Nina tabia ya kupenda vitu vikubwa na vyenye rangi nyeusi

Nina tabia ya kupenda vitu vikubwa na vyenye rangi nyeusi

Tajiri Sinabay

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,333
Reaction score
3,619
Asamaleko wadau

Mimi nina hii tabia ya kupenda vitu vikubwa na vyeusi. Pengine kama inakuwa na sababu fulani naweza kupata jibu hapa.

Tangu enzi nanunuliwa mavazi nilikuwa napenda sana nguo nyeusi,
Viatu ndiyo kabisa..

Lakini pia tangu nimeanza kuwa mimi Mfumo wa maisha yangu haujawahi kubadilika kwenye hii hali.

Yaani kamavazi napenda yale makubwaa halafu ni meusi kuanzia suruali hadi flana.

Simu pia napenda iwe kubwaa halafu nyeusi, hata kama ni kitochi napenda kutumia zile kubwa zinazosemwa ni za wakulima.

Mwanamke pia napenda Awe mkuubwa halafu mweusi.

Chombo cha usafiri pia (pikipiki) napenda iwe kubwa halafu nyeusi (niliwahi kumiliki sina kwa sasa)

kwa ujumla hii hali ninayo karibia kwenye kila kitu.
Sio tatizo kwangu ila nataka nijuwe tu pengine kuna kitu kinasababisha hiyo hali.
 
Back
Top Bottom