Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani

Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani

Ok mficha uchi hazai:::: Kuna plani ya utajiri hapa🤝

BIASHARA YA MTUMBA JUMLA
Hii ni biashara ambayo ninataka kuifanya... Kwanzia mwezi ujao baada ya kuwa nimeifanyia research kwanzia mwezi wa 3 (nikazunguka mikoa 4.... Na kukusanya taarifa za uhakika kutoka field)

👉Mimi sina mtaji mkubwa wa kuwa muuzaji wa jumla ila niliplan kuanza kwa nnavyoweza... Mafanikio yakija lengo n kuwa muuzaji wa jumla

HII NI KWAAJILI YAKO NA YOYOTE MWENYE NDOTO YA KUFANYA BIASHARA MAKINI (Akiona inamfaa aje kushirikiana)

👉Mpaka Sasa nimefikia 75% kuikamilisha hii project nikiwa na maana.....
Teamwork ya kufanya nayo kazi kwa mikoa yote minne (watu wa kuaminika na wenye uhitaji wa kazi)
👉 Namna ya kulinda mtaji na kuleta faida isiyo na shaka (hili nitaeleza kwa ufupi huko chini)
👉 Kazi itafanyika vipi, utaratibu wake tayari upo...
👉Masoko ya uhakika

NAMNA YA KUIFANYA HII BIASHARA KWA MTAJI WA KAWAIDA IKIWA WASHINDANI WAKO ZAIDI YA 60% WANAMITAJI MIKUBWA

Kuna mbinu kadhaa nimeziweka ili kusaidia kukabiliana na hilo tatizo.
1. Kuingia ubia usio kuwa rasmi na store kubwa za Mizigo wenye mtaji mkubwa kwanzia 500m - 1B, hii itafanya pia sisi tusiishiwe mzigo kirahisi
(Aliyekutangulia sio adui yako, unaweza mtumia kuinuka🤝

2. Masoko mengi ndio mkombozi wetu..... Wauzaji wajumla wengi Dar wanafanya biashara kwa namna mbili
👉 Direct ofisini
👉 Online
Sasa kwakuwa wao ndio wanalisha nchi nzima hvyo soko lao kubwa lipo Online....(twende pamoja), Weakness inayowakumba karibu wote ni kuwa matapeli na mawinga wamekuwa wengi, pia hawana ofisi za jumla mikoani🤝
Wengi wanaoagiza mizigo Dar kutoka mikoani ni wafanya biashara wakubwa ambao wao ndio wanawauzia machinga😁
Sasa huu udhahifu ndio faida yetu itaanzia hapo🤝

Soko letu halitoingiliana na soko lao,,, sisi tutaifanya hii biashara kimachinga ili kukuza mtaji haraka pamoja na kukwepa vitu kama kodi za moja kwa moja n.k
(Hapa Kuna maelezo mengi Sana maana masoko ndio moyo wa biashara ulipo🤝🤝

Hapa tutatafuta masoko mengi kadiri iwezekanavyo.... Nguvu kubwa itakuwa hapa (hii sehemu ntadeal nayo mwenyewe,,, pori kwa pori , tutahakikisha tumeliteka soko la mikoani ipasavyo)

3. Tutafungua store yetu ndogo Dar es salaam ambayo itakuwa na connection na store kubwa hapa mjini... Hapo ndo patakuwa headquarter ya ofisi zetu mikoa yote

3.Mikoani kwa kuanza tutaanza na machinga kwanza, hatutokuwa na ofisi rasmi ambapo kila mkoa mahesabu ya chini wawepo machinga 7.... (Sehemu zilizochangamka,,,, hili eneo nnauzoefu nalo maana nimewah kuwa machinga Sana tu kwahyo nnauzoefu)

Minimum ofisi iwe na machinga 20 mikoa yote tutayoanza nayo.... Kazi yao ni kuuza mzigo wa store kwetu kwa Bei ya kutupa ili tukuze mtaji na mzunguko wetu ukue)

Kupata maeneo ya machinga hiyo kazi ndogo Sana kwangu..... Mikoa nilopita
Dodoma 👉 Center yetu Machinga complex
Tanga 👉 Tangamano
Geita👉 Katoro
Dar 👉 headquarter

4. Mikoani huwa kunakuwa na minada sehemu tofauti tofauti...... Team yetu itahakikisha inakamata vizuri meza minadani zisizopungua 10 jumla kwa mikoa yetu ya kazi (hii inawezekana)

MAKADIRIO YA FAIDA NA MAELEZO YA AWALI.
Kwa wasio na uzoefu na hizi kazi... Hali iko hivi
Mtu ukinunua Belo moja la nguo za kike.... Mfano Shifon blouse Grade A kutoka China, unapata kwa 410k, humo ndani kunakuwa na makadirio ya pcs 300- 400, hapo inakuwa ni sawa umenunua kila nguo moja 1400

Baada ya hapo unazichambua kali, medium na lonya (Yani unazitenga kutokana na ubora ili uzipe bei stahiki)

