Nina wasiwasi na mke wangu...

Nina wasiwasi na mke wangu...

Dah, pole sana.
Hapo umepigwa ndugu.
Hakuna cha safari ya Dodoma wala Singida, mkeo yupo hapo hapo Dar anapigwa miti kwa kwenda mbele.

Daah nitajua tu mwishowake mkuu ubaya haufichiki kiongoz
 
Mashemeji zako wanamuita mkeo bila kukupigia simu wewe na kukuomba ruhusa kuwa wanamuhitaji mkeo?

Sijawahi kuona hili

Nilimuacha aende ili nije kumuoji vizur nini shida ya huko mkuu
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.. Too much upole wako ndo maana mkeo kakupanda kichwani, sisemi katoka kuliwa ila ukionganisha dots hata kama hujui kusoma ila picha utaiona

Pole sana mkuu, usikuchukue tu maamuzi magumu ya kuua, yakikuzidia mpe red card maisha mengine yaendelee.
 
Hapana mkuu huwa naamua lakini hii sikutaka ku doubt coz nikimkataliga safar analalamika na kuona namuonea lakini pia nikwasababu tu kaeleza kuwa kaitwa na hajui nini shida kwa heshima tu za mashemeji nikamuacha aende ili akirud anieleze vizur hicho kilichomfanya akaitwa huko
Mzee tatizo ni wewe kwenye hiyo ndoa. Wakwe au mashemeji watamuitaje ndugu yao bila kupitia kwako?

Story yako naiona ni chai na hauko serious. Nikupe tu mfano mmoja jana nime drive Dar to Dom nilitoka saa tano nimefika saa mbili na robo usiku na waliopanda Shabiby walifika saa nne. Mkeo kaondoka saa saba kafika saa mbili usiku ni ngumu. Kama story yako ni kweli haustahili kuwa mume
 
Unasema ni Wife alafu unasema humchunguzi. Wewe nj Mpumbavu kweli wewe. Wife ni tofauti na Mchumba unayekaa nae tu, au ni tofauti na Kidemu unachoishi nacho. Mchumba au Demu wa kawaida unaweza usimchunguze kwasababu hujamuoa kwahiyo huna Mamlaka nae.

Bro! Mke anauma unatakiwa umchunguze na umuwekee mipaka. Narudia tena unatakiwa umchunguze japo kuna wapuuzi wanasema Mwanamke hachunguziki akitaka kufanya anafanya tu, ni bora umchunguze ujue ili akizingua Kama mnaachana muachane kiroho safi.
 
Aisee labda mimi ni dikteta, ndugu zake hata wazazi wake wakiwa wanamuhitaji hunipigia mimi kuniomba nimruhusu aende.
 
Habar wana JF,
Naimani mko wazima.

Kiukweli nimekuwa na wasiwasi na safari ya wife, sijui kwanini lakini ni safari ambayo siielewi kabsa wakuu. Nina mashaka nayo coz naona mapicha picha tu.

Ni kwamba wife kasafiri juzi ijumaa kuelekea Singida lakini safari yake sielewi elewi kabisa, kwasabubu kwanza ni safari ya kushtukiza lakini pia mpaka now sielewi aim ya safari ni nini mpaka now.

Alhamisi amerudi kutoka kazini usiku tunalala ndiyo ananipa taarifa ya kuwa kesho Ijumaa anasafiri, nikamuuliza unaenda wap? Akaniambia kapigiwa simu na dada zake wamemuita ambao wanakaa Singida. Nikamuuliza kunatatizo akasema hapana, ila sijui wanashida gani na mimi ndiyo wamenipigia simu niende.

Kiukweli nilikuwa nimechoka nahitaji kupumzika, sikutaka ku complicate kitu, nikamjibu sawa nikalala. Then asubuhi nikajiandaa nikaenda kazini vizur. Niko job ananipigia simu kuwa ndiyo anatoka home anaelekea stendi kupanda bus. Iikuwa almost kama saa 7 hivi mchana nikamjibu haya na nikamuuliza kama kunakitu chochote anahtaji akasema hapana yuko powa.

Basi nikakata simu lakini kiukweli ghafla akili yangu ilishikwa na wasiwasi juu ya safari yake but sikutaka ku doubt anything nikapotezea. Baadaya kupita kama lisaa akanitumia message kuwa amepata basi but akifika Dodoma atashuka kuna ndugu yake anamchuka then wanaenda wote.

Daah, sikutaka pia ku doubt wala mambo mengi nikamjibu sawa, nikaachana naye nikaendelea na kazi zangu, but bado sikuona sababu ya yeye kushuka Dodoma. By saa 2 ndiyo ananiambia ndiyo wanaondoka Dodoma nikamjibu sawa safari njema tukaacha hivyo. Basi mi nikarud home usiku kwakuwa nilishapita somewhere nikapata chakula nikafika home niko good, nikaoga nikaingia kwa bed nikampigia ananiambia kashafika ila kachoka na safari nikamuacha nikapumzika.

Sasa leo Jpili tumeongea asubuh vizur tu na tukaagana baadae by saa 7 mchana ananiambia ndiyo anataka kurudi leo. Nikamuuliza mbona hukuniambia asubuhi na kwanini usingeondoka asubuhi? Sijaona cha maana anachonijibu, basi nikamwambia haya kama unarudi leo. Tuakaacha baada ya kama nusu saa ananipigia simu ananiambia kuwa yupo stendi, mara gari sijui hakuna, mara zimejaa, mara nimechoka nasikia usingizi, nikamwambia sasa siungebaki ili uondoke kesho asubuhi akasema sawa tukaacha.

Baadae ananitumia message eti amepata gari ila linaishia Dodoma kwaiyo atashuka Dodoma. Aloo nikasema kimoyomoyo hapo Dodoma hapo siyo bure, coz kwenda kashuka Dodoma kurudi baada arud kesho kama kweli kakosa usafiri na tumekubalina anarudi kesho mapema na sidhani kama kweli alikosa usafiri by that time ananiambia kuwa kapata usafiri.

Ila unaishia Dodoma so ataenda kulala Dom, sikutaka ku complicate nikamjibu sawa basi nikaachana nae. Ila cha ajabu baada ya hapo akawa kimya hakusema kama kafika au laa. Yaani ndo ananitumia text saa hii, saa 5 usiku kuwa alifika salama ila alishindwa kuniambia coz vidonda vya tumbo vilimshika akafikia kupumzika. Heheheh nacheka ila najua mwenyewe wakuu but sijamjibu na sitamjibu lakini namsubiri arudi kesho nikitoka kazini anieleze vizuri kuhusu hii safar yake.

Japokuwa mimi siyo mtu wa kumchunguza mwanamke na sipendi kabisa kuchunguza mtu sababu naelewa what’s gonna happen.

Wakuu kama kuna la kuniongezea karibuni sana, uwanja ni wenu.
Huyo ni mkeo kabisa au ni mnaishi kishkaji tu?
Namaanisha ndugu zake wanakutambua?
Hao ndugu zake wa Dodoma na wa Singida unawajua na wanakujua na una mawasiliano yao?
Je uliongea nao kujiridhisha kama kweli wanamuhitaji aende?
Maswali ninayo mengi ila jibu kwanza hayo tujue pa kuanzia
 
Shemeji alipaswa kukupigia na kukuomba wewe umruhusu mkeo. Ujachelewa sana simama imara
Hapana mkuu huwa naamua lakini hii sikutaka ku doubt coz nikimkataliga safar analalamika na kuona namuonea lakini pia nikwasababu tu kaeleza kuwa kaitwa na hajui nini shida kwa heshima tu za mashemeji nikamuacha aende ili akirud anieleze vizur hicho kilichomfanya akaitwa huko
 
Hapana mkuu huwa naamua lakini hii sikutaka ku doubt coz nikimkataliga safar analalamika na kuona namuonea lakini pia nikwasababu tu kaeleza kuwa kaitwa na hajui nini shida kwa heshima tu za mashemeji nikamuacha aende ili akirud anieleze vizur hicho kilichomfanya akaitwa huko
Hao dada zake unawajua?
Na uliongea nao hata kwa simu kupata ukweli?
 
Back
Top Bottom