Kiongozi kwanza pole.
mimi nakushauri kwamba cha kwanza kamwe usitumie hela yako yote kwenye kufungua biashara.
Anzisha biashara yenye kutumia mtaji mdogo kabisa na ambayo haitakusumbua hata kidogo ili kuweza kuhifadhi kiasi kingine cha pesa.
Tumia hela kidogo sana kiasi kisichozidi elfu 35,000 fungua biashara ya kukaanga chapati.
Mtaji Mkuu:
Huu ni mtaji usiorudisha faida. Ni msingi wa biashara yako.
Hotpot-10,000
Kaangio ya chapati-4,000
Sukumio la chapati-7,000
Jiko la mkaa-4,000
Baking Powder-1,000
Chumvi-1,000
Tafuta stuli hapo nyimbani.
Jumla kuu-27,000
Mtaji endeshi:
Huu ni mtaji unaokurudishia faida. Hii itaendesha biashara yako kila siku na ndio wenye kukupa faida.
Ngano kilo 1-2,000
Mkaa-500
Mafuta-1000
Jumla kuu-3500/=
Maelekezo:
a. Katika kilo moja ya chapati toa chapati 20 za chapati na kishauza chapati 2 kwa sh. 500(20Γ·2Γ500)=5,000 ambayo ni mauzo yote kwa kilo moja.
b. Chukua 5,000 ya mauzo -3,500 ya mtaji = utabakiwa na 1,500 kama faida.
c. Amka asubuhi na mapema sana saa 12 hakikisha unakaanga chapati zako mbele ya unapoishi hapo barabaran wanapopita watu.
d. Hakikisha chapati zako ni nzuri, tamu na yenye kuvutia.
e. Hii biashara inafanywa na jinsia zote. So usiome Soo kuwa wewe ni mwanaume.
Matokeo:
a. Ukifanya vema kwa siku nakuhakikishia kilo 2 za chapati kuisha ni uhakika in which utapata faida ya 3,000 kwa siku.
b. Ukifanya hivo kwa 26 katika mwezi utakuwa na faida ya Tsh. 78,000/=
e. Endelea hivyo hivyo mpka uweze kuuza kilo 4 per day. Hii itategemea ubora wa bidhaa yako, location ya biashara na customer service yako kwa mtaji.
Asante.