Nina tatizo la kutosikia vizuri, natafuta kazi

Nina tatizo la kutosikia vizuri, natafuta kazi

Acha Maneno

Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
54
Reaction score
112
Mimi ni kijana niliesomea uhasibu kwa ngazi ya Diploma, na pia nimesomea ICT kwa ngazi ya certificate.

Nina changamoto ya usikivu hafifu.

Hali hii ya kutosikia vizuri imekuwa inaninyima fursa za ajira sana hadi ikafikia kipindi napata msongo wa mawazo.

Naomba mwenye uwezo wa kunisaidia anishike mkono niweze kupata ajira yoyote halali ambayo inaweza nisaidia kwenye maisha yangu kiuchumi.

Asante na Mbarikiwe.
 
Sio pekeako mkuu ata mm na shida kama iyo japo na jipambania Cha kwanza acha dhana ya kuji linganisha icho ndo kitu kikubwa mno we jikubali jinsi ulivyo msongo wa mawazo inapotea wenyewe trust me
 
Kijana hata mimi ninatatizo kama lako lakini nimepata ajira serikalini jitahidi kusoma degree alafu uombe ajira za utumishi kama unaelewa madesa ukimaliza degree utapata ajira
 
Back
Top Bottom