Nina mtaji wa Tsh Milioni 20, nataka kufanya biashara ya ng'ombe

Nina mtaji wa Tsh Milioni 20, nataka kufanya biashara ya ng'ombe

Mkuu karibu.
Nilishafanya ya mbuzi mwaka 2018 na hao kidogo.
Hiyo pesa kwa ng'ombe halitoshi labda uanze kwa kuunga kwa mzoefu.
Kuna gharama nyingi kama:
-Kupiga kambi ya manunuzi(Centre)
-Ukusanyaji na uswgaji toka minadani(Wapo unawalipa)
-Kuzunguka kwenye minada(Wasaidizi utawakuta huko)
-Malisho ya hao ambao ushawanunua(Utanunua nyasi au mashudu)
-Malipo ya uhifadhi na mlinzi
-Matibabu kwa watakaopata homa
-Upakiaji na Usafirishaji
-Ushuru na vibali vingine
-Machawa nao wamo(watoa miongozo)
NB:Nenda pale mabibo mwisho mtafte tajiri mmoja anaitwa Halubu
 
Kabla hujaingia kichwa kichwa nenda kafanye utafiti mwenyewe huko Pugu kaa hata wiki uone namna mifugo inavyoingia na kuuzwa

Angalia wakifika, wanafikishwa wapi na wanalipa ngapi kwa kuwapumzisha na chakula pamoja na maji
Je madalali wakoje

Kuna changamoto nyingi sana katika hiyo biashara
Ila ukipambana na kuzijua ABC basi huna shida, ila usiingie kichwa kichwa

Lazima ujue bei zake pia kama zinalipa
Nitafanya kwenda pugu mnadani
 
Mkuu karibu.
Nilishafanya ya mbuzi mwaka 2018 na hao kidogo.
Hiyo pesa kwa ng'ombe halitoshi labda uanze kwa kuunga kwa mzoefu.
Kuna gharama nyingi kama:
-Kupiga kambi ya manunuzi(Centre)
-Ukusanyaji na uswgaji toka minadani(Wapo unawalipa)
-Kuzunguka kwenye minada(Wasaidizi utawakuta huko)
-Malisho ya hao ambao ushawanunua(Utanunua nyasi au mashudu)
-Malipo ya uhifadhi na mlinzi
-Matibabu kwa watakaopata homa
-Upakiaji na Usafirishaji
-Ushuru na vibali vingine
-Machawa nao wamo(watoa miongozo)
NB:Nenda pale mabibo mwisho mtafte tajiri mmoja anaitwa Halubu
Sawa mkuu
 
Binafsi sikushauli, biashara ya ng'ombe mbuzi ina changamoto nyingi sana ktk kununua na kuuuza hasa cku za mwanzo utakutana na changamoto nyingi sanaaa , usipokuwa makini unaweza kata mtaji wako, unaweza ukanunua ng'ombe kwa laki 8 ukaja sokoni wakakuambia huyu ni laki saba, yaani changamoto ni kubwa sanaaa,

Milioni 20 inatosha kuashisha duka kuuubwa ukauza jumla na reja reja alafu maisha yakaenda bila kutoa jasho jingiii, kama utaitaji mchnganuo wa biashara nyingine karibu mp rafiki
 
Duh kiaje mkuu?
Dalali wanaweza kukupa taarifa vizuri siku ukileta mzigo wa kakukwamisha.

Kwa kifupi tafuta mtu anaejua kumtathiminisha ng'ombe ambaye akimuona anajua ana kilo ngapi hapo unaweza kupata faida kinyume na hapo utapata shida sana.

Hiyo kazi inachangamoto nyingi.

Unaweza kununua ng'mbe mikoani ukafikisha Pugu ukakuta bei imeshuka. Tofauti na hapo Kuna mda ng'ombe wanakufa au kukimbia;

Kuna jamaa alowahi kupata hasara mpaka akawa analia na alikuwa mzoefu.
 
