Nina stess kali za kuoa mpaka nakonda mwili

Barikiwa kwa kufafanua vizuri
 
Ahsantee mkuu , Mungu akubariki sana kwa ushauri wako murua,,,itabidi nisahau memory za nyuma na matukio hayo ili nisonge mbele.
 
Siyo hivyo mkuu labda ni hofu ya umri na kuwaza je itakuwa lini? MUNGU namiaamini sana sema kuna wakati unapitia hali fulani ya ukimya mpaka unasema mmh!
 
Achana na huyo Binti, tafuta hela, wanawake wazuri watakuja tu. Kuoa ni kujitakia stress zaidi na UMASKINI MDAU!
 
Tuliooa na 24 sijui tunaweka wapi sura zetu. Huu ushauri auzingatie. Kama stress za kuwa single haziwezi sijui kama anaweza kuvumilia za ndani ya ndoa
Tuliooa na 24 sijui tunaweka wapi sura zetu. Huu ushauri auzingatie. Kama stress za kuwa single haziwezi sijui kama anaweza kuvumilia za ndani ya ndoa
Naamini mambo yatakuwa sawa kabisa sema ni ili stress fulani ikichanganywa na kaupweke fulani
 
Achana na huyo Binti, tafuta hela, wanawake wazuri watakuja tu. Kuoa ni kujitakia stress zaidi na UMASKINI MDAU!
Hiyo tayari kasha olewa kitambo,,pengine huyu wa chuo bado na Hadi aje amalize shule huko eti nimemsubiri tu?
 
Kama mshale mkononi mwa shujaa ndivyo walivyo Wana wa ujanani, mkuu kuliko kuwaka tamaa oa kwanza inavoonekana wewe ni mcha Mungu.
Amina mkuu MUNGU anaenda kuniangazia,,namheshimu sana MUNGU mpaka hapa mtaani kwangu jina langu naitwa Mtumishi au Mchungaji,maana kile ulichokibeba au maisha yako halisia ya kiroho Huwa hayajifichi,,maana sisi ni Nuru ya ulimwengu
 
Hiyo tayari kasha olewa kitambo,,pengine huyu wa chuo bado na Hadi aje amalize shule huko eti nimemsubiri tu?
Waweza subiri, ila kuoa siyo lazima, take your time, jiimarishe kiuchumi, zidi kukomaa kiakili, usiendekeze ku trust mwanamke, nenda na flow.
Ila kuoa ni stressful na kutakuletea UMASKINI tu...
Jiandae kisaikolijia na kimaisha kwanza ili hata ukimpata mwenza na akaku disappoint usije kuokota makopo mtaani!
 
πŸ˜† Kwamba kuokota makopo kisa stress zimezidi!
 
Kama una imani ya kuoa ,fanya mpango uoe tena unaye mpenda ,achana na vijana wa humu ni malaya wa kutupa.

Hayo mambo kawaida ,yule aliyeolewa sio bahati yako tena kaa mbali naye kabisa..Kupata wa kuendana naye ni msimamo tu ..Sisi wengine tumeishi Dar tena tukiwa na kazi nzuri ,miruzi ilikuwa kama hiyo na umri umeenda..Inafika hatua ,hawa wasichana sehemu za kazi wanakupakazia kwamba unatoka nao ila sio kweli ,mwishoe tumeoa kwetu na tunaishi fresh tu.

Kila kitu ni nia ,wanawake hawana maajabu so tafuta yule mwenye tabia nzuri ,ndoa zenyewe zinaweza kufa muda wowote so fanye vile roho yako inapenda ,kama unasita usije kujaribu kuoa huyo kiumbe .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…