Kuna comments kama ya huyu uliem quote huwa naziona then naamua kuzipotezea tu mkuu. Wangejua bongo hii hii hata katika watu wanaolipwa hela nyingi sipo, pamoja na kulipwa 14+ per month. Kuna watu wanakunja mara mbili ya hiyo.
Umasikini ni mbaya sana, ndo chanzo cha wivu na frustrations za hivi, kwa hiyo mimi huwa naelewa sana watu wa namna hii.
Mimi nimeweka nidhamu kubwa sana pia katika ku save. Na save 2/3 ya net income yangu, I live a very simple life.
Kitu kikubwa kinachoniumiza kichwa ni namna ya kuizalisha hiyo pesa, kama nilivyosema awali sijawahi fanya biashara ya kuzalisha hata 500.