Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Kwa wapangaji Kuna faida gan mzee??
Tatizo la nyumba za kupanga, kuna wapangaji wengine vichwa maji ni wachafu na waharibifu. Weza kuta siku akitoka gharama ya ukarabati ni sawa na pesa yote aliyokulipa kama pango. Fikiria kitu kingine. Ila UTT usiisahau pia😎
 
Kunatofauti kati ya kulima na kuweka mpunga :sasasijajua unataka kusema nini kati ya hapo
Wewe hutaki utajiri? Mbona yote hayo unayajua na hufanyi.

Bla bla bla zako za fulani, fulani, fulani hazina mantiki.
Sema mimi ninafanya kisha tukiswalishe utusaidie majibu!
Ukishikwa sikio na wakubwa mbele za watu huwa tunachutama sio kupayuka mikelele tena mamaaa naumizwaaa
 

Nisinge andika kama sifanyi mtaji wangu ndio mdogo nilinunua gunia 120 kwa laki moja kipindi cha mavuno saiv gunia hilohilo linauzwa 150000 hapo bila kukoboa : sasa ukikoboa nakuuza mchele kwa 2850 kwa KG ndio bei tunayojumlisha kwa huku hapo kwenye hyo 50000 iliyoongeza kuna nyingine tena inaongezeka kwakila gunia la mpunga utakalo koboa so naongea vitu ambavyo naviishi sio brabra mkuu
 
tafuta eneo lililo changamka hasa barabarani,kwenye senta ambapo kuna muingiliano wa watu nunua uwanja jenga flem za biashara kwa ajili ya kupangisha .utanishukuru baadae
 
tafuta eneo lililo changamka hasa barabarani,kwenye senta ambapo kuna muingiliano wa watu nunua uwanja jenga flem za biashara kwa ajili ya kupangisha .utanishukuru baadae
..mkuu wazo zuri ila eneo kama hilo kwa mjini linaweza kuwa zaidi ya 100m..eneo tu!..ni sawa au zaidi ya kununua plot maeneo watu walishajenga na kuwa na huduma zote huwa yanakuwa bei kubwa sana.
 
..mkuu wazo zuri ila eneo kama hilo kwa mjini linaweza kuwa zaidi ya 100m..eneo tu!..ni sawa au zaidi ya kununua plot maeneo watu walishajenga na kuwa na huduma zote huwa yanakuwa bei kubwa sana.
 
unapoa amua kuwekeza una angalia maeneo ambayo ni machanga kulingana na kias ulichonacho .mfano unaweza nunua eneo ambalo sio katikati ya mji na pamechamka kias kwa bei ya kawaida lakin ukajikuta baada ya muaka mmoja au miwili pamepanda thamani ya kibiashara
 
For me kujenga nyumba ya kupangisha ni the best ukitulia utafanya hayo yote kutoka kwenye kupangisha
 

Mie nakubaliana na wewe. Mwaka 2020 niliweka gunia 200 kwa tsh 45k mpaka 50k kwa kila gunia. Nikaweka store. December 2020 hazikupanda bei kutokana na changamoto zile za mzee baba. 2021 zikapanda nikauza kwa 90k. Nilipata faida kama 8m sema ilichelewa sana.

Kuna mshikaji wangu yupo Tabora yeye alianza hii mambo zaidi ya miaka 15 iliyopita. Msimu uliopita alikuwa na gunia 15,000. Kaziuza kwa 130k kwa kila gunia. Jamaa kapiga 1.95B yaani hapo kwa haraka. Jamaa kapiga zaidi ya 1B kama faida.

Najua wengi watadharau ila mie ni shuhuda.
 
Acha theory mingi mingi Boss,
Watu wamekua wakubwa ujue na wengine wako kwenye mounga huo unaofundisha hapa longo longo
Huo ndio ukweli acha kudharau. Sema tu changamoto zipo. Uzuri kama alivyosema mpunga hauliwi na wadudu unaweza kuhifadhi hata miaka 4 mpaka upande bei. Hapo utakuwa unafanya mambo mengine wakati unasubiri upande.
 
Gunia 15,000 sio mchezo aisee
 
Yupo sahihi. Ingia mashambani utajua hujui

Mkuu mpunga inahitaji kwa uujue vizur napia upate vijana au madalali waaminifu wakununua mpunga toka kwa wakulima mfano unampa mtu pesa akukusanyie gunia 100 kwakila gunia pesa yake ya ulanguzi ni2000 Sasa yeye anaenda vijijini kukusanya akikusanya anakupigia sim tayar boss we unapeleka gari kubeba kuleta stop

Sasa hao unaowapa pesa nao wakifika huko huwapa pia vijana wa baiskel kwenda kuchukua ndani ndani uko nahutokomea na pesa so siku unataka kuchukua gunia unakuta unahasara ya gunia10 au wamekununulia mpunga haujakauka vizuri siku unakoboa unauza unatoka umekatika chenga au biriani warangi ya njano

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana hapo nimesema ingia shambani. Halafu hao watu usiwape pesa ya gunia 100 at once. Mpe ya gunia 20 kwanza. Kidogo Kidogo mpaka ukamilishe.
 
Ndio maana hapo nimesema ingia shambani. Halafu hao watu usiwape pesa ya gunia 100 at once. Mpe ya gunia 20 kwanza. Kidogo Kidogo mpaka ukamilishe.
Mkuu hapo ww unataka kukusanya gunia1000 mwanzoni kabisa mwa mavuno Bei huwa ndogo Sasa hapo inakulazimu ununue haraka guni nyingi utalazimika ununue kwa mfumo huo wakuwapa watu pesa ukisema ukomae ww utashangaa Hadi Bei imepanda hata gunia500 hujafikisha a

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…