Nina ndoto ya kufikisha miaka 100 ya kuwa hai duniani

Nina ndoto ya kufikisha miaka 100 ya kuwa hai duniani

Waefeso 6:2-3​

“Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”
Amri ya tano inasema, “Waheshimu baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako” ( Kutoka 20:12 )
Sasa kama mama hawapo amheshimu nani
 
Naona kama kuishi mda gani ni jambo la kurithi pia kutoka kwa kizazi chenu🤔 japo haina garentii
Shubamiiit, kuna koo unakuta bibi kaona vimbwele. Yaani mama wa babu yupo hai na anapenda ugoro na tumbaku kuliko kula.
 
Ni kwa neema ya Mungu tu hakuna ndoto na wala si takwa lako au juhudi zako kama Mungu kakupangia 100 utatoboa na kama hujapangia sahau
 
Habari Wadau see

Mimi nina miaka 27 na ninataka nife nikiwa na umri wa miaka 100 hivi 😁

Yaani niishi hadi mwaka 2100

Nifanye nini ili nitimize ndoto hiyo ukiachana na kuomba Mungu?
utakuwa umeifanyia nini dunia katika hiyo miaka 100, legacy wise?
 
Shubamiiit, kuna koo unakuta bibi kaona vimbwele. Yaani mama wa babu yupo hai na anapenda ugoro na tumbaku kuliko kula.
Mimi bibi yangu ana 104 na alikua mtu wa pombe kali 😂
 
Sasa ukiachana na kuomba Mungu hapo unategemea nini?kuishi miaka mingi hata hiyo 100 ni neema kutoka kwa Mungu,ni yeye pekee ndio mwenye uwezo wa kuiachilia kwa mtu amtakaye.Kama ilivyokuwa kwa Hezekia,soma 2Wafalme 20:2-6...
Umenena vyema sana mtu wa MUNGU.
 
Usijiulize nitaishi miaka mingapi duniani. Jiulize nitaifanyia nini dunia mpaka nitakapoondoka duniani.

NB: Kufa siyo hoja, hoja ni hali ya uhusiano wako na Mungu wako pindi ambapo muda wa kuwa hai duniani utakapo koma.
Na hii ndio maana halisi ya maisha,ndo mana maandiko yanasema "heri wafu wafao katika bwana tangu sasa."
 
Ata ukiishi miaka buku,kama maisha yako ni ya ovyo ovyo na huna MUNGU ndani yako bado utaishi miaka hyo kwa mateso sana,na utatamani kifo kikujie lakn kitakukwepa,mjue sana MUNGU uwe na amani,wana amani nyingi wale waipendao na kuishika sheria za MUNGU.
 
Habari Wadau see

Mimi nina miaka 27 na ninataka nife nikiwa na umri wa miaka 100 hivi 😁

Yaani niishi hadi mwaka 2100

Nifanye nini ili nitimize ndoto hiyo ukiachana na kuomba Mungu?
Miaka 100 utakuja kupata shida uteseke bure.
Kwepa kuuawa na watu ila usikwepe kuchukuliwa na Mungu kwenye umri stahiki. Maximum miiaka 95 ni recommended. 100 hapana, labda Mungu aseme mwenyewe
 
Back
Top Bottom