CCM hawataki mabadiliko ya haki kwa vile ubatili wa sasa unawanufaisha/yanawanufaisha.
Siku ikitoka madarakani, CCM itayadai haya haya yanayopiganiwa na chadema maana ndio UKWELI NA HAKI.
CCM tendeni haki ili kesho HAKI iweze kuwalinda, vinginevyo mnajipalia mkaa! Mkitoka mtakuwa kama KANU maana kila mmoja atakumbuka atrocities mlizowatendea wengine na mtalipizwa visasi kama siyo kufutika kabisa.
Senegal wanabadiri Tume ya uchaguzi iwe chombo huru, iwe kama moja wapo ya mihimili ya dola inayojitegemea kama mahakama, bunge na executive, wangelikuwa na akili kama za CCM wangelimaintain hiyo tume maana kwa sasa walioingia madarakani vitawalinda kuiba kura huko mbele. Wameamua kutenda haki na kweli.
Kuna watu bado wanaona maisha ni mazuri kwa sababu wanakula na kunywa bia kama Chalamila.
Ila hawaoni hali ya baadae kwa vizazi vijavyo na sera za dunia kiuchumi kuwa hazitaweza kamwe kumsaidia Mtu mnyonge kuishi duniani zaidi ya kwenda uhamishoni huko Ahera.
Kama ardhi inauzwa ,bandari inauzwa ,wanayma wanauzwa , Misitu inauzwa, Viwanja vya ndege vinauzwa , Bahari wanapewa wakorea wavue samaki wapeleke kwao halafu wabongo wabaki na mapanki kama kule mwanza enzi zile za JK, ni wazi kuwa bila kuitoa CCM madarakani hali itakua mbaya kwa wananchi huku watawala wakiwa mabilonea kwa kodi za wananchi.
Nilimsikiliza Mwiguli akisema kuwa wanakopa ili wajenge barabara. Yaani ni mambo ya aibu kabisa kuwadanganya wanatanzania.
Ndugai aliweka wazi kuwa nchi itapigwa mnada.
Yaani kwa sasa tumefikia mil.65 katika kipindi ambacho wafanyakazi na walipo kodi wengine wanakamulia tozo na kikokotoo na kodi za kila aina . Wakati ambao kuna makampuni mengi ya Kamari na yanalipa kodi mamilioni ya pesa kila dakika. Wakati ambao line za simu zinalipiwa kodi kila mwezi na kila dakika ukiweka vocha na kutuma pesa.
Wakati ambao ukinunua umeme hata kama ni mpangaji unakatwa pesa ya kumiliki nyumba, wakati ambao kila Magufuli alijitahidi kujenga madaraja na kuunganisha kila mkoa na wilaya na kujenga stendi na masoko makubwa karibu nchi nzima ,wakati ambao Magufuli alikua amepanua bandari ya Tanga ,mtwara na Tanga,wakati ambao kila lita ya mafuta inakatwa pesa za TARURA,TANROAD na REA. Wakati mbao mabasi yanalipa mabilioni ya pesa Latra kwa faini za VTS,Wakati amabo watalii wameongezeka kutokana na ugonjwa wa korona kuisha,Wakati amabo tumepata pesa za kiuza bandari na misitu na viwanja vya ndege,wakati ambao tuna walipa kodi wengi zaidi kutokana na kuongezeka kwa idaidi ya watu,wakati ,ambao kuna ongezeko la viwanda kama vile vya sukari na Sementi na wakati ambao Bunge ni la Chama kimaoja .
Sasa waziri anashindwa kutuambia Pesa zinazokatwa kwa ajili ya TARURA zinakwenda wapi. Kwa nini tusiambiwe zinapatikana Sh. Nagapi kwa Mwaka na zinatumika sh.Ngapi. kwa nini zisitumike hizo mana zinakatwa kwenye umeme,maji na Mafuta . Hii nchi imekosa msimamizi makini. Ni bora atokee mtu jasiri kama Makonda awahiji watendaji kwa data kuwa kama mfano tunakusanya bil 500 kwa mwaka za Tarura kwenye mafuta na Umeme na bado nyingine za barabara. Inakuaje tushindwe kuwatumia wajenzi wa ndani kujenga barabara za vijijini kila mwaka km 500. Ambapo ukishajenga mwaka huu mwaka kesho unasonga mbele na kupunguza eno la kujenga miundombinu.
Tunakopa lakini utasikia zimejengwa barabara km 12 ,au 70 na zinachukua hata miaka mitano mpaka uchaguzi ujao.
Futa Safari za nje + Tozo za mafuta TARURA na TANROAD+ Tozo za TARURA kwenye umeme ni pesa nyingi sana kama zikisimamiwa vizuri na Mtu kama Paulo Makonda kwa CCM lakini kwa sasa ni Lisu wa Chadema ndiye ameonyesha njia mana Makonda bado anaunga mkono jitihada za kuuza nchi na kusafriri na mikopo inayosimamiwa vibaya na serikali ya CCM
2025 Tumweke Mtanzania anayeweza kubishana na wawekezaji kwa sababu ya kujua sheria na haki za wananchi kwenye Rasilimali zao.
JPM alikua mwanasayansi lakini pia alikua na uzoefu wa miaka 20 kwenye uwaziri. Hivyo ilikua ni rahisi kukataa jambo ama kisayansi lakini kwa uzoefu wa kujua mbinu za upigaji.
Ndio maana Alikua analifuatilia na kuangalia mwenyewe sio kuwaomba watu wamsaidie kama ilivyo sasa , "Hili nalo Mkaliangalie " badala ya kusema hili nitaliangalia na kulichunguza nikinaini kuwa mnafanya tofauti nitawatoa wahusika.
Hili nalo makaliangalie as if halimhusu yeye na hana muda wa kuliangalia..