simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,418
- 9,209
Kama unaogopa sana risk unaweza ukawekeza pale DSE,
Stock ipi inao mwelekeo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama unaogopa sana risk unaweza ukawekeza pale DSE,
Ahsante wadau kwa michango ya mawazo mnayoendelea kuitoa. Ila sehemu ya mawazo aliyotoa Ng'wanapagi imenichekesha. Yaani ushauri wa kufuga bundi. Sasa uchaguzi ukiisha na soko la hayo mayai ya bundi si litakuwa halipo tena hadi uchaguzi mwingine? Bundi wenyewe wanatisha na kutokana na bundi kuhusishwa sana na imani za kishirikina ufugaji wake utanijengea mahusiano mabaya na jamii inayonizunguka na pengine hata kupelekea kufukuza wateja wangu katika biashara zangu zingine.
Mkuu ushawahi kufeli tangia umeanza biashara zako? Kama jibu ni ndio nambie marangapi, tuendelee kushauriana.
Daah. Sema niko huku porini kunakonipa riziki yangu ya kila siku lakini ningekua Dar hili wazo ningeliiba na ndani ya wiki mbili nakuhakikishia ningekuwa nishaanza biashara. Wazo zuri sana.
Wana JF,
Ni kwamba mimi ninaishi Dar es Salaam. Umbali kutoka yalipo makazi yangu hadi city centre ni wastani wa kilometer 18. Nimeajiriwa sehemu ambako kwa maisha yetu ya kitanzania nadiriki kusema kwamba mshahara si mbaya kivile. Kutokana na ajira hii niliyonayo nimeweza kujenga nyumba ya kisasa kiasi fulani na pia kufungua miradi kadhaa hapa hapa jijini.Kwa kiasi kikubwa hii miradi inasimamiwa na mke wangu akisaidiwa na watu wengine tuliowaajiri.
.
Mkuu japo sijaelewa unakoelekea lakini niseme tu kuwa kama ni kufeli katika biashara jibu ni "ndiyo" niliwahi kufeli mara moja. Hii ni miaka 12 iliyopita. Lakini katika biashara hizi zingine nilizogusia hapa ambazo kwa sasa zina miaka minne tangu nizianze jibu litakuwa "hapana" sijawahi kufeli. Sasa nasubiri ushauri wako Steven.
Kutoka Post ya kwanza , na hili jibu ulilotoa, nakushauri uendelee kupanua kile ambacho ushakianzisha sababu katika majibu yako inaonyesha 90% wewe sio risk taker.
Mkuu Nyaka-One
Mimi cha kukushauri fungua duka mojawapo kati ya haya.
-Duka la nafaka kwa matumizi ya Binadamu (Mchele,maharage,mtama,mahindi,sembe,ulezi uwele,mtama,n.k)
-Duka mchanganyiko la Bidhaa tofauti lina faida saana niliona kwa bosi wangu mmoja kama litasimamiwa vizuri.
-Duka la Spare Parts za magari,pikikipi,bajaj na vipuli mbali mbali
-Duka la Hardware & Electronics Instruments
mojawapo kati ya hayo ukiamua kuwekeza haswa utaongeza faida kwanz hela haitaisha yoote kuiwekeza
N.B: kama utaamua kuchukua wazo mojawapo hapo juu toka kwangu au toka kwa wadu wengine, naomba nitumie nafasi hii kuomba ajira tena! Itakuwa vizuri ukiniajiri katika kipindi hiki ambacho upo kwenye Building new project ili nianze na 1
Kwenye mawazo yangu nina uzoefu,.
Ni hayo Mkuu serious usinipite nakuomba tafadhali! Fursa hii
jamani muwe mnapitia au kusoma vizuri post na mawazo yanayotolewa. .... rejea mleta post ameweka TOR (Terms of Reference) za mradi anaotaka apate mawazo ufanyike ..... anataka mradi utakaofanyika eneo LA nyumbani anapoishi ambapo haitachukua muda wake mwingi wala muda Wa mwenza wake katika usimamizi .... mradi wenye minimum supervision yao binafsi .... hii ni backyard project
I stand to be corrected
Mkuu Bluetooth, uko sahihi kabisa. Ahsante kwa kuwakumbusha wachangiaji ku refer kwenye the most important Term of Reference ambayo ni mradi kutakiwa kufanyika nyumbani ninapoishi. Niseme tu kuwa niko serious na jambo hili na naomba msichoke kutoa mawazo yenu pale mnapodhani kuwa mawazo hayo yatajenga.