Matunzo 02
JF-Expert Member
- Jul 7, 2026
- 1,620
- 3,165
Ukikuta kijana wa kiislamu ukimuuliza anaoa lini anakuambia kuwa bado Kuna jambo sijaweka sawa... ila ukija kwa wakristo utaambiwa Mungu hajanionesha mke au mume ila chakushangaza wakati huo ana mahawara kibaoWaislamu wanaoneshwa na nani mke wa kuoa?
Nilidhani kila mwenye imani na Mungu basi atafikiria mke/mume ni kutoka kwa Mungu
Sijasoma uzi ila nahisi wewe ni Church boy kwenye moja na mbili uliemtanguliza mungu kwenye kila kitu chakoWakuu habari ya uzima wenu na majukumu ya maendeleo yenu naamini MUNGU anazidi kuwapigania usiku na mchana.
Basi twende moja kwa moja kwenye maada,kiukweli wakuu nakabiliwa na stress mpaka kuna wakati nashindwa kutimiza majukumu yangu ya kazi kisa kuwaza itakuaje kuhusu ndoa?,,lini ntaoa kwa sasa naelekea miaka 31,kila anae kuuliza umeshaoa namwambia bado ansema unasubiri nini?,hata waumini wenzangu kanisani wananishambulia kwanini sioi?,wengine angalia utazeeka,yaani maneno yamekuwa mengi saana na wengi wananiuliza kila utakae pokea simu yake anakuuliza shemiji/wifi mzima?
,kuna wakati stress zinanikaba mpaka nashindwa kuomba maombi vyema sababu ya stress,,inaweza fululiza mpaka wiki nipo stressed najikuta hata usingizi sipati nikiwa stressed sana kuna wakati nikiamka saa 10 usiku sipati tena usingizi mpaka asubuhi wakati huo nawaza.,,,mpaka mwili unapungua watu wananiuliza mbona umepungua sana?,,japo pia mimi ni mwembamba na nimwana maombi
(Story kidogo)
Namkumbuka kuna Binti aliwahi kunambia anipenda kama miaka mitatu nyuma imepita, basi mimi nikamwambia sawa,nikamwambia ngoja niingie kwenye maombi ili MUNGU kama amepanga tuwe pamoja itakuwa,chakushangaza nilimuotea kama ndoto 3 kuwa anawanaume wengine,pia kuna ndoto nyingine ilionyesha anisaliti,basi tukaendelea baada ya muda nikashangaa mawasiliano yakapungua baada ya kukwambia mbona naona kama vitu havipo sawa? ghafula akawa hajibu text zangu kwa wakati,majibu yakawa Shortcut,, oohh nikajua mambo yamegoma hapa,,
Baada ya muda kidogo nikipata ishu ya kazi ya uchoraji maeneo fulani,,,ile naenda kufanya ile kazi,chakushangaza nikayaona yale mazingira ya ile ndoto niliyoota kuwa yupo na kundi la wanaume wamemuzunguka, wakati huo nikiwa namuita jina lake hakugeuka kunitazama amenigeuzia mgongo huku akiendelea kuongea na wale wanaume,, baada ya kufika pale nikashangaa kuna mazingira Yale ynafanana na eneo hilo na wakati huo huyo Binti alikuwa akiishi huko kwa bibi yake,, so baadae mahusiano yakawa kama hayaeleweki ,,,pia nikasikia kuwa mama ake alikuwa akimsumbua kwamba asije akazalia nyumbani kumwaibisha,,,,,baada ya muda nikaja kugundua hilo eneo alipokuwa anaishi kwa bibi yake kuna jamaa alikuwa akitembea nae,,
Kwa kufupisha story na huyo jamaaa ndiye amemuao mpaka sasa,,na kipindi anakuja kutoka mahari jamaa Binti alinambia na pia alitaka kuja wabarikiwe kanisani alipokuwa anasali huyo Binti maana ndipo naposali pia,,akini me nikamwambia binti utakujaje madhabahuni wakati ulikuwa unafanya uasherati na huyo mtu,so wakamaliza nyumbani kwao,,
Kuna siku alikuja huku akiwa na mimba ya pili kujifungua kwao,,nikashangaa akaomba namba yangu tukaanza kuzungumza na mazungumzo yakawa ya kasi kidogo na usiku anakutumia text za usiku mwema na mimi nipo makini na ndoa za watu, Binti akishaolewa hata kama tulikuwa karibu huwa nakata mawasiliano nae,,,mala ananiambia alinipenda kule alienda tu basi lakini alitamani mmii ndiye nimuoe,,,,mala labda mimi sikuwa mke sahihi kwako?
Kwa ufupi: So hilo jambo pia lilinipa stress na nikawa nawaza na ninawaza au ningemuoa tu labda pengine ningekuwa mbali kimaendeleo maana naona kama nimesimama sehemu sionei mwelekeo,pesa napata lakini zinaisha bila chochote cha maana.
Kiukweli wakuuu oooh nipo na stress,,,naona kama nipo kwenye vita ya kiroho, sahizi tena yupo binti huyu wa chuo alisema anahitaji ndoa na Mimi lakini bado ana miaka minne mbele ya kutimiza ndoto zake ,,sahizi ameenda boarding,
Nawaza sana MUNGU anipe wepesi kwa hili,natamani nianzishe maisha ya ndoa na moyo upo radhi kabisa nasikia msukumo ndani wakufanya maamzi,,,,lakini sijui hii hofu inatoka wapi yakutochukua maamzi,
Hili jambo linanikosesha furaha na amani kisa kuwaza ndoa,mpaka kuna wakati unawaza au ningemuoa fulani?
