Nina mtaji wa milioni 6 nataka nianze biashara ya bodaboda

Achana na biashara kichaa hio, kwa hela hiyo vuta toyo au bajaj ukomae mwenyewe. Ukosi 50 kwa siku.
The best ni toyo ya mizigo paki sokoni ukiwa na wateja wako wawili tu watu wa magengeni uhakika. Nidhamu ya Kazi, uharaka, uaminifu, networking, tengeneza group lako la wasap la wateja wako, pesa utazikimbia.
 
Sikushauri biashara ya boda bora ungeniambia uwe wakala wa kuziuza sio wewe uwe boss na mafuta haya yanavyopanda utakula maumivu zitagegeduliwa siku ikirudishwa imeshachakaa na hela hujapata wewe cha kufanya anzisha mradi mdogo wa kulima mchicha au fungua duka la bidhaa na nafaka zisikosekane.

Au kama una eneo lipo free hulipii anzisha mradi wa nguruwe ukiwa na nguruwe wako wawili tu dume na jike na banda la kawaida la gharama nafuu unaweza anzisha kitu ambacho kitakuwa kwa kasi na nguruwe analika sio nyama ya kudoda.
 
Asante kwa ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…