Mwsho Bei zako ziwe kimachinga kabisa.... 5000 (kali kabisa) , 3000 (medium) na 2000 (za kawaida)

Au Kuna mbinu nyingine huwa iko hivi.... Unazimwaga zote kwa Bei g ya 5000, then zikienda zinapungua na wewe unaenda unashusha Bei🤝🤝
Mwsho wa siku belo moja linaweza leta profit ya 800k mpk 700k

(Swala hapa ni technique za biashara, Kuna watu hii biashara imewashinda na wengine imewatajirisha... Kwahyo swala sio mtaji pekee kuna mengi ya kuzingatia)

USHUHUDA: 1. Kwasasa nataka nikaanze hii kitu Tanga..... Huwezi amini pale Tanga mjini kwa wadigo hakuna sehemu wanafungulisha balo za mikoba ya mtumba uhakika

2. Pia machinga wa pale,,, kiatu ambacho dar n 3500 wao 5500 hawakuuzii (sio kwasabb wanapenda Sana pesa, ni kwamba wananunua vitu Bei g all kwa supplier wao

3. Geita pia the same story... Wanauziwa vitu Bei ya rejareja halafu wanaaminishwa ndo Bei ya jumla hiyo


Kwahyo sisi lazima tuwawini... Lengo litakuwa kuuza Kama machinga Bei ya chini Kama wachina (ili mwisho machinga wawe wanakuja kununua kwetu kwa Bei ya jumla🙏)

NOTE: Mzigo wa headquarter lazima uishe kwa namna yoyote ile..... Kwahyo hapo ofisi itakuwa inapata faida mara mbili, kujiuzia mzigo na faida baada ya kujiuzia mzigo


👉 Wafanyakazi 20 au 30 tutawalipaje?
... Watajilipa wao wenyewe, sisi tutawapa mzigo kwa Mali kauli, mfano anapewa pcs 20 za blauz kwa Bei ya 2500
Yeye ataenda kuuza 5000 au 4000 au 3000 (cha juu chake🤝)
Kwastayl hii tunaweza kuwa na wafanyakazi hata 1000

👆👆👆 Hii ndio mbinu anayoitumia azam kwenye biashara yake ya ice cream..... Wale wanaozunguka dar na madeli pia wanalipwa hivyo kwa commission kadiri anavyouza Sana ndivyo anaingiza Sana... Hapo unaongeza uchapakazi na kuua roho ya uvivu


hsanteni na karibuni🤝🤝. Uandishi najua sio mzuri na moangilio sio wa kisomi ila tuvumiliane.... Kama unaswali uliza au ukitaka tuishi kwenye hayo malengo karibu
Dah,
Inaelekea hiyo sekta unaijua vizuri broo, ila naomba kuuliza:-
hivi wale wauzaji wa mitumba wanaokuwa na mzigo wa tai tupu au chupi pekee, au rundo la soksi peke yake.. huwa wamechagua hizo vitu au wanakuwa wamebambikiziwa na wauzaji wa jumla?
 
Habari wana jf

Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani ambayo inaingiza kipato kizuri kwa siku ambayo haitaniletea hasara?
Kama hujawahi kufanya biashara tafuta partner kwenye biashara iliyoanza au franchise ili ujifunze biashara kisha uongeze mtaji. Vinginevyo kama ndio unaanza jipange kwa lolote litakalotokea.

NB: usitumie mtaji wote, weka akiba kiasi fulani kama asilimia 40
 
Dah,
Inaelekea hiyo sekta unaijua vizuri broo, ila naomba kuuliza:-
hivi wale wauzaji wa mitumba wanaokuwa na mzigo wa tai tupu au chupi pekee, au rundo la soksi peke yake.. huwa wamechagua hizo vitu au wanakuwa wamebambikiziwa na wauzaji wa jumla
Huwa wamechagua wao wenyewe.... Kwasababu belo zipo kila aina.
Kuna viatu, chupi, tai, nguo, mikoba,,,, yani kila kitu cha mtumba!!!

Sasa ukiona mtu amepata mzigo tofauti na alichokikusudia tatzo hapo linakuwa ni sehemu aliyochukulia mzigo..... Wengi wenye kesi za hivi huwa wameagiza online🤝

Hapo kwa lugha fundi kakutana na winga alojifanya muuzaji wa jumla, wengine huwa wanakutana na changamoto ya kutumiwa mzigo outdated au low quality.... Yote hayo yapo kweny hii biashara

Maana belo linakuwa limefungwa hujui ndani kuna nn... N kama kubet bro🚶🚶
 
Habari wana jf

Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani ambayo inaingiza kipato kizuri kwa siku ambayo haitaniletea hasara?
Kwanza lazima utambue kwamba hakuna business au hata investment isiyokuwa na hasara na kama hutak kukutana na hasara au changamoto wewe sio mfanyabiashara na utaangukia pua.
 
Back
Top Bottom