Nina wasiwasi na elimu za wana JF

Nina wasiwasi na elimu za wana JF

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Inapotokea inawekwa mada ya Kiingereza humu kwenye majukwaa, basi inasusiwa kama Bunge la katiba na UKAWA! Mada hiyo hiyo ikiwekwa kwa lugha ya Kiswahili, basi watu wataichangamkia kama posho, kuisoma kwa wingi na kuweka maoni yao...
Hili linanitia wasi wasi na elimu za wana JF wengi ambao wanajifanya wana tu bachelor, na wengine hata wakishindanisha vyuo vyao kwa kusema ukisoma chuo flani hufi njaa!

Naombeni mnijuze wana MMU kama lugha ya malkia ni sheedah au ni hulka tu.

Naona wengi wameanza kuja kwa jazba: But the reality, haya mambo ya kukimbia umande lugha ya Malkia ndio maana tunaingizwa mikataba mibovu coz wataaalam wengi wanapata shida ya kuitetea nchi kwa kutumia yai...
 
endelea tu kuwa na wasiwasi
 
Kwani lugha ndio kigezo kuwa mtu kasoma?...wengine kingereza ni lugha yao ya tatu au hata ya nne, wapo ambao wana Phd na hawakuzisoma kwa kingereza
 
Inapotokea inawekwa mada ya Kiingereza humu kwenye majukwaa, basi inasusiwa kama Bunge la katiba na UKAWA! Mada hiyo hiyo ikiwekwa kwa lugha ya Kiswahili, basi watu wataichangamkia kama posho, kuisoma kwa wingi na kuweka maoni yao...
Hili linanitia wasi wasi na elimu za wana JF wengi ambao wanajifanya wana tu bachelor, na wengine hata wakishindanisha vyuo vyao kwa kusema ukisoma chuo flani hufi njaa!

Naombeni mnijuze wana MMU kama lugha ya malkia ni sheedah au ni hulka tu...

Yaani wewe ndo unawakilisha hao wajinga na wapumbafu. Tunatakiwa tuwe na mashaka na elimu yako maana yaonyesha kwako wewe aliyeelimika ni anayejua kizungu.
 
Thamini cha kwako Kiswahili ndo lugha ya Taifa na kumbuka jf sio waliosoma tu ilimradi unajua kuandika na kusoma na ukakidhi vigezo na masharti ruksa.
 
elimu siyo kujua kuongea kingereza kwa ufasaha ila ni faida kwa msomi kujua lugha ya kingereza angalau cha kuweza kuchangia chochote au kutoa maoni pale lugha hii inapotumika!!
 
sasa ukiandika hivi unataraji tuchangie nini

The ministres of inside things has rufuse to work antil parlement of Laws completed.
 
sasa ukiandika hivi unataraji tuchangie nini

The ministres of inside things has rufuse to work antil parlement of Laws completed.

Mkuu umeniua na cheko...!!!
Sote twafahamu kiingereza no shida kwa watanzania lakini tunalojukumu LA kujifunza japo kidogo maana kuna mambo kweli yanatia aibu.
Kwa mfano; mpo ofisini kikao cha chai siku ya kutumia kiingereza inajulikana kabisa kwamba Leo kikao kitakuwa kifupi lakini siku za kiswahili mambo yanakuwa marefuu...!!!
 
Nafikiri kwa kiswahili na hata nikiota ndoto ni kiswahili. Nijipe shida ya nini katika kuchangia mada ya kiingereza JF. Kwani wote tumesomea lugha ya kiingereza. Kwanza hata wewe mwenyewe ni shida na kituko mbele ya wenye lugha.
Kwako nini cha ajabu wakati ndo lugha yetu ya Taifa. Nahisi utakuwa unatumia mkorogo kupata weupe wa ngozi ili ufanane nao hao wenye lugha hiyo. Pole sana kwa kuwa na mawazo hasi!
 
mista mleta mada whati do yu say?!.eer do you min zati most jf membazi don know english?.eer i think zati is not true.becoz that.........yu know.....according to mulugo,tanganyika got its independent in.....yah "thenkyo vere macheeeeee"
 
Yaani kwa mujibu wako kuwa na elimu ni kujua lugha ya kiingereza tu, je, sisi tunaosoma kwa kijapan inakuweje. Naweza kuongea na kuandika lugha fasaha tatu; Kiswahili, Kifaransa na Kijapan ina maana sina elimu ?
 
You who has started topic you think you to know english language is mean education, education is a key of life not inglish language, you want people to donate post in english? Why not our international language kiswahili?
 
Inapotokea inawekwa mada ya Kiingereza humu kwenye majukwaa, basi inasusiwa kama Bunge la katiba na UKAWA! Mada hiyo hiyo ikiwekwa kwa lugha ya Kiswahili, basi watu wataichangamkia kama posho, kuisoma kwa wingi na kuweka maoni yao...
Hili linanitia wasi wasi na elimu za wana JF wengi ambao wanajifanya wana tu bachelor, na wengine hata wakishindanisha vyuo vyao kwa kusema ukisoma chuo flani hufi njaa!

Naombeni mnijuze wana MMU kama lugha ya malkia ni sheedah au ni hulka tu.

Naona wengi wameanza kuja kwa jazba: But the reality, haya mambo ya kukimbia umande lugha ya Malkia ndio maana tunaingizwa mikataba mibovu coz wataaalam wengi wanapata shida ya kuitetea nchi kwa kutumia yai...

tukuza kiswahili wewe ukitaka kizungu ingia jf palace
 
Kwani tunashindana lugha humu!??..ka vp andika na kichina bac!
 
Je,kuna ukweli kwenye maneno ya mleta mada?Yawezekana anataka kupata/kuleta vitu vipya kwa kiingereza.Tutafakari!
 
kuna wengine tulisoma kwa lugha ya ki-polish, sasa kizungu hapa inakuwa irrelevant. na kiswahili ndo inakuwa lugha ya wengi humu. sasa ukisema mimi niwasilishe hoja humu kwa ki-polish mtaelewa?, that being said elimu has nothing to do with kidhungu!
 
Back
Top Bottom