Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Usiogope kuongelewa kijana wewe jiangalie mipango na maisha yako mtu anayeongelea watu mara nyingi ana ishu ya kufanya ndio maana anapata muda wa kukuongelea pga moyo konde fanikisha lengo lako
 
Miaka 30 bado unasubiri kupewa ramani na bro wako, si uingie mtaani upambane.

Hauko serious na maisha.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Njoo nikuhifadhi kwangu huku unatafuta ramani yako ya maisha.
 
Usijichanganye eti uuze simu utoke kwa bro ukaapangishe,ukishalipa kodi utakuwa unakula nini...Yani ni bora uuze hio simu alafu io pesa ya simu uone namna ya ufanye nini nayo ukiwa apo apo kwa broo yani ukitoka kwa bro uwe una uhakika na kitu cha kufanya....Binadamu tumeumbiwa kusema tangu kuzaliwa kwetu,maneno yetu yasikutishee[emoji110]
 
Sasa hyo hela braza ako si angekupeleka VETA ukachukue fani yoyote ila bado hujachelewa km braza bado ana nia ya kukuendeleza kielimu kachukue long course VETA ya electronics umri bado unao mwingi tu wa kujipanga usikimbilie maisha
 
Sasa hyo hela braza ako si angekupeleka VETA ukachukue fani yoyote ila bado hujachelewa km braza bado ana nia ya kukuendeleza kielimu kachukue long course VETA ya electronics umri bado unao mwingi tu wa kujipanga usikimbilie maisha
Bro akili yake ipo kwenye ufundi wa simu yani awazi kingine baada ya kuhitimu masomo pia ajanipa msingi wowote
 
Utahama huna kipato? Utaishije

Baki hapo mradi hujafukuzwa ila weka juhudi ya kazi
Umemshauri vema kitaa unga Wa ugali kilo 2000 sasa kama anajua ni rahisi mbona anakula Milo mitatu hapo atajua hajui akitoka

Akajichanganye kwa mafundi baada ya mwka atakuwa yuko vizuri ndio atoke kwa bro
 
Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.

Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.

Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.

Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.

Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.

Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.

Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.

Dah nimeoa na 26
 
Back
Top Bottom