Nina ndoto ya kufikisha miaka 100 ya kuwa hai duniani

Jikite kwenye kuomba rehema za Mungu tu, maana ni yeye pekee mwenye kuamua nani aishi ama yupi afe.

Kucheki afya hospitalini pamoja na kuzingatia mifumo ya afya Kwa Ujumla sio tiketi ya wewe kuishi miaka 100.

Wazee wetu akina Nyerere, Ben Mkapa, Mzee Mwinyi, JPM hao wote walikuwa wakipata matibabu ya Daraja la kwanza, lakini haikusaidia, hakuna kati yao aliyefika miaka 100 πŸ™Œ

Tunaishi kwa Neema tu πŸ™πŸ™
 
Nifanye nini ili nitimize ndoto hiyo ukiachana na kuomba Mungu !!!
Unachosema kinaendana na mtazamo wa wengi wanaoamini kuwa afya na maisha vyote viko mikononi mwa Mungu.

Ni kweli kwamba matibabu ya kisasa, mazoezi, na kuzingatia afya ni mambo muhimu ambayo yanaweza kusaidia kuimarisha afya yetu, lakini mwisho wa yote, mambo haya hayawezi kuzuia kifo au kuhakikisha maisha marefu.

Mifano ya viongozi kama Mwalimu Julius Nyerere, Benjamin Mkapa, na wengine waliopata huduma bora lakini wakafikia mwisho wa safari zao za maisha, zinaonyesha mipaka ya uwezo wa kibinadamu.

Imani na kumtegemea Mungu ni kielelezo cha kuelewa kwamba rehema na neema zake ndizo zinatuwezesha kuishi kila siku.

Kila mtu anaweza kufanya jitihada za kuhifadhi afya, lakini imani inatufunza kwamba Mungu ndiye mwenye neno la mwisho. Kwahiyo, kuomba rehema na kuishi kwa shukrani ni muhimu, tukikumbuka kwamba uhai ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
 
Miaka yote hiyo ya nini..
Mtu unafikisha umri unakuwa wakuanikwa juani kama mpunga na jioni wanakuimgiza ndani, kesho asubuhi wanakuanika tena.

We miaka 100 hata nguvu ya kutomber huna, unaishi ili iweje, starehe nambari UNO duniani ni kwichi kwichi.

Sitaki nifike huko.
 
hakikisha unakuwa na vyanzo vya pesa ambavyo havitakupa stress, ardhi,nyumba,kilimo,ufugaji ukiweza kuviweka sawa hivi umeanza kufaulu!.

hakikisha ulaji wako ni salama,zingatia ulaji mzuri natural ktk vingi unavyovitia mdomoni mwako
kiujumla zingatia afya yako pia mazoezi walau yakukutoa jasho,usikae kizembe!.
makazi yako nashauri yawe kijijini,sio kijijini sana kuwe na upatikani wa huduma za kijamii zote!.
weka mbali mtu ambae ni hatari kwako, nawe uishi kwa upendo na wengine kikubwa kuwa halisi!.

pombe,sigara futa hivyo vitu!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…