Nina samaki aina ya sato, nipe soko

Nina samaki aina ya sato, nipe soko

Gumasa

Member
Joined
May 10, 2023
Posts
32
Reaction score
32
Habarini za majukumu ndugu wadau wa JF.

Ninafanya biashara ya kuuza samaki aina ya sato. Size ya samaki wanaopatikana kwa wingi kwa sasa ni wale wanaovuliwa katika nyavu ya nchi 4 mpaka nchi 4.5.

Kama kuna mdau anafanya hii biashara ya samaki mahali popote na angependa kupata mzigo kutoka kwangu namkaribisha sana.

Nina uwezo wa kukuanzia samaki wengi kulingana na mahitaji yako, hata kama utahitaji piece 1000.

Mauziano ni keshi mkononi, maana yake unahesabu mzigo wako kulingana na makubaliano then unakabidhi hela mkononi. Hiyo ndiyo heshima na nidhamu ya fedha ili tuepuke kurogana na kuuana kabisa.
 
Nimekusoma sana Mkuu Wangu.
Nina uzoefu Sana na Ziwani
1000 pieces ni sawa na Tani Moja au Tani kasoro.
Hao samaki ni Bungu wadogo.
Fanya hivi nenda kwenye mahoteli makubwa omba orda uwe unawasambazia pia mashuleni au vyuoni.
Pia soko la nje ya Nchi Kwa maelewano mazuri.
 
PC moja ni sh ngapi,auPC 1000 ni sawa na kilo ngapi?unapatikana wapi?
PC moja ni samaki mmoja.Kwa size ya samaki wa nyavu ya nchi 4.5 wanaingia 2 katika kilo moja.Bei ya pc ni maelewano kulingana na soko lako au kama utahitaji kwa kilo napo ni maelewano.Mzigo nashushia mwanza baada ya makusanyo kutoka mialo mbalimbali ya ziwa victoria
 
Badala ya kutaja ukubwa wa Samaki unataja saizi ya Wavu uliotumika kuvulia samaki. Wewe kama ni mvuvi tafuta mtu wa masoko akusaidie kazi.
 
Habarini za majukumu ndugu wadau wa JF.

Ninafanya biashara ya kuuza samaki aina ya sato. Size ya samaki wanaopatikana kwa wingi kwa sasa ni wale wanaovuliwa katika nyavu ya nchi 4 mpaka nchi 4.5.

Kama kuna mdau anafanya hii biashara ya samaki mahali popote na angependa kupata mzigo kutoka kwangu namkaribisha sana.

Nina uwezo wa kukuanzia samaki wengi kulingana na mahitaji yako, hata kama utahitaji piece 1000.

Mauziano ni keshi mkononi, maana yake unahesabu mzigo wako kulingana na makubaliano then unakabidhi hela mkononi. Hiyo ndiyo heshima na nidhamu ya fedha ili tuepuke kurogana na kuuana kabisa.
IMG-20230513-WA0004.jpg
 
Nimekusoma sana Mkuu Wangu.
Nina uzoefu Sana na Ziwani
1000 pieces ni sawa na Tani Moja au Tani kasoro.
Hao samaki ni Bungu wadogo.
Fanya hivi nenda kwenye mahoteli makubwa omba orda uwe unawasambazia pia mashuleni au vyuoni.
Pia soko la nje ya Nchi Kwa maelewano mazuri.
Mashuleni na vyuoni unataka ale hasara
 
Back
Top Bottom