Nina mtaji wa milioni kumi; nifanye biashara ipi kati ya hizi nilizochagua?

Biashara huwa inaanzia na wazo na ukiwa nje ya biashara mara nyingi huwezi kujua biashara ipi inalipa.kwa tathimini yangu toka nianze biashara naona ukitaka biashara yako iende vizuri kuwa na WAZo ambalo hu deal direct na final consumer ,yani uwe na biashara ambayo unaweza kuwauzia wafanya biashara wa jumla na rejareja nje ya hapo biashara utaiona ngumu sana hasa ya ku deal na wateja wa rejareja njoo pm nikupe wazo ambalo utakula hela
 
Kwa uzoefu wako inabdi km kiasi gani kinahitajika..?
Kwa uzoefu wangu, japo inategemea sana unataka kuweka nini kwa kuanzia, ila kama haitahusisha mbao, cement, nondo na vifaa visivyotoka haraka, unaweza kuanza na 15m hadi 20m. Na hapo utakuwa umejibana sana, labda kama ndio kujikongoja hivyo, ila kwa serious business 10m kwenye vifaa vya ujenzi haitoshi, ila kwenye uwekezaji mwingine ni pesa ndefu tu.

Mfano, kama utauza bomba za kuchomelea na accessories zake, yaani sticks, disks, rangi, vitasa vya mageti, bawaba za geti, sheets za urembo nk utashangaa hiyo 10m inakata na mzigo ni mdogo sana.
 
Ukiandika hapa wote tukafaidi mawazo yako je?
 
Anzisha danguro, hakikisha mademu wote ni weupe na wana matako makubwa...
 
Ni sahihi Mkuu, ila kwa kiasi alichonacho cha milioni 10 nadhani haitatosha labda kama anaweza kuanza kuwa dealer wa Saruji na vifaa vichache vya Plumbing

Maana ukiagiza mifuko 300 ya Saruji utatakiwa kuwa na shilingi 4,576,000 hapo ukiagiza kiwandani
 
Kwanini...?
Mambo ya
Business proposal
SWOT
E.t.c
Naonaga ujinga tuuu...
Sawa niliyasoma chuo ila niliyakariri ili nifaulu darasani ila ukija mtaani ukitaka kutoboa....
1. Anzisha biashara
2. Weka bei kama ulizozikuta sokoni
3. Soma MCHEZO ukiwa mchezoni
4. Tafuta taarifa field
5. Tafuta waliokutangulia wakuongoze na kukupa hint

Makaratasi na mambo hayo ya darasani TUPA HUKOOOO

#YNWA
 
Biashara zote hapo zinawezekana kasoro ya vifaa vya ujenzi mtaji wako ni mdogo.
Ya vyombo vya nyumbani naikataa, haina mzunguko mkubwa inataka location nzuri zaidi kuliko hizo nyingine.

Ya small electronics, gadgets na accessories ina mzunguko mkubwa zaidi. Ila kila biashara inataka upewe codes zake kabla ya kuingiza mtaji mazima.
 
Nakuja chap japo ungeandika hapa pia ingependeza zaidi...
 
Hapo nmekupata mkuu unaonekana mzoefu ww kwny septa ya ujenzi..
 
Namba 5.[emoji871]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…