Nina Tshs. 45 milioni, Nifanye biashara gani?

Nina Tshs. 45 milioni, Nifanye biashara gani?

Ahsante wadau kwa michango ya mawazo mnayoendelea kuitoa. Ila sehemu ya mawazo aliyotoa Ng'wanapagi imenichekesha. Yaani ushauri wa kufuga bundi. Sasa uchaguzi ukiisha na soko la hayo mayai ya bundi si litakuwa halipo tena hadi uchaguzi mwingine? Bundi wenyewe wanatisha na kutokana na bundi kuhusishwa sana na imani za kishirikina ufugaji wake utanijengea mahusiano mabaya na jamii inayonizunguka na pengine hata kupelekea kufukuza wateja wangu katika biashara zangu zingine.

Mkuu ushawahi kufeli tangia umeanza biashara zako? Kama jibu ni ndio nambie marangapi, tuendelee kushauriana.
 
Mkuu ushawahi kufeli tangia umeanza biashara zako? Kama jibu ni ndio nambie marangapi, tuendelee kushauriana.

Mkuu japo sijaelewa unakoelekea lakini niseme tu kuwa kama ni kufeli katika biashara jibu ni "ndiyo" niliwahi kufeli mara moja. Hii ni miaka 12 iliyopita. Lakini katika biashara hizi zingine nilizogusia hapa ambazo kwa sasa zina miaka minne tangu nizianze jibu litakuwa "hapana" sijawahi kufeli. Sasa nasubiri ushauri wako Steven.
 
Daah. Sema niko huku porini kunakonipa riziki yangu ya kila siku lakini ningekua Dar hili wazo ningeliiba na ndani ya wiki mbili nakuhakikishia ningekuwa nishaanza biashara. Wazo zuri sana.

Kama kununa hisa huezi au haupo interested, na hukn hakuna msongamano wa makazi tafuta eneo hata la heka1 au mbili moja hukohuko ulipo ufanye kilimo cha greenhouse nahop hautakuwa na dificult management na utapatafaida maradufu pia.
 
naomba kujua hizo miradi ambazo zimekufikisha hapo baada ya miak minne
 
We ni mwenyeji wa Wapi?

Kagombee Ubunge ulikotoka, ni biashara nzuri sana. Kwa sasa nunua Jezi ukaanzishe mashindano ya Nyaka-One cup. Tafuta vijana wawili wenye ushawishi mkubwa waeleze nia yako kisha wagaie laki 5 kila mmoja.
 
Last edited by a moderator:
Wana JF,
Ni kwamba mimi ninaishi Dar es Salaam. Umbali kutoka yalipo makazi yangu hadi city centre ni wastani wa kilometer 18. Nimeajiriwa sehemu ambako kwa maisha yetu ya kitanzania nadiriki kusema kwamba mshahara si mbaya kivile. Kutokana na ajira hii niliyonayo nimeweza kujenga nyumba ya kisasa kiasi fulani na pia kufungua miradi kadhaa hapa hapa jijini.Kwa kiasi kikubwa hii miradi inasimamiwa na mke wangu akisaidiwa na watu wengine tuliowaajiri.
.

naamini ungeweka wazi miradi uliyonayo sasa,ingekuwa rahisi watu wengine kutoa mawazo ya biashara zaidi.Unaweza pewa wazo la biashara litalosupport miradi uliyonayo sasa ama kuwa supported na miradi uliyo nayo sasa...
 
Mkuu japo sijaelewa unakoelekea lakini niseme tu kuwa kama ni kufeli katika biashara jibu ni "ndiyo" niliwahi kufeli mara moja. Hii ni miaka 12 iliyopita. Lakini katika biashara hizi zingine nilizogusia hapa ambazo kwa sasa zina miaka minne tangu nizianze jibu litakuwa "hapana" sijawahi kufeli. Sasa nasubiri ushauri wako Steven.

Kutoka Post ya kwanza , na hili jibu ulilotoa, nakushauri uendelee kupanua kile ambacho ushakianzisha sababu katika majibu yako inaonyesha 90% wewe sio risk taker.
 
Kutoka Post ya kwanza , na hili jibu ulilotoa, nakushauri uendelee kupanua kile ambacho ushakianzisha sababu katika majibu yako inaonyesha 90% wewe sio risk taker.

