Nina wiki ya pili kazini, ila nataka kuacha kazi

Watu wa Kyagata hao... Acha tu.
Mazingira ya hii kampuni tu hayajanivutia.

Ni kazi ya mkataba wa mwaka mmoja(renewable).

So naona siwezi kuendelea nao mbele.

Ndio kwanza nina week ya pili kazini ila nataka kuacha.

Mnanishaurije?
 
Kisaikolojia ni kwamba mtoa mada hataki kuacha kazi bali akili yake ipo kwenye vita ya kukubaliana na uhalisia na mabadiliko ya makazi.......ni jambo la muda mfupi lakini lenye msukumo mkubwa sana kwenye nafsi......nafsi yako inamwambia yeye hastahili kuwa hapo na kifikra hayupo hapo ndio maana muda mwingi anaongea na simu na watu wa Dar......Ni Hali ya kawaida kisaikolojia na huwa inakwenda inaisha taratibu baada ya kuyazoea mazingira......
 
Kupigwa kipapai kunakuaje mkuu?
Kama ni kazi unarogwa na mfanyakazi au wafanyakazi wenzako uikimbie kabisa uiache bila sababu ya msingi wao wanaleta watu wao


Kama ni nyumba yako unarogwa na ndugu au jamaa unaitelekeza kabisa na unahama na mkoa hurudi tena na hutaki kurudi tena wanahamia wao


Kipapai ni maarufu sana [emoji1787]
 
Sasa kwa akili hizo ataweza kazi za kukaa camp porini kuudumia wazungu wanaokuja kuwinda kwa miezi 6 bila kurudi nyumbani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…