GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Nina Kumbukumbu ya nchi kadhaa barani Afrika ( ikiwepo Kenya ) na hata za huko Kwingineko duniani zilizokuwa na 'Kiherehere' cha kuwa Vinara wa Upambanaji wa Ugaidi duniani jinsi ambapo ziligeuka kuwa 'Target' ya Mashambulizi ya Makundi ya Ugaidi yaliyopelekea Vifo na Uharibifu mwingi.
Je, Mamlaka ya Tanzania imekubali kuwa Kituo cha Mapambano ya Ugaidi ili ipate Pesa nyingi kutoka kwa Mataifa Matajiri na UN ili 'wazipige' au Tanzania ina uhakika kuwa ina Uwezo mkubwa wa Kijeshi, Kiusalama na Kiulinzi Barani Afrika na huenda hata duniani pia?
Nimesikitishwa mno na Maamuzi haya ya 'Kukurupuka' na sasa kwa hiki 'Kiherehere' chetu cha kutafuta Sifa na kutaka kupata Pesa kutoka UN na kwa Mataifa Makubwa na Tajiri tujiandae kuwa 'Target' ya akina IS, Al Shabaab na Al Qaeda ( kama bado wapo ) na wakianza Kutuvizia, Kutupiga na Kutuua tafadhali tusianze kusema kuwa wasababishi wa Matendo hayo ya Ugaidi ni Wanasiasa wetu wa Vyama Vikubwa vya Upinzani nchini Tanzania.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stegormena Lawrence Tax usingelikubali hili kwa 'Kukurupuka' badala yake ungelipima Kwanza kutokana na Mifano iliyoko ya nchi zilizokuwa na 'Kiherehere' kama hiki chetu jinsi zilivyokiona cha Moto kwa Mashambulizi ya Makundi makubwa ya Ugaidi duniani.
Binafsi nimesikitika mno na ninaogopa!