Nina nyumba uswahilini inatengeneza Tsh. 40,000/- kwa mwezi, niendelee au napoteza muda?

Nina nyumba uswahilini inatengeneza Tsh. 40,000/- kwa mwezi, niendelee au napoteza muda?

Sasa kasema nyumba ipo kati, imezungukwa na mijengo pande zote nne, na kila kajenga hajaacha hata uchochoro,
Angalia hii imekaa kwenye ardhi ndogo tu lakini inatosha kwa familia hata 4

Ni ubunifu tu na hela kama ipo
Mimi ningefanya hivyo ila kwa hii ni ndefu kidogo maana moja inatosha
Screenshot_20231012_093707_Google~2.png
 
Hii hesabu haina ukweli labda umeamua kupotosha ama haujui


Utt wanatoa faida ya asilimia moja kwa mwezi kwa kiwango ulichowekeza
Hivyo hiyo million tano utapata elfu hamsini na sio elfu sitini uliyoandika

Mi mwenyewe nikajua kuna benki huko inatoa riba kwa bei kubwa na hamniambii
 
Najua kuna mnaofanya hii biashara na inawalipa sana. Kama inakulipa basi ni ether;
1. Unapangisha fremu za maduka (kama location n nzuri au barabarani)
2. Wenye apartment katikati ya mji
3. Wenye biashara ya guest/lodge au hoteli

Kwa upande wangu, nina nyumba ndogo sana vyumba 2 na sebule na kimoja cha nje. Nilikinunua hiki kibanda mwaka 2019 kwa milioni 5.[emoji3064]

Kipindi hiko sina nyumba nilikurupuka kutaka kumiliki atlest kijumba mjini. Kina sehemu ndogo sana. Yaani huwezi kujenga wala kuendeleza kitu kingine kimebanana sana mahali ilipo imezungukwa na majirani ambao nao kila mmoja amejenga hadi mwisho wa uwanja wake.

Nikaanza kupangisha. Bei za huku kwasababu hamna umeme hamna maji basi bei ni elfu 10.
Sasa kwa hii elfu 10 nawaza hadi sasa 2023 sijafikisha hata laki 3 au 5 niliopokea kwene hiki kijumba.

Natamani kukiuza lakini hakiuziki. Naona hata uvivu kukikarabati maana nitapoteza hela tena.

Nawezaje kuongeza thaman ya hiki kijumba muda unaenda?

Mawazo yanayonijia;
1. Nikifanye guest (changamoto ni kadogo, kako katikati ya uswazi labda nilale mwenyewe).
2. Niweke hata mashine? Sielewi!

Toa ushauri jinsi wewe ulivyoongeza thamani ya nyumba yako, au unavoweza kupiga hela kupitia kijengo.
Ii
 
Back
Top Bottom