Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani

Dah,
Inaelekea hiyo sekta unaijua vizuri broo, ila naomba kuuliza:-
hivi wale wauzaji wa mitumba wanaokuwa na mzigo wa tai tupu au chupi pekee, au rundo la soksi peke yake.. huwa wamechagua hizo vitu au wanakuwa wamebambikiziwa na wauzaji wa jumla?
 
Habari wana jf

Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani ambayo inaingiza kipato kizuri kwa siku ambayo haitaniletea hasara?
Kama hujawahi kufanya biashara tafuta partner kwenye biashara iliyoanza au franchise ili ujifunze biashara kisha uongeze mtaji. Vinginevyo kama ndio unaanza jipange kwa lolote litakalotokea.

NB: usitumie mtaji wote, weka akiba kiasi fulani kama asilimia 40
 
Dah,
Inaelekea hiyo sekta unaijua vizuri broo, ila naomba kuuliza:-
hivi wale wauzaji wa mitumba wanaokuwa na mzigo wa tai tupu au chupi pekee, au rundo la soksi peke yake.. huwa wamechagua hizo vitu au wanakuwa wamebambikiziwa na wauzaji wa jumla
Huwa wamechagua wao wenyewe.... Kwasababu belo zipo kila aina.
Kuna viatu, chupi, tai, nguo, mikoba,,,, yani kila kitu cha mtumba!!!

Sasa ukiona mtu amepata mzigo tofauti na alichokikusudia tatzo hapo linakuwa ni sehemu aliyochukulia mzigo..... Wengi wenye kesi za hivi huwa wameagiza online🤝

Hapo kwa lugha fundi kakutana na winga alojifanya muuzaji wa jumla, wengine huwa wanakutana na changamoto ya kutumiwa mzigo outdated au low quality.... Yote hayo yapo kweny hii biashara

Maana belo linakuwa limefungwa hujui ndani kuna nn... N kama kubet bro🚶🚶
 
Habari wana jf

Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani ambayo inaingiza kipato kizuri kwa siku ambayo haitaniletea hasara?
Kwanza lazima utambue kwamba hakuna business au hata investment isiyokuwa na hasara na kama hutak kukutana na hasara au changamoto wewe sio mfanyabiashara na utaangukia pua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…