Nina wazo la kuondoa msongamano wa watu Kariakoo, Dar es Salaam

Nina wazo la kuondoa msongamano wa watu Kariakoo, Dar es Salaam

Bado inatumika hiii ?labda hajaitangaza maana mi huwa sipendi kukata tiket stendi

Sent using Jamii Forums mobile app

Ilitangazwa sana tu kuna hadi matamasha yalifanywa kuipromoti ila bado haikushika kasi, mwaka juzi kama sikosei walipewa tuzo ila ajabu huwezi kuta mtu anaijua nadhani wale jamaa walipoona wabongo hawaelewi wakapunguza kasi ya uwekezaji huko.

I believe bado inafanya kazi.
 
Hii idea lazima ifanikiwe.
Mawazo negative kama ya kina Bufa huwa hapo tu. Hawakosagi watu wa namna hii. Hata Zuckerberg alipigwa mkwara mara kadhaa na Panel ya Maprofesa pale Harvard. Tazama leo hii (bilionea wa tano)
 
Habarini wakuu


lengo langu kubwa ni kuwafikia wateja walipo kwa bei ile ile ya kariakoo, kuwasaidia wafanya biashara wanaotoka mikoani na kufata mzigo, mtu mmoja mmoja anayefuata mahitaji kariakoo, hii itasaidia kupunguza foleni na msongamano wa watu pale kariakoo, itasaidia kutokutapeliwa, na kupata unachokihitaji kwa wakati muafaka, hata wa mikoani itawasaidia kununua bidhaa kwa bei ya kariakoo

Nahitaji watu ili tuweze kusaidiana kutimiza lengo hili

1: Mtu anayeweza kutengeneza application
2: mpiga picha mzuri sana
3: sponsor (kama atapatikana)

Wakiwa wakazi wa dsm itapendeza sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Wazo zuri sana.

Twende tupige kazi. App kama hii itachukua 3 months kuwa live.
 
Hii idea lazima ifanikiwe.
Mawazo negative kama ya kina Bufa huwa hapo tu. Hawakosagi watu wa namna hii. Hata Zuckerberg alipigwa mkwara mara kadhaa na Panel ya Maprofesa pale Harvard. Tazama leo hii (bilionea wa tano)
Tatizo mkiambiwa ukweli mnadhani tunawachukia. Mazingira na uelewa wa watu nje na TZ ni tofauti sana

Mtu wa Ileje hawezi nunua kitu online badala ya kwenda mwenyewe achilia mbali idadi ya wanaomiliki smartphone. Jumia wenyewe wanaenda kwa kusuasua na wanakubali africa kuna changamoto kubwa kufanya biashara online na hili ni kampuni kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu hata nyie wa dsm...sasa hivi tunawajua vizuri sana...zamani ndo tulijua mnaishi kariakoo na posta kwenye maghorofa...kumbe kwenye maghorofa kwa asilimia kubwa ni makaratasi na makompyuta...nyie mnaishi kwenye mbavu za mbwa kama sisi tu wa mikoani.....hata nyie kariakoo mnaenda😛😛😛😛😛😛
.... na pengine wanapigwa (tapeliwa) kifala kuliko hata wa mikoani.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana

Ila bado una changamoto katika kulifanikisha hili jambo

Kwa mtazamo wangu (wa juu juu usio wa utafiti), wajasiriamali kutoka mikoani ambao wanafuata mzigo kariakoo, hawapo conscious sana na matumizi ya teknolojia katika kupata bidhaa na masoko ya bidhaa zako

Wazo lako litafanikiwa ila unahitaji muda, ili uje uone matunda. Kwa hiyo lazima uwe mvumilivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri lile wazo la mkuu wa Dar la kuhamisha uuzaji wa magari, angefanya hili na kuanzisha sehemu nyingine na storage za uhakika ingekuwa bora sana

Sent from my SM using Tapatalk
 
Idea yako ishafeli sababu wabongo zaidi ya Instagram na WhatsApp hawawezi kutumia app nyingine yoyote.

Kuna app ya kukata tickets za mabasi ya mikoani, very useful, unakata kwa bei ile ile ya Ubungo bila kwenda Ubungo ila watu hawakutumia bado wanataka kwenda Ubungo ndo sembuse hiyo ya Kariakoo.



Sent using Jamii Forums mobile app
App gani hiyo mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafanyaje kazi? Kwamba naorder vitu kwenye app halafu unaniletea nilipo mikoani? Ni order and delivery app? Au unaonganisha muuzaji na mnunuzi tu halafu wewe unakula service fee?
 
Una wazo zuri mkuu. Ila njia unayotaka kuitumia sidhani kama itachangia kupunguza wingi wa watu kariakoo, ila itasaidia watu kupata kile wanachokihitaji kwa wakati kuliko kuzunguka mtaa mmoja kwenda mwingine mwisho wa siku unatokea ulipoanzia na bidhaa unayoitaka huyaipata.

Pia mkuu, ukiongelea app za kununua na kuuza bidhaa kwa njia ya kuangalia picha ya bidhaa na bei kisha kuwasiliana na supplier zipo mkuu, Mfano Jumia, Kupatana n.k, ila Tatizo watanzania hatujafikia huko, watu wanapenda waione bidhaa dukani na wakutane na muuzaji laivu na kuanza ku bargain bei.

Mwisho mkuu, kupunguza msongamano wa watu kariakoo ni kuathiri biashara za pale, maana katika msongamano wa watu ndipo biashara hufanyika. Nchi zote duniani zina maeneo ya masoko huria kama Kariakoo ambapo uhakika wa kupata bidhaa yoyote upo. Hivyo ule msongamano ndio fursa yenyewe.

Nadhani mkuu, Angalia zaidi namna ya kuboresha biashara ya pale Kariakoo kuliko kuwa na primary target ya kupunguza msongamano wa watu.

Ni mawazo yangu tu.
Ahsante kwa ushaur murua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom