Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Jenga Lodge!!! Hyo hela inatosha Sana,Tena hata lodge mbili, ulifanya hivyo matunda utayaona mapema sana.
Juzi nimekaa dodoma siku nne lodge moja nzuri inaitwa "karen lodge" room ni 50,000 kwa siku alafu ni nyumba ya kawaida ila standard sana ilikuwa ina wageni wa kutosha nikaingiwa na wazo kama lako changamoto ilikuwa ni pesa ila ipo kwenye mawazo yangu.
 
Kwenye business it's all about ROI(Return of investment) Kuna aina ya biashara return yake after investment ni kubwa na risk yake inaweza kuwa calculated. Biashara zozote ambazo wewe ndio unapanga Bei huwa tamu saana na ndio Zina return nono.

Ukituliza akili Kama una 64mil unaweza kudouble capital yako after a short time na risk Yake sio kubwa kihivyo, Kwa Sasa Kuna kitu huko majuu kinaitwa liquidation pallets yaani ni zile old stocks au returned item Kutoka kwa wateja kwa sababu ya rangi au size yake imekuwa tofauti na mtu aliyoagiza.

Ukienda UK, US, Dubai, Australia... Unakuta mzigo godown unaambiwa uchague fungu la item unalotaka... Kuna mzigo wa Air condition pekee, Tower fan pekee, Mapasi ya steamer, Oven microwave e.t.c ...mzigo wa fungu la million 30 unaweza kupewa kwa million 2 tu na pia risk yake sio kubwa sababu unaziona Air conditioner zako na technically hazioozi Wala kuexpire.

Ukifikisha bongo hapa ukaanza kuuza kwa jumla kwenye Duka kubwa au warehouse yako kwa bei ya fasta kwa wauzaji wa jumla na rejareja wa kariako au hata fina consumer unaweza wauzia pia.

Ukikutana na mataikuni wa Hii business wakakuonyesha Namna ya kucrack codes za wakamua mapato ndio fasta unabadilishiwa jina unaitwa Freemason.

I'm talking from my experience..been there, done that.

Hii business wanaifanya wasudan, wanaigeria, Somalians Sana Sana wenye exposure na network.

Pitia link Hii hapa ujifunze zaidi
 
Very interesting aisee.... So, kufanya hii inabidi kwenda mwenyewe physixally kwenye stores nchi husika?
 
Very interesting aisee.... So, kufanya hii inabidi kwenda mwenyewe physixally kwenye stores nchi husika?
Wana option kadhaa Kuna zile za kununua mzigo kwa auction online na wanakutumia via Agent Hadi kwako... Wana legit and reputable companies za kuuza bidhaa from. If supermarket kaka Aldi na Gardenline. But sishauri saana njia hii maana sijawahi kuitumia.

But njia nzuri ni kwenda physically after 1 week utakuwa umepakia mzigo wako na unausunuri pale Bandarini. Fanya research unaweza kutumia bandari ya aidha Dar au Mombasa znz na kadhalika.

But it really pays a lot.

Namjua jamaa yangu Msudani anatengeneza pesa nzuri mno from this business, Yuko Zanzibar yeye.

But kwa sababu huwezi kumove place to place wekeza kwenye real estate na mostly Lodge na achana na monthly payment za wapangaji. Potential location, usimamiz mzuri na passion to do it will take you far.
 
Na 2 na 4 ni nzuri.
1.zinalinda mtaji
2.Wateja ni uhakika
Kama huna changamoto za usimamiaji fanya no 2 kwanza then mapato fanya no 4.
Kama mda wa kusimamia ni tatizo jenga za kupangisha zitakuokoa wakati wa shida.
Wakati wa shida ni upi
1.Kamba kukatika kazini
2.kusimamishwq Kazi
3.kufukuzwa
4.ulemavu nk

Ushauri kama una pesa fanya maendeleo haraka sana kabla ujaingia kwenye ndoa, kufanikiwa kwenye ndoa utegemea na utulivu wa mke
 
Wife kusimamia ni ngumu kiukweli. Hapo kwenye usimamizi ni changamoto hasa. Na kama hii idea ya ufugaji wa MBUZI inahitaji usimamizi wa karibu hasa, ndio kinachonirudisha nyuma kwenye hii idea.
Pia ni rahisi kupigwa.
Pana mtu alipigwa mbuzi 100 usiku mmoja tena wa laki na nusu kila mmoja.Porini huko watakula dili na wezi akinunuliwa bodaboda tu anauza mbuzi hao
 
Pia ni rahisi kupigwa.
Pana mtu alipigwa mbuzi 100 usiku mmoja tena wa laki na nusu kila mmoja.Porini huko watakula dili na wezi akinunuliwa bodaboda tu anauza mbuzi hao
Duuuhhhhhh...!! Mbuzi 100 walisukumwa kwa usiku mmoja? Daaaahhhhh!!!
 
IBA YAANI 8BAA
TENGENEZA.WANA WAKO WA.UKWELI (SIORATROAD)MPIGE.MIKWANJA YAMAANA AKIKISHEN MNAUHAKIkA MNAPOENDA KUNA.MZIGO
DHAMBIHII HAITANIHUSU KAMWE NNWEWE NA ROHO YAKO
MUANDIKE NA MIRATHI KABISA MSITUSUMBUE SIKU YA MWISHO
 
Biashara yeyeto na mswahili usiyokuwa nayo karibu kwa siku hesabu maumivu. Mimi nimepoteza jumla ya milioni 400 sababu sikuwa na mda
 
IBA YAANI 8BAA
TENGENEZA.WANA WAKO WA.UKWELI (SIORATROAD)MPIGE.MIKWANJA YAMAANA AKIKISHEN MNAUHAKIkA MNAPOENDA KUNA.MZIGO
DHAMBIHII HAITANIHUSU KAMWE NNWEWE NA ROHO YAKO

MUANDIKE NA MIRATHI KABISA MSITUSUMBUE SIKU YA MWISHO
Mkuu vipi? Nenda kalale aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…