Nina wasiwasi sana kwa 'Kiherehere' cha Tanzania Kukubali kuwa Kituo cha Mapambano ya Ugaidi Afrika

Nina wasiwasi sana kwa 'Kiherehere' cha Tanzania Kukubali kuwa Kituo cha Mapambano ya Ugaidi Afrika

Nina Kumbukumbu ya nchi kadhaa barani Afrika ( ikiwepo Kenya ) na hata za huko Kwingineko duniani zilizokuwa na 'Kiherehere' cha kuwa Vinara wa Upambanaji wa Ugaidi duniani jinsi ambapo ziligeuka kuwa 'Target' ya Mashambulizi ya Makundi ya Ugaidi yaliyopelekea Vifo na Uharibifu mwingi.

Je, Mamlaka ya Tanzania imekubali kuwa Kituo cha Mapambano ya Ugaidi ili ipate Pesa nyingi kutoka kwa Mataifa Matajiri na UN ili 'wazipige' au Tanzania ina uhakika kuwa ina Uwezo mkubwa wa Kijeshi, Kiusalama na Kiulinzi Barani Afrika na huenda hata duniani pia?

Nimesikitishwa mno na Maamuzi haya ya 'Kukurupuka' na sasa kwa hiki 'Kiherehere' chetu cha kutafuta Sifa na kutaka kupata Pesa kutoka UN na kwa Mataifa Makubwa na Tajiri tujiandae kuwa 'Target' ya akina IS, Al Shabaab na Al Qaeda ( kama bado wapo ) na wakianza Kutuvizia, Kutupiga na Kutuua tafadhali tusianze kusema kuwa wasababishi wa Matendo hayo ya Ugaidi ni Wanasiasa wetu wa Vyama Vikubwa vya Upinzani nchini Tanzania.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stegormena Lawrence Tax usingelikubali hili kwa 'Kukurupuka' badala yake ungelipima Kwanza kutokana na Mifano iliyoko ya nchi zilizokuwa na 'Kiherehere' kama hiki chetu jinsi zilivyokiona cha Moto kwa Mashambulizi ya Makundi makubwa ya Ugaidi duniani.

Binafsi nimesikitika mno na ninaogopa!
Ugaidi ni mtamu kwani tutapata fungu la ndululu za chee kama za Uviko19, siku hizi kila anayekamatwa ni gaidi ilimradi dunia isikie kilio chetu na walete pesa.
 
Nikifikiria mipaka yetu ilivo wazi kuanzia uingozwaji wa silaha holela za burundi na Congo, nikiwaza mbinu za IS na Alshabaab halafu wajue mipango yao mingi yawkuwadhoofisha hufanyika Tanzania, nikiwaza jinsi tusivyo na ukaguzi hata wa detector kwenye mabenki, hospitali, mashuleni, masokoni, vyuoni naona bado giza ni nene mbele yetu
 
Nikiwaza zaidi tulivo hatuna doria za kudumu kuanzia asubuhi hadi mchana, hapa unaona kabisa tukiwa targeted tutaisha sana
 
Nikifikiria mipaka yetu ilivo wazi kuanzia uingozwaji wa silaha holela za burundi na Congo, nikiwaza mbinu za IS na Alshabaab halafu wajue mipango yao mingi yawkuwadhoofisha hufanyika Tanzania, nikiwaza jinsi tusivyo na ukaguzi hata wa detector kwenye mabenki, hospitali, mashuleni, masokoni, vyuoni naona bado giza ni nene mbele yetu
Ni hatari Sana!!yani hii nchi yetu Mungu tu aendelee kuisimamia!!!

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Majamaa now yanawachora tu siku wakitangaza rasmi utaona intro ya warning tuache kiherehere
Itapigwa ambush
Mpaka Policcm na kamanda zero aanze wasingizia wafuasi wa CHADEMA na mbowe!
 
Aisee tumeisha.

Yani hadi Rwanda kaukwepa huu mtego alafu sisi maintaprinyuwaaa wa misaaada tumeshindwa kusoma alama za nyakati!
 
Aisee tumeisha.

Yani hadi Rwanda kaukwepa huu mtego alafu sisi maintaprinyuwaaa wa misaaada tumeshindwa kusoma alama za nyakati!
Acheni woga wanaume wa Dar nyie, hao magaidi walipokuwa wanachinja watanzania hapo Kitaya mtwara, tuliwakosea nini?? haya majitu hayana cha sababu wala nini, ni mijitu inayopenda damu za watu tu, hawana sababu kabisa, jiulize pale Congo wanaua raia kila siku, Congo imewakosea nini?? dawa ni kupambana nao tu
 
Basi sawa kabisa kijana ngangari wewe kweri-kweri.
 
Back
Top Bottom