Nina ugonjwa wa Hyperthyroidism. Professor wa Urology aliniandikia Tadalafil 5Mg lakini hazijasaidia

Nina ugonjwa wa Hyperthyroidism. Professor wa Urology aliniandikia Tadalafil 5Mg lakini hazijasaidia

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,913
Reaction score
4,695
Habarini, mimi ni baba wa watoto wanne, nina umri wa miaka 38. Nimekuwa nikiugua hyperthyroidism (diffused multinodular goiter) kwa miaka mitatu sasa.

Kabla ya kuanza kuugua hyperthyroidism nilikuwa na tatizo la nguvu za kiume kwa takriban miaka saba.

Baada ya kugundulika na hyperthyroidism, tatizo la nguvu za kiume lilizidi kuongezeka. Nilimwona Profesa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo (Urology) ambaye aliniandikia dawa ya Tadalafil 5mg ili kusaidia kurejesha nguvu za kiume.

Nimekuwa nikitumia dawa hii kwa zaidi ya mara 20 katika vipindi tofauti ndani ya miaka mitatu, lakini tatizo halijaisha na hyperthyroidism bado ipo.

Kwa sasa sina hamu kabisa ya tendo la ndoa na nguvu za kiume zimepungua. Nikiwa usingizini uume unasimama vizuri, lakini nikijaribu kushiriki tendo na mke wangu, hamu haipo kabisa.

Wakati mwingine uume hausimami, au ukisimama unakuwa legelege na unalala mara tu ninapoanza tendo. Hali hii imeniletea hofu na wasiwasi kila ninapotarajia au kuhitajika kushiriki tendo.

Tatizo hili limekuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, tangu nipate hyperthyroidism, na hata kabla yake kulikuwa na dalili. Wakati mwingine nawaza labda nimerogwa, ingawa sitaki kuamini mambo ya kishirikina.

Kwa miaka 12 sasa nimekuwa nikikumbwa na changamoto mbalimbali za kiafya mfululizo. Wakati mwingine ni uzito mkubwa, mara shinikizo la damu, mara bawasiri, kisha hyperthyroidism. Tatizo moja linaisha, jingine linaanza.

Kwa sasa naweza kukaa mwezi mzima bila kushiriki tendo kutokana na hali ya hyperthyroidism pamoja na hofu ya kushindwa kufanya tendo. Nikijaribu, uume unasimama sekunde chache kisha unalala au hausimami kabisa.

Uzito wangu ni kilo 80, urefu 164 cm. Shinikizo la damu limekuwa kati ya 137/90 hadi 140/84, mapigo ya moyo 60–70 kwa dakika.

Kuanzia juzi pia nimeanza kuhisi maumivu kwenye korodani moja, sijui kama ni ngiri au tatizo lingine.

Naomba ushauri wa kitaalamu na njia sahihi za matibabu.
 
Huy ana Presha sasa sijui ya kushuka au kupanda..

But vitunguu swaumu vinashusha Presha sasa awe makini..
Tafuta tangawizi 1, vitunguu swaumu punje 7 (saga pamoja), sagia kitunguu maji 1 katia na kipande cha limao.
Kunywa 1*3

Mchana tikiti maji kipande1, parachichi 1, ndizi 2, karanga mbichi kiganja.

jioni saa 12 chai ya karafuu, hiriki, mdalasini, asali na karanga tena.

Ndani ya wiki 2 mambo safi.
 
Shida imeanzia hapo kwenye wasiwasi..
Wasi wasi ni sumu namba 1.

Fanya mazoezi, punguza hizo kilo jitahidi zirudi kwenye 60 hivi, halafu tumia vitu Intelligent businessman
Kakushauri, fanya hivyo miezi miwili mpaka mi3, utapona usipopona hapo njoo, tukusaidie zaidi
Mazoezi muhimu sana, kamba, squats, bridge legs, baiskeli.
 
