Baba Ndubwi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 1,223
- 1,992
Ila sio vibaya kuanza na ng'ombe wachache huku ukiendelea kuongeza uzoefuKanitisha sana aisee
Madalali jau sana sometimesna hawa daima huwa ndio wanaofelisha biashara za watu. Tamaa za madalali unaweza jikuta ukahisi una nuksi.
Nitafanya kwenda pugu mnadaniKabla hujaingia kichwa kichwa nenda kafanye utafiti mwenyewe huko Pugu kaa hata wiki uone namna mifugo inavyoingia na kuuzwa
Angalia wakifika, wanafikishwa wapi na wanalipa ngapi kwa kuwapumzisha na chakula pamoja na maji
Je madalali wakoje
Kuna changamoto nyingi sana katika hiyo biashara
Ila ukipambana na kuzijua ABC basi huna shida, ila usiingie kichwa kichwa
Lazima ujue bei zake pia kama zinalipa
Sawa mkuuMkuu karibu.
Nilishafanya ya mbuzi mwaka 2018 na hao kidogo.
Hiyo pesa kwa ng'ombe halitoshi labda uanze kwa kuunga kwa mzoefu.
Kuna gharama nyingi kama:
-Kupiga kambi ya manunuzi(Centre)
-Ukusanyaji na uswgaji toka minadani(Wapo unawalipa)
-Kuzunguka kwenye minada(Wasaidizi utawakuta huko)
-Malisho ya hao ambao ushawanunua(Utanunua nyasi au mashudu)
-Malipo ya uhifadhi na mlinzi
-Matibabu kwa watakaopata homa
-Upakiaji na Usafirishaji
-Ushuru na vibali vingine
-Machawa nao wamo(watoa miongozo)
NB:Nenda pale mabibo mwisho mtafte tajiri mmoja anaitwa Halubu
Sijataka kuweka pesa yote nimeona nianze na mtaji huoIla sio vibaya kuanza na ng'ombe wachache huku ukiendelea kuongeza uzoefu
Laki Tatu na kuendelea,,, kama wa kunenepesha wazuri ni wa laki 5hadi 7,ili uje kuuza milioni na zaidi, baada ya kunenepeshaWasukkuma mnaitwa huku
Mwekezaji kaja anawataka uwanjani
Shukrani mkuuLaki Tatu na kuendelea,,, kama wa kunenepesha wazuri ni wa laki 5hadi 7,ili uje kuuza milioni na zaidi, baada ya kunenepesha
Dalali wanaweza kukupa taarifa vizuri siku ukileta mzigo wa kakukwamisha.Duh kiaje mkuu?
Duh naona bora nifikilie biashara nyingine aiseeDalali wanaweza kukupa taarifa vizuri siku ukileta mzigo wa kakukwamisha.
Kwa kifupi tafuta mtu anaejua kumtathiminisha ng'ombe ambaye akimuona anajua ana kilo ngapi hapo unaweza kupata faida kinyume na hapo utapata shida sana.
Hiyo kazi inachangamoto nyingi.
Unaweza kununua ng'mbe mikoani ukafikisha Pugu ukakuta bei imeshuka. Tofauti na hapo Kuna mda ng'ombe wanakufa au kukimbia;
Kuna jamaa alowahi kupata hasara mpaka akawa analia na alikuwa mzoefu.
Shukrani mkuu naona nifikirie biashara nyingineBinafsi sikushauli, biashara ya ng'ombe mbuzi ina changamoto nyingi sana ktk kununua na kuuuza hasa cku za mwanzo utakutana na changamoto nyingi sanaaa , usipokuwa makini unaweza kata mtaji wako, unaweza ukanunua ng'ombe kwa laki 8 ukaja sokoni wakakuambia huyu ni laki saba, yaani changamoto ni kubwa sanaaa,
Milioni 20 inatosha kuashisha duka kuuubwa ukauza jumla na reja reja alafu maisha yakaenda bila kutoa jasho jingiii, kama utaitaji mchnganuo wa biashara nyingine karibu mp rafiki
Mkuu kabla ya yote nenda Mnada wa Ngombe pugu Ujuwe Bei ya kuuzia Then njoo Utembelee minda ya Wilayani KITETO husisani Mnada wa Dosi Dosi tarehe 01/14 Kwa mwezi mara mbili na Mnada wa Kibaya 02/15. Bei za Ngombe kipindi hichi zipo chini sana, Nakushauri ununue Ng'ombe 50 Kwa laki 4 Kwa Moja, unawanenepisha Hadi mwezi wa Tisa/(09) Unawauza Kwa Milioni Hadi Milioni na laki nne,Nawasalim kwa jina la muungano!! ,
Wakuu nina mtaji wa 20m nataka nianze biashara ya ng’ombe kutoka mikoani nakuleta Pugu DSM, naomba kujua ABC za hii biashara na kama inalipa au lah
Kaka umetishaUtakuja nishukuru lkn swala LA kuleta ng'ombe mjini acha kabisa ni sawa na kutupa hela yako
Nunua mbuzi wa elfu stini stini utapata zaidi ya mbuzi mia tatu peleka Comoro. Lakini Fanya utafiti kwanza ila ukifanikiwa kupeka mara tatu tu wewe ni tajiri.