Inawezekana kabisa. Ali Hassan Mwinyi alifikisha 98.
Jitahidi, pamoja na masuala mengine ya msingi kama mazoezi, ule angalau apple mbili kila wiki, utakuja kunishukuru.
1. Dhibiti kabisa kiwango cha uzito wako (maana yake uzingatie sana mlo wako). Watu wengi wanaanza kwanza kufa tumboni kabla ya kufa nafsini. Sijui unanielewa?
2. Akili yako isiwe na msongo kupitiliza na wala isikae bila kazi yoyote (kumbuka kwamba msongo ni mzuri kama hauvuka wastani wake.)
3. Jijenge kiroho, kimwili, kitaalama, kijamii, kiuchumi na kimkakati.
4. Jihadhari na pollutions - noise, light pollution, dust/air, media, psychological, etc.
5. Jiulize kila siku sababu ya kuishi - unategemea kuacha alama gani duniani? Ukipewa miaka 100, mwingine akapewa 30, kuna tofauti? Usiishi ili tu ishie baadaye, bali ishi ili uishi daima. Sijui unanielewa?