishi hapo barabaran wanapopita watu.

d. Hakikisha chapati zako ni nzuri, tamu na yenye kuvutia.

e. Hii biashara inafanywa na jinsia zote. So usiome Soo kuwa wewe ni mwanaume.

Matokeo:
a. Ukifanya vema kwa siku nakuhakikishia kilo 2 za chapati kuisha ni uhakika in which utapata faida ya 3,000 kwa siku.

b. Ukifanya hivo kwa 26 katika mwezi utakuwa na faida ya Tsh. 78,000/=

e. Endelea hivyo hivyo mpka uweze kuuza kilo 4 per day. Hii itategemea ubora wa bidhaa yako, location ya biashara na customer service yako kwa mtaji.

Asante.
Mkuu jamaa ameomba ushauri wa biashara ya laki4 na nusu, sasa mbona wewe unampa wazo la mtaji wa elfu 35.

Huoni kama unamrudisha hatua 15 nyuma.....!!
 
Huu uzi una Madini mengi sana ila pia unaonesha kabisa uelewa wa watu kuhusu biashara ukoje kwa maana ya uelewa chanya au hasi!

Siwezi kufanya QUOTE yeyote ila kwa ujumla ina aminika kuwa :
Msingi wa kwanza kabisa wa Biashara sio hata mtaji bali ni wazo lako ukijumlisha na Utayari wako ndio vitu vyamsingi kabisa.

Hii haimanishi kuwa mtaji si muhimu No...

Mtaji ni Muhimu ila ukiwa na wazo madhubuti kwanza unaweza kupata mtaji tu bila shaka kabisa kwani kuna watu wanazo pesa ila hawajui wawekeze sehemu gani kwahiyo utapata tu wakupatner nao.
Pia kama hutaki kushirikiana na mtu utaomba tu watu wakushike mkono na wakiona unachokifanya kina mantiki watakusapoti tu kwahiyo Don't dig deeper kupata mtaji kabla ya kwenda deep kwenye Nini unataka kufanya na Mtaji huo na pia ZINGATIA Biashara ina kawaida ya kwenda opposite na unavyopanga at first... Je utakuwa tayari ku persevere!???
 
Back
Top Bottom