Duh naona bora nifikilie biashara nyingine aisee
 
Binafsi sikushauli, biashara ya ng'ombe mbuzi ina changamoto nyingi sana ktk kununua na kuuuza hasa cku za mwanzo utakutana na changamoto nyingi sanaaa , usipokuwa makini unaweza kata mtaji wako, unaweza ukanunua ng'ombe kwa laki 8 ukaja sokoni wakakuambia huyu ni laki saba, yaani changamoto ni kubwa sanaaa,

Milioni 20 inatosha kuashisha duka kuuubwa ukauza jumla na reja reja alafu maisha yakaenda bila kutoa jasho jingiii, kama utaitaji mchnganuo wa biashara nyingine karibu mp rafiki
Shukrani mkuu naona nifikirie biashara nyingine
 
Nawasalim kwa jina la muungano!! ,

Wakuu nina mtaji wa 20m nataka nianze biashara ya ng’ombe kutoka mikoani nakuleta Pugu DSM, naomba kujua ABC za hii biashara na kama inalipa au lah
Mkuu kabla ya yote nenda Mnada wa Ngombe pugu Ujuwe Bei ya kuuzia Then njoo Utembelee minda ya Wilayani KITETO husisani Mnada wa Dosi Dosi tarehe 01/14 Kwa mwezi mara mbili na Mnada wa Kibaya 02/15. Bei za Ngombe kipindi hichi zipo chini sana, Nakushauri ununue Ng'ombe 50 Kwa laki 4 Kwa Moja, unawanenepisha Hadi mwezi wa Tisa/(09) Unawauza Kwa Milioni Hadi Milioni na laki nne,
Bei ya kukodi eneo la malisho haezidi laki Tano, Mchumgaji ni Elfu sabini Kwa mwezi unaweka wawili,. Kwanzia mwezi wa Saba unanunuwa mabua masjambani unawalisha wanenepe, mabua ekari mia ni laki Saba, wanakula Hadi mwezi wa kumi.
Siwezi kueleza yote , wewe njoo ujifunze kwanza then ndio ufanye biashara. Njoo na nauli tu na gharama za lodge, ujifunze tutakupa watu wanaofanya hiyo kazi uone ugumu na changamoto zake zilivyo nyingi
 
Nunua mbuzi wa elfu stini stini utapata zaidi ya mbuzi mia tatu peleka Comoro. Lakini Fanya utafiti kwanza ila ukifanikiwa kupeka mara tatu tu wewe ni tajiri.
 
Kwa pesa hiyo sio ndogo kwamaana kuna watu wananunua ngo'mbe 10 wanakuja wanawauza kisha wanafuata wengine na maisha yanakwenda vizuli . Unaweza kuanza lkn kabla ya yote fanya kwanza ujue soko nk . Nimekupa wazo la biashara yako, sasa tutoke hapo boss

Bonafsi sikushauli kufanya biashara hiii kwa maana ina changamoto nyingi sana, kama unataka biashara ya kusafili , nenda kanunue mahindi, maharage lete dar , utauza, peleka manze pale madalali wanakupa mteja unaenda unauza, maharade unaweza peleka tandika nk ..

Lkn kuna biashara nyingi ambazo kwa mtaji wako unaweza fanya tu, kuna jamaa ana mtaji wa milion 10 , tigo pesa, m-pesa, nmb wakala ,crdb wakala nk , kwa mwezi anapata faida ya milioni 2. Kuna mtu ana mtaji wa milioni 4 anafanya biashara ya kuuza vinywaji lain julma na reja reja, soda maji, juic nk kwa mwezi anapata faida ya laki 9.

, nimekupa mchanganuo huo, lkn kuna biashara moja siwezi weka hapa njoo mp nikulishe madini,
Ng'ombe watakufilisi
 
Duuuh! nilikua nawaza kuanza kununua mbuzi nasafirisha,ila michango ya humu inaogopesha sana.
 
Back
Top Bottom