Kama Huna Any Support System (Back Up Ya Ajira, Asset Yako Iwe Ya Kurithi au Yako Mwenyewe Inayokuingizia Hela, Back up ya kazi / biashara za wazazi)
Fanya Yafuatayo Regardless Umesoma Au La
1. Swallow ur pride usijione kama wewe ni wa kufanya kazi za aina flan (za kisomi) pekee.
2. Nunua Smartphone Kali
3. Nunua Bajaj Used iliyo on mint condition Sajili Bolt, Uber, Taxify and the likes. Kama salio likiruhusu funga mfumo wa gas
4. Ukiwa na hicho chombo chako cha usafiri jihusishe na udalali wa vitu tofauti tofauti magari, apartments za kupangisha na vyumba ya hotels or lodges, viwanja (from clean sources)
5. Always be open minded, ukiona au kuletewa fursa hata kama huna interest nayo ipokee sikiliza na ujifunze. Kama huna mpango nayo weka information akilini itakusaidia one day. Binafsi Nina ushahuda na hili.
Utanishkuru baadae kama we ni msomi ukija shoboka na ajira za hata 2 M take home kwa mwezi niite mbwa. Nimekaa pale [emoji1428]
Exposure utayopata kwenye hzo mishe itakufungua kwenye mambo mengi sana. Biashara ulizotaja ni nzuri ila kwa mtaji huo kupoteza ni rahisi sana. Ukiwa serious 150k unafunga daily….umekosa sana 100k (Yes its possible maana huna boss chombo ni chako mwenyewe)
Kaa fikiri wenye viduka vya mangi wanafunga net profit 100k - 150k daily yet wanaweza jiongeza na kuwa exposed na mazingira ya hela tofauti wakiwa kazini ??
Wapo vijana wengi nawajua wametoka chuo hawana mishe wanajiongeza na hzo mishe wanapata na ujasiri wa kuanzisha na familia na wengine hata kununua viwanja. Service ya bajaji sio kubwa wengi wana request bajaji kuliko magari. Achia mbali wateja wa offline.
Well Mtazamo Tu, All The Best [emoji817]