Nina zaidi ya kilo 100 na nina umri wa miaka 19: Nifanyeje?

Nina zaidi ya kilo 100 na nina umri wa miaka 19: Nifanyeje?

Mimi njia ninayotumia kupunguza mwili uwa ni migogoro ya hapa na pale lazima nipungue .

Na wewe jaribu hiyo ,anza kuwakwaza majirani ili muanzishe ligi za kutukanana ,vamia mipaka yao wakushitaki kwenye baraza la ardhi ,ukirudi nyumbani usiku weka mziki mkubwa mpaka wasilale walale wanakutukana na asubuhi uitwe ofisi ya mtaa kwa kuwabugudhi watu ,wakisema ulipe faini kawashitaki PCCB ,wakiletwa watu wa NEMC kubali kulipa faini ila kama huna kubali wakuweke mahabusu ukikaa uko waombe ndugu waje wakutoe ,wakikutoa wambie hata bila wao ungeweza kujidhamini yaani iwe vita mpya na ndugu ,waite wachawi wote ndiyo wanaharibu akili yako yaani kikubwa usikose hekaheka nakuhakikishia haipiti miezi miwili utakuwa umepungua .

Mimi natumia njia hiyo nikihitaji niwe na mwili wa kawaida na uwa nafanikiwa vyema kabisa
 
Back
Top Bottom