Mkuu fikiri upya Tena juu ya hiyo dhana ya faida ya haraka,, kinacho tukwamisha vijana wengi ni kutaka faida ya haraka mwisho wa siku tunajikuta tunapoteza na kuanza upya.
Ushauri wangu tafuta wazo lolote la biashara hata ufugaji watafute wajuzi na wazoefu na hicho kitu then Anza taratibu, trust me faida itakuja yenyew tu.
Lakini kwa mtaji huo nakushauri Anza ufugaji ndege (kuku, Bata n.k) shirikisha watu wenye uzoefu wa kufuga hao ndege, nadhan hiyo ndio njia rahisi japo changamoto hazikwepeki na ndio mafanikio yenyew.
Hata hao unaowaona wanapata faida ya haraka haraka walianzia mbali Sana na wamepitia hangamoto ambazo wengi tunazikwepa, faida ni matokeo ya michakato ya mtu binafsi, uki focus kwenye faida Sana bila kuangalia what it take kupata hiyo faida lazima upotee, ndio maana unakuta mtu anafanikiwa na kupata faida kubwa katika biashara ambayo mtu mwengine imemfilisi.
Katika yote mtangulize Mungu utafaikiwa