Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.

Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.

Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.

Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.

Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.

Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.

Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
Du! Yaani unazeeka hata kabla ya kuanza maisha! Nenda kajenge au kapange uwe na kwako badala ya kuwa chawa
 
Hakuna lisilowezekana mwanangu. Jiongeze utafanikiwa.
Ahsante ndugu yangu hakika naenda kupambana sana na sifanyi makosa tena nimechelewa sana lakini bado kuna mtu anakwambia ubaki kwa bro ujipange kwa mwaka na nusu aisee hiyo kitu siwez japo sina fedha ila ntaenda kupanga kigumu mengine yatajulikana huko mbele ila kurudisha mpira kwa kipa siwez
 
Bro wangu ana daycare nusery school na kaajili watu zaidi ya kumi pia ana school bus kadhaa ila cha kushangaza ni huwa apendi sisi tusogee kazini kwake kwahiyo hata kutuajili awez anaajili watu baki tu
Usimlaumu kwa hilo bro anaelewa hata wewe najuwa unaelewa mambo ya bosi kugombeza mfanyakazi wake sasa yeye hayupo tayari kufanya hivyo kwa ndugu zake na unajuwa kabisa kazi hizi za kuajiliwa zilivyo full kufatiliana na kufokewa we utamuona kaka ako mbaya tafuta mishe jiingize huko kwenye cctv camera au kwenye cm.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.

Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.

Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.

Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.

Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.

Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.

Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
Uza simu hii kubwa Kisha andika Uzi wa kiasi utakachokua nacho mkononi Kisha watu watakupa idea ya kitu gani uanze nacho kwa mtaji wako huo mdogo.

Itakua Bora zaidi ukaanza na inshu za protector za simu hii itakupa channel zaidi maana tayari una ujuzi wa simu pia.
 
Usimlaumu kwa hilo bro anaelewa hata wewe najuwa unaelewa mambo ya bosi kugombeza mfanyakazi wake sasa yeye hayupo tayari kufanya hivyo kwa ndugu zake na unajuwa kabisa kazi hizi za kuajiliwa zilivyo full kufatiliana na kufokewa we utamuona kaka ako mbaya tafuta mishe jiingize huko kwenye cctv camera au kwenye cm.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Nimekuelewa kaka upo sawa sana
 
Uza simu hii kubwa Kisha andika Uzi wa kiasi utakachokua nacho mkononi Kisha watu watakupa idea ya kitu gani uanze nacho kwa mtaji wako huo mdogo.

Itakua Bora zaidi ukaanza na inshu za protector za simu hii itakupa channel zaidi maana tayari una ujuzi wa simu pia.
Ahsante mkuu nimekuelewa
 
Kama uko interested kufanya kazi uarabuni njoo nkupe mwongozo inbox.

Maisha hayana formula, mimi nilishika sana pesa nikiwa na miaka 18 tu mpaka nikiwa na miaka 29 lakini nilikua mpumbavu sikufanya maendeleo. Labda cha kujivunia wakati huo ilikua ni wana niliowasaidia ambao nao hawakuja kunifaa nilipoanguka. Miaka 30-32 nilikua choka mbaya nikarudi kukaa kwa mama mzazi. Baada ya hapo mambo yakanyooka na sikufanya tena makosa yangu ya nyuma.
Maisha ni kujifunza kutokana na makosa
 
Njoo Singida tulime alizeti,Dar utapoteza sana muda kama kaka yako mwenyewe bado anakaa kwenye chumba kimoja unategemea nini?[emoji276]
 
Nipe namba zako mkuu mimi wala sichagui fursa kama nafasi ipo nakuja tu
 
Dharau zimekuja baada ya kuwaruhusu wakujue na kukuzoea. Niskilize hapa kwa makini.
1.Amka asubuhi moja kinunda sana, salamu basi jikatae, misaada ya ki wacky sijui unaenda nje unarudi sasa hivi nichukulie vocha goma, niitie fulani kaa kimya. Mara wiki kadhaa utaskia "siku hizi umebadilika" usijitetee jibu kikauzu NDIO.(HAPA UNARUDISHA HESHIMA).

2. Usihame kwanza, tumia hayo maarifa ya kutengeneza simu, mwambie brother akupe pesa kidogo kama 360k, anza kununua simu mikononi smart za kawaida infinix,techno,e.t.c unaweza pata hata tatu kwa bei ya chini uza kwa bei ya juu kidogo.Ambatanisha na issue ya kwenda kwa fundi simu kufanya kazi kama msaidizi ila usikae katika usaidizi kwa zaidi ya mwezi, kuwa fundi(JIAMINI) umesoma,ikikushinda unaomba assist kwa mafundi wengine.
3.Issue za mademu potezea, bora upige za kushtukiza tu mbali na mtaa wako. Halafu usipende kutongoza mademu wenye njaa kama wewe,tongoza matured na mpambanaji.Sasa huna kitu na unataka demu ambae hata vocha hawezi jinunulia si atakupa stress za kila saa kutoa masimulizi ya njaa na misemo kama vile "siko poa,tucheki kesho"😆
4.Endelea kujifunza ufundi youtube,na kusoma soma, google vitu mkuu.
5. WAZA MAMBO MAKUBWA,NGUVU UNAYO
 
Sijashindwa tatzo sina connection hata ya kupata kazi nilishaomba humu hata kuwa kama kibarua sikupata msaada
Askari wa miguu, humu msaada ni 0% to 5%, mara mia uandae vipeperushi vya huduma na gharama na utenge siku uvagae maeneo ya majumba na ofisi uwape offer yako.
Weka huko instagram,facebook n.k
Hawa wanaokuona kama umembwele wana ndugu zao kibao tu wanaishi kama wewe, tena wamewachunia, hata wakiombwa 10k hawatoi.
Wengi kama sio wote humu ukumbuke ukirudi generations chache tu baada ya baba unakuta wachunga ng'ombe n.k ni koo za kimaskini. Usipanic😆😆😆.
Ukiona mtu ana nyumba hata 2 range rover sita, ukienda kidogo tu kwenye ukoo wao utakuta kuna wauza mihogo,chapati mtaani hata wakisema huyo mtu ni mjomba,ba mdogo watu wanashangaa na hawaamini.
Bongo life la kifala usipanic kabisa. Puuza wapuuzi. Kuwa kaksi.
Nadhani unacheka cheka sana na raia,ukumbuke huku sio kwenu,nuna.Cheka kwenye deal na sherehe tu,na mara chache ikilazimu😆.
 
Back
Top Bottom