Habar mim baba wa watoto4 Umri miaka38 Niko matatizo la hyperthyroidism diffused multnodullar goita kwa miaka3,Sasa hapo awali kabla ya huu ugonjwa wa hyperthyroidism nlikua nashida ya nguvu zakiume kwa miaka7,

Sasa baada kuhainga nakuwa ktk dozi ya hyperthyroidism nguvu zakiume zilizid kupingua nkakutana na Prof wa urology akanisdikia dawa ya tadalafili mg5 ili kutibu shida ya nguvu zakume,Sasa nimetumia dawa hii ya tadalafili kwa mara20+ ktk vipindi tofaut ndani yamiaka3 ila tatizo la nguvu zakiume haijaisha na pia hyperthyroidism ipo pale pale

Sasa Hadi Sasa Sina hisia kabisa na mke nguvu hamna nkiwa usingizini uume inasimama vizur tu,ila nkimuhitaji mke hata tukiandaana Sina msisimuko uume hausima au unaweza simama legelege nkiingiza ukeni unalala,Hali hii imepelekea kuwa na hofu nawasiwasi pindi mke ahitajipo tendo au mim nkihataji bas ntajikuta siwezi uume haisimami,Hali hii ipo kwa kipindi kirefu Sasa zaid ya miaka3 tangu niwe hyperthyroidism nahata kabla pia

Mpaka nimewaza vibaya kuwa au ntakupa nimerongwa ila staki kuamini mambo ya ushirikina
Mara magonjwa hayaishi kuniandama kwa miaka12 Sasa mara uzito mkubwa,mara preshha,mara bawasili,mara hyperthyroidism yaan linatola hili linakuja Lile

Naweza kaa mwezi sijashiriki tendo sababu ya hyperthyroidism na kwakuogopa kufeli nawasiwasi hofu yakushindwa nanikijaribu bas uume utasimama ukiingia sekunde unalala ukeni au hautasimama kabisa,nna kg80 urefu 164cm,BP 137/90,140/84 prc70,60

Wakuu nauhitaji msaada wenu waushauri na matibabu.pia tangu juzi nimeanza hisi maumivu ya korodani moja sjui ni ngiri ana
Mna angaika sana....mwili ni kama gari lazima uchoke na muda wa kuchoka umetofautiana kutokana na mambo mbalimbali kama magonjwa ajali umri...nk
 
Mkuu Pole sana
Jaribu kuepuka vyakula vinavyoweza kuvuruga dawa za
matibabu yake
Acha kutumia chumvi kabisa kwenye chakula chako
Na pia acha....
Mayai
Kuku
Maini
Maziwa na Mtindi
Samaki
Kahawa
Vyakula vya sukari nyingi

Pia anza kufanya mazoezi ya mwili na viuongo , kukimbia, kuruka kamba.....
 
Mna angaika sana....mwili ni kama gari lazima uchoke na muda wa kuchoka umetofautiana kutokana na mambo mbalimbali kama magonjwa ajali umri...nk
Wewe umekuja na huku,ulishwandwa lile swali, sikupi jibu...
Haya fanya hili la chekechea kama unaweza......

1760392864895.png
 
Pole sana; Utateseka sana maana unamuwazia mke na huo ndo Mthihan ukubwa unaokupa hofu.

Kuna wanawake wengi sana wanatoka nje na wala watume zao hawana Hilo tatizo.

Mimi Sina msaada kwenye tiba, ila Nina msaada eneo Moja, usimuwaziw mke wako sana, utakufa kwa mawazo.

As long as yupo, anakuheshimu, wewe usiwazw anapata wapi tendo la ndoa, kama ni shida sana atajiongeza.
 
Kwa hilo tatizo lako approach yangu ni kama ifuatavyo.

Kuondoa inflammation.
Kwa kutumia diet(sio mboga na matunda) na fasting Kupunguza stress ya mwili kusaga chakula na concentration iwe kwenye healing.

Liver detox.
Una historia ya magonjwa huko nyuma obviously ini limekuwa katika kazi ya ziada.

Heart rhythm.
Unaweza kuona havihusiani Ila watu wengine wanakuwa misdiagnosed na hiyo ishu ya nguvu za kiume problem si hyperthyroidism bali ni metabolism problem.

Rebuild stage.
Tatizo la thyroid litakuwa address separate kwa herbs kama Lycopus, Melissa n.k.

So ku deal na ishu yako nahtajika total reset ya mwili, Naongelea in herbal protocol sio symptoms treatment.
Hii reset itachukua miezi mpaka kuwa Sawa.

