Mwanachama #001
Tafadhali ficha kitambulisho changu Mheshimiwa.
Najua nimemkosea Mungu na ubinadamu..pole pole napoteza akili yangu...sikutaka yoyote haya...Nina miaka 25, mama na mke , nina VVU lakini mume wangu hajui.
mwanzoni mimi nilidhania alijua.maana nilihisi nilipata kwake... Nilikutana naye 2016, kisha nikabainika kuwa na VVU wakati nilienda klinic kwa
pole Dada yangu, huwez jua mipengo ya Mungu kat yako wewe mwenye vvu na mumeo Nan atatangulia mbele ya haki.
Hivyo basi kwa kuwa dhamila yako haitaki apate magonjwa mumeo, nakushauri ufanye mambo yafuatayo:-
Kwanza tambua Mungu anasamehe ata Kama ulidanga au vyovyote, Muombe msamahaa then acha kabisaaa kila siku kujihukum. Jikabidhi kwake na familiya yako mkaombe rehema za Mungu. Atasikia
Pili, miaka 4 ambayo umemaliza mumeo hajapata ugonjwa ni waz Kuna ulinzi Mungu amemuwekea ili kusudi mlee watoto wenu kwa pamoja.
Tatu, ushauri wangu naona watoto wenu bado wadogo ukimwambia ndo kwanza ndoa itavunjika, baba ataoa mke mwingine au atapata kipozeo Cha mtaani na huyo mke mwingine ndo anaweza kumpa maradhi na hivyo watoto wakapata shida Sana
Hivyo basi kwa mtazamo wangu na ushauri, usimwambie kwanza subiria watoto wakue kidogo.
Lakin wakati unasubiria watoto wakue, fanya mambo yafuatayo kwa uhaminifu Sana:-
1. Meza dawa kwa ratiba kikamilifu, kula vizuri, hacha mawazo kabisaaa na uwe mtu wa kuchangamka.
2.Usikubali kabisa kabisa kabisa yaan hata kidogo, kufanya mapenzi na mumeo kabla hajakuandaa, nadhan unanielewa kuandaliwa kupi namahanisha.
Na akianza kukuandaa, weka akili yote kwake ili kuruhusu..........kulainika, ukiona wakati mwingine hauna mudi kabisa, nunua mafuta yanayofaa kitaalam ya kuweka kule chin......, Uweke kabla ya mumeo haja anza shughuri. Hii yote ni kumkinga asichubuke akiwa kwenye tendo.
3. Tatu Kama unafanya kazi, jitahidi sana kuweka akiba kubwa, kwa Siri kubwa, namahanisha ata Kama utapata hela ya kiwanja nunua kwa Siri, jina la kiwanja andika watoto wako, hati tunza kwa Siri. Hii itakusaidia ata pale utakapo kuja kumwambia baada ya watoto wenu kukua kidogo, ata Kama hatakuelewa, kale ka kiwanja katakusaidia upate pa kuishi.
Dada yangu Amin usiamin kuwa na virusi siyo mwisho wa maisha, bado unaweza kuishi mpaka ukaona wajukuu wako Kama utajikubali na kumtegemea Mungu.
Mwisho.usisimulie watu wengi, ili kusudi Siri isitoke haraka. Mungu uangalia nia ya moyo inadhamilia nini.
Naomba nisihukumiwe kwa mawazo yangu na Samahan kwa uandishi mbaya nimeandika nikiwa safarin
Barikiwa.