Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata Div One ya point 11...PHY-A, CHEM-A, MATH-A, BIO-C, Additional MATH-B....ningpenda kujua kati ya A level na DIT (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama DIT ni kuzuri zaidi, je Mining Engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
Asenteni.
kijana naona kama una uroho wa pesa ya haraka ndo maana unataka kufanya shortcat.kama unataka kuwa mtaalam kwenye fani yoyote usijaribu shortcut kwani soko la ajira linahitaji wasomi wenye digree moja au zaidi hivyo jiunge a lever. baadae chuo kikuu utafanikiwa
 
diploma ni nzuri maana utasoma miaka miwili then kama ukipenda kusoma degree itakua poa pia....ukimaliza diploma utakua tofauti na wa form6 maana tayari utakua na ujuzi na hata degree haitokusumbua kivile....ila sijajua maswala ya loan(kama utahitaji) itakuaje??? na kusoma form6 kiasi flani ina kaugum tofauti na diploma....

huo mzunguko wote ni wa nini? kwani huyo kijana ni kiraza?
 
Mungu wangu tutafika kweli jamani kama wadogo zetu ndio wanawaza mshahara ni sh ngapi mtu hata hujaingia darasani kweli? na wazazi wanachangia sana hii mitindo maana kuna mmoja alikuja hapa analalamika kuwa wazazi wake wamemuambia kuwa hana msaada kwa sababu