Mkuu Masatu, ni vigezo gani ulivyotumia hadi ku determine hiyo 90% ambayo ume conclude nayo kuwa mimi ni risk-averse investor? Yaani 90% umeipataje? Umeangalia idadi ya miradi niliyokwisha fanya ambayo ni minne (mmoja niliofanya na kufeli 12 years back na hii mitatu inayoendelea vizuri) au umeangalia aina ya miradi? Na je katika masuala ya ujasiriamali kuitwa risk taker lazima uwe na idadi ya miradi mingi iliyofeli? I don't think so my bro.
 
Mkuu Nyaka-One
Mimi cha kukushauri fungua duka mojawapo kati ya haya.
-Duka la nafaka kwa matumizi ya Binadamu (Mchele,maharage,mtama,mahindi,sembe,ulezi uwele,mtama,n.k)
-Duka mchanganyiko la Bidhaa tofauti lina faida saana niliona kwa bosi wangu mmoja kama litasimamiwa vizuri.
-Duka la Spare Parts za magari,pikikipi,bajaj na vipuli mbali mbali…
-Duka la Hardware & Electronics Instruments…
……mojawapo kati ya hayo ukiamua kuwekeza haswa utaongeza faida… kwanz hela haitaisha yoote kuiwekeza…

N.B: kama utaamua kuchukua wazo mojawapo hapo juu toka kwangu au toka kwa wadu wengine, naomba nitumie nafasi hii kuomba ajira tena! Itakuwa vizuri ukiniajiri katika kipindi hiki ambacho upo kwenye Building new project ili nianze na 1…
Kwenye mawazo yangu nina uzoefu,.
Ni hayo Mkuu…serious usinipite nakuomba tafadhali! Fursa hii…
 
jamani muwe mnapitia au kusoma vizuri post na mawazo yanayotolewa. .... rejea mleta post ameweka TOR (Terms of Reference) za mradi anaotaka apate mawazo ufanyike ..... anataka mradi utakaofanyika eneo LA nyumbani anapoishi ambapo haitachukua muda wake mwingi wala muda Wa mwenza wake katika usimamizi .... mradi wenye minimum supervision yao binafsi .... hii ni backyard project

I stand to be corrected
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana kwa ujasiriamali na mafanikio mpaka hapo ulipofika , mimi napingana na mdau aliyesema wewe sio risk taker , anafanya miradi 2 ambayo amasema inampa faida lazima kuna risk fulani alichukua kuanza hizi biashara anyway kurudi kwenye wazo , jitahidi kuangalia vision yako ya muda mrefu ikoje ili tukusaidie , nafikiri ungejikita kwenye real estate , viwanja au kujenga tu nyumba moja , vitu vingine vingi vitahitaji usimamamizi wa karibu sana
 
jamani muwe mnapitia au kusoma vizuri post na mawazo yanayotolewa. .... rejea mleta post ameweka TOR (Terms of Reference) za mradi anaotaka apate mawazo ufanyike ..... anataka mradi utakaofanyika eneo LA nyumbani anapoishi ambapo haitachukua muda wake mwingi wala muda Wa mwenza wake katika usimamizi .... mradi wenye minimum supervision yao binafsi .... hii ni backyard project

I stand to be corrected

Mkuu Bluetooth, uko sahihi kabisa. Ahsante kwa kuwakumbusha wachangiaji ku refer kwenye the most important Term of Reference ambayo ni mradi kutakiwa kufanyika nyumbani ninapoishi. Niseme tu kuwa niko serious na jambo hili na naomba msichoke kutoa mawazo yenu pale mnapodhani kuwa mawazo hayo yatajenga.
 
Na sasa nimeelewa! All the best Kamanda
 
kuna bank unaweka hela kwenye fixed deposit account na kisha unachukua 90% ya hiyo hela kuendelea na uwekezaji. kama utaweka mil 100 utapata mil 12 kwa mwaka. na mil 90 unaichukua kama mkopo unafanya biashara nyingine. PM Mimi.
 
Aisee embu nunua, Toyota coaster, au Nissan civilian, then Anza biashara ya daladala, Kwa siku unaingiza 100000 mpaka 130000, Kwa mwezi ni 3m toa laki 5 ya service, 2.5m profit *11 month = 27.5 m that you are minimum profit per year, baada ya miaka 2 , utaweza tanua biashara Kwa kuongeza Ile tata marcopolo, ambayo hesabu yake ni kilo 2 Kwa siku, per month ni 6m, Asa hapo unataka Nini Tena, u keep doing it baada ya mda utakuwa kama akina abood kama sio hood bus, but u need to be a good risk taker in this business
 
Back
Top Bottom