Kama unataka magic pill ngoja wataalamu waje.
Tafuta tangawizi 1, vitunguu swaumu punje 7 (saga pamoja), sagia kitunguu maji 1 katia na kipande cha limao.
Kunywa 1*3

Mchana tikiti maji kipande1, parachichi 1, ndizi 2, karanga mbichi kiganja.

jioni saa 12 chai ya karafuu, hiriki, mdalasini, asali na karanga tena.

Ndani ya wiki 2 mambo safi.
😂
Kuwa serious basi jamaa anaumwa
 
Kwa hilo tatizo lako approach yangu ni kama ifuatavyo.

Kuondoa inflammation.
Kwa kutumia diet(sio mboga na matunda) na fasting Kupunguza stress ya mwili kusaga chakula na concentration iwe kwenye healing.

Liver detox.
Una historia ya magonjwa huko nyuma obviously ini limekuwa katika kazi ya ziada.

Heart rhythm.
Unaweza kuona havihusiani Ila watu wengine wanakuwa misdiagnosed na hiyo ishu ya nguvu za kiume problem si hyperthyroidism bali ni metabolism problem.

Rebuild stage.
Tatizo la thyroid litakuwa address separate kwa herbs kama Lycopus, Melissa n.k.

So ku deal na ishu yako nahtajika total reset ya mwili, Naongelea in herbal protocol sio symptoms treatment.
Hii reset itachukua miezi mpaka kuwa Sawa.

Kama unataka magic pill ngoja wataalamu waje.
😂
Kuwa serious basi jamaa anaumwa
Kwaiyo ushauri wako ni upi boss Nini nifanye nipone
 
Pole sana. Mungu Atajaalia Utapata ufumbuzi wa tatizo lako
Hivi wewe hauna dawa kweli?
Embu msaidie mdau tiba kidogo.
Dawa ni kuwa na mwanamke asiyekupa mashinikizo ya tendo.
Anaekusaidia kukutuliza kukuambia usijipe shinikizo bado anakupenda na kukuheshimu hata kama hapati huduma ya ngono kwa kiasi kinacho mtosheleza.
Just kidding 😜
 
Kwaiyo ushauri wako ni upi boss Nini nifanye nipone
Anza na diet. Ketogenic diet. High fat and zero carbohydrates. Nyama nyekundu yenye mafuta mengi hasa ng'ombe, mbuzi, kondoo,samaki wenye mafuta mengi. Mafuta mengi itakuwa source ya energy badala ya sukari ambayo ni chanzo Cha inflammation.
Asiguse matunda yana sukari (fructose), ngano,ugali, wali(hizi ni forms of sugar, carbs).
Kaa mbali na seed oil (alizeti, canola).

Mboga kidogo sana. Hasa Seaweed, yale majani majani ya baharini ni the best yana madini mengi.
Maini mara moja kwa wiki(hii ni multivitamin Ila usizidishe)
Mtindi mara moja moja(kwa bacteria wazuri tumboni)

No breakfast ni mwendo wa brunch(breakfast lunch) kula kuanzia saa 5 mchana au saa 7 mwisho saa 2 usiku.
Ukijaribu hii system utaona mabadiliko ambapo hali itakuwa mbaya siku za mwanzo hii inaitwa Keto Flu, ni mwili unajisi reset Kisha hali itaanza kuimarika.

Kumbuka Mafuta mafuta mafuta. Kwa wingi.

Herbs Tafuta.
Hawthorn kwaajili ya heart rhythm.
Milk thistle kwa liver detox
Bugleweed kwa thyroid
Melissa kwa nerves
Ashwaghanda kwa stamina.

All the best.
 
Habarini, mimi ni baba wa watoto wanne, nina umri wa miaka 38. Nimekuwa nikiugua hyperthyroidism (diffused multinodular goiter) kwa miaka mitatu sasa.

Kabla ya kuanza kuugua hyperthyroidism nilikuwa na tatizo la nguvu za kiume kwa takriban miaka saba.

Baada ya kugundulika na hyperthyroidism, tatizo la nguvu za kiume lilizidi kuongezeka. Nilimwona Profesa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo (Urology) ambaye aliniandikia dawa ya Tadalafil 5mg ili kusaidia kurejesha nguvu za kiume.

Nimekuwa nikitumia dawa hii kwa zaidi ya mara 20 katika vipindi tofauti ndani ya miaka mitatu, lakini tatizo halijaisha na hyperthyroidism bado ipo.

