Nina nyumba uswahilini inatengeneza Tsh. 40,000/- kwa mwezi, niendelee au napoteza muda?

Kiuze Tu hutakosa mtu anaekitaka..hiyo pesa kanunue kiwanja kikubwa sehemu
 
Mkuu, mali ndo huleta fedha, Biashara hazifanywi na pesa za mfukoni. Biashara zinafanywa na pesa za watu wengine kupitia mabank, kama unauhakika na biashara unaenda bank unakopa ila Vijana hawakopesheki sababu ya mawazo kama haya, hawataki kuwa na mali ila wanataka kuwa na fedha.

Kama una M90 yako na una ardhi. Kata title, jenga nyumba zako za kupanga, weka wapangaji. Kama una uhitaji pesa nenda bank peleka hati chukua mkopo fanya biashara. Hao wapangaji watakupa kodi itakusaidia kupunguza marejesho.
 
Hayo mawazo mawili yote mazuri.
Ila hilo la kwanza utakuwa unamsaidia Ibilisi kueneza zinaa
 
Benk hawakubali labda uniambie benk gan wanakubali ??
mfano NMB: Wanatoa mkopo wa biashara lakin biashara ndo kipaumbele kiwanja au nyumba ni mdhamana tu.
Mkuu, Fungua akaunt, jipe miezi 6 ya kupitisha fedha bank kidogo kidogo iingie na kutoka, kata leseni hata ya uuzaji malimao au angalia ni biashara gani unaweza isemea kuwa unafanya hata kama huifanyi kikamilifu. Hiyo 40 ya kodi ukipambana ukaongeza zako ukawa unaingiza inakaa siku moja mbili ukaitoa ni mzunguko mzuri tu wa kuanza kukopeshwa m1, 2 mpaka hata 5. Jiongeze boss.
 
Kigeuza kuwa ,kibanda umiza,Yani sehemu ya kuangalizia mechi ,za ligi kuu bara,na nyingine za ulaya ,asa premier league ,la Liga ,na league ya Italy na Saudi league pro ,utalidisha Hela Yako chapu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…