Nina uraibu wa kutegemea sana chatGpt, nisaidieni namna ya kuacha

Kujua tatizo ni mwanzo WA kutatua tatizo
 
Ukiweza kuifanya GTP ikupatie fedha ndio huo uraibu utakuwa na maana.
 
Ushauri huu ametoa mwenyewe unaemtuhumu kwako

 
Huwa natumia ku solve changamoto za maisha.
Mfano nikiumwa ulimi ,napiga picha kisha natuma kwenye chatgpt,ina nipa majibu.
ULimu wako mrefu na umevimba.

Kwa kweli naona hakuna changamoto,maisha yana bore
Juzi kati hapa Kuna mwamba katoka kupiga x-ray, ikaitupia Ile picha na kuiliza ifanye interpretation, alichojibiwa ndo hicho hicho alichoenda kuambiwa na daktar, dawa tu ndo zilikuwa tofauti.
Chatgpt ni nzuri kama unaitumia wisely.
 
Sioni kama kutumia ChatGPT ni uraibu. ila matumizi yako ndio yanamtofautisha mtu na mtu.

Kwa maelezo yako unaitumia GPT kama search engine, which is cool.
ila pia kama unaitumia kupangilia vizuri mawazo yako ambayo yako scattered ni jambo zuri...

GPT ni tool kama zilivyo nyingine tu... Designers wanaitumia, Writers, Preachers n.k n.k.

ila ukitaka kujiimarisha jifunze kutumia akili yako kujiboresha kwa ku engeneer prompt vzr, ili app itengeneze algorithm ya kukuboreha na sio kukudumaza

Nenda kwenye settings za gpt, iamrishe mambo na namna unavotaka kupata majibu na ikupe challenge za kuboresha kumbukumbu na uelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…