Kwa sasa sina hamu kabisa ya tendo la ndoa na nguvu za kiume zimepungua. Nikiwa usingizini uume unasimama vizuri, lakini nikijaribu kushiriki tendo na mke wangu, hamu haipo kabisa.

Wakati mwingine uume hausimami, au ukisimama unakuwa legelege na unalala mara tu ninapoanza tendo. Hali hii imeniletea hofu na wasiwasi kila ninapotarajia au kuhitajika kushiriki tendo.

Tatizo hili limekuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, tangu nipate hyperthyroidism, na hata kabla yake kulikuwa na dalili. Wakati mwingine nawaza labda nimerogwa, ingawa sitaki kuamini mambo ya kishirikina.

Kwa miaka 12 sasa nimekuwa nikikumbwa na changamoto mbalimbali za kiafya mfululizo. Wakati mwingine ni uzito mkubwa, mara shinikizo la damu, mara bawasiri, kisha hyperthyroidism. Tatizo moja linaisha, jingine linaanza.

Kwa sasa naweza kukaa mwezi mzima bila kushiriki tendo kutokana na hali ya hyperthyroidism pamoja na hofu ya kushindwa kufanya tendo. Nikijaribu, uume unasimama sekunde chache kisha unalala au hausimami kabisa.

Uzito wangu ni kilo 80, urefu 164 cm. Shinikizo la damu limekuwa kati ya 137/90 hadi 140/84, mapigo ya moyo 60–70 kwa dakika.

Kuanzia juzi pia nimeanza kuhisi maumivu kwenye korodani moja, sijui kama ni ngiri au tatizo lingine.

Naomba ushauri wa kitaalamu na njia sahihi za matibabu.
Pole sana ndugu
Kwa sasa, ningependekeza:

1. Ufuatiliaji wa Tiba ya Hyperthyroidism: Ni muhimu kushauriana tena na mtaalamu wako wa magonjwa ya Endocrinology kuhusu matibabu ya hyperthyroidism yako. Matatizo ya nguvu za kiume yanaweza kuongezeka ikiwa tatizo la thyroid halijatibiwa ipasavyo. Hivyo, hakikisha kwamba unaendelea kufuatilia matibabu yako na kuangalia kama kuna uwezekano wa marekebisho ya dozi au mbinu nyingine ya kutibu hyperthyroidism.


2. Uchunguzi wa Tatizo la Korodani: Maumivu kwenye korodani moja yanaweza kuwa ni dalili ya tatizo la hernia au la zingine, kama vile epididymitis au infeksheni. Hii ni muhimu kuchunguzwa na daktari wa magonjwa ya mfumo wa mkojo au mtaalamu wa upasuaji ili kujua chanzo cha maumivu hayo na kupata matibabu sahihi.


3. Matibabu ya Erectile Dysfunction (ED): Tadalafil inaweza kuwa haifanyi kazi vizuri ikiwa tatizo linahusiana na hali ya juu ya homoni au shinikizo la damu. Ikiwa hujafanya hivyo tayari, unaweza kuzingatia kufanya uchunguzi wa kina kuhusu homoni zako (kwa mfano, testosterone, prolactin, nk.) pamoja na afya yako ya moyo. Uwezekano wa tatizo la kisukari pia unaweza kufuatiliwa, kwani kisukari pia kinaweza kuchangia ED.


4. Mashauri ya Kisaikolojia: Kuishi na hali ya kiafya kama hii mara nyingi kunaweza kusababisha wasiwasi na hofu, ambayo pia inaweza kuathiri nguvu za kiume. Kuwasiliana na mtaalamu wa afya ya akili (psychologist) au mshauri wa afya ya kijinsia kunaweza kuwa na manufaa katika kupunguza shinikizo na kuboresha hali yako ya kihisia, ambayo inachangia sana katika utendaji wa tendo la ndoa.


5. Shinikizo la Damu: Shinikizo la damu unaloshuhudia linaweza pia kuwa na athari kwa nguvu za kiume, hivyo ni muhimu kuendelea kufuatilia shinikizo lako la damu na kuzingatia mabadiliko ya mtindo wa maisha kama vile kupunguza chumvi, kufanya mazoezi, na kula vyakula bora. Dawa za shinikizo la damu pia zinaweza kuchangia matatizo ya nguvu za kiume, hivyo ni jambo la muhimu kulizungumzia na daktari wako.
 
Back
Top Bottom