Tumbo sahizi naona kama maumivu upande wa mbavu naona stress zinazidi mpaka dalili ya vidonda vya tumbo,,,
Naona nikipata mke stress zitaisha 😱😱😱
Poleni kwa Uzi mrefu kidogo.
Mke wa kuoa ihusishe Jamiii utapata mke safi kabisaWaislamu wanaoneshwa na nani mke wa kuoa?
Nilidhani kila mwenye imani na Mungu basi atafikiria mke/mume ni kutoka kwa Mungu
Amina mkuu,,,lakini si kwamba naogopa kutongoza ,,me labda nikutofanya uasherati bila ndoa lakini swala la kuaproach nawezaKwanza Nakuhurumia.
Maisha jinsi yalivyo bila shaka huko mbelen ww utakufa na stress😊😊😊
Ninaheshim Iman yako na sitaliingilia hilo.
Ila Binafsi sijaona kitu cha kukupa stress , bali nimeona udhaifu upande wako. (Nje ya Iman yako ya Kilokole).
Kwanza 🙄🙄🙄🙄yaan unataka Binti ndio aje akutongoze?. Au aseme anakupenda?. Ndio useme ametoka kwa bwana?
Najua Ww unaogopa kutongoza kwasababu unaona utaingia dhambini na kufanya uasherat.
ila ni jambo la lazima kufanya kama mwanaume. Fanyia kaz hilo.
Pili, kwanini usioe Mpendwa mwenzako hapo kanisani?.na ww ndio umfuate . Usisubiri aoteshwe kwenye ndoto kuwa ww ni mwanaume sahihi kwake. Bali ww ndio uchukue hatua.
Tatu, huo umri usikupe stress.
Stress iwe kupambania maisha yako ya hapa duniani yawe bora.
Ila naona umejikita kupambania ya Peponi pekee na ukasahau kuwa kuna maisha pia ya hapa duniani.
Nne, Usiogope. Bwana wako yuko pamoja na ww siku zote za Maisha yako.
Mkuu me alinambia tu ananipenda anataka tuwe wapenzi wakati huo sikuwa hata na wazo juu yake kwa wakati huoKosa liko hapo nilipopaweusisha.
Usimpe Mungu majukumu yaliyo ndani ya uwezo wako.
Kwanza umekwepa jukumu la kutongoza hadi binti ndiye akakutongoza, bado tena uka-seek approval kwa Mungu.
Kamwambie mchungaji wako arudishe sadaka zako maana anakula sadaka halafu kondoo hulishwi vyakula vinavyotakiwa.
Ahsantee mkuu nimekuelewaKwenye Biblia nzima, wapi umeona mtu anamuuliza Mungu kwamba amuoe nani? Achana na ile ya mtumishi wa Ibrahimu.
Sasa kama akina Ibrahimu, Yakobo, Musa n.k ambayo wanaitwa mababa wa Imani hawajanukuliwa popote wakiomba Mungu awaonyeshe wanawake wa kuwaoa, inamaanisha, jukumu la uoaji na uolewaji liko kwenye uwezo wa kiakili aliotipatia Mungu.
Usimtwishe Mungu jukumu lililo ndani yako tafadhali.
Yaani hapo ni sawa na unampa Mungu kazi ya kukutongozea.
Acha hizo mazee, weka vigezo vyako unavyovitaka kwa mwanamke, Kisha unaoona wanaendana hata kwa 50%, tongoza na uachane na pigo za "namuuliza Mungu", utazeeka bila kuoa.
NB: Watu wenye pigo zako ndiyo hufanya sisi wanaamini Mungu tuonekane hatujielewi, kumbe ni vichungaji vyenu uchwara uchwara vinawakaririsha "Blind faith", ni sawa na Yesu aliposema "kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake, wote watatumbukia shimoni"
Wito: Kuanzis Leo, achana na Imani kipofu (Imani isiyotumia akili), fuata Imani inayoona (inayotumia akili)
Amina mtumishi!Unapata stress kwa kuiwazia ndoa!!!!!. Kuoa ni ww (mwanaume) unaamua kisha unatekeleza. Suala la kuoa huwa likishafikia wakati wake unajikuta tu unafanya mipango ya kuoa na unaoa kweli.
Kila jambo na wakati wake na hakuna kitu chenye nguvu kubwa duniani kushinda wakati. Wakati wako wa kuoa ukifika utaoa tu
Hiyo ni kweli aliwekeza pande zote mbili,ilipo tiki moja ndo hivyoTulia kwasasa na kuoa ni kutafuta kama kilimo huwezi ukawa na mmoja ukaenda naye mpaka mwisho weka plann ya wengi ndani ya mwaka mmoja utamuona aliye sawa kwako nenda naye huyo huyo mmoja anaweza badilila mbeleni ukarudi nyuma mwenzako unayemuongelea ulikuwa unamuota aliweka mitego mingi ndio maana mmoja ulivyonasa akaachana na wengine ndivyo hivyo nawe ufanye tega mitego mingi
Au unabeti mtumishi maana hv ndo humaliza helaDaah mtumishi haya mambo ni moto,,,,ukijiuliza upo mwenyewe tu mmh
Huu 'useengee' wa kuomba kutafutiwa au kukuchagulia mke asijaribu kabisa.ukikoswa omba ushaur kwa mchungaj wako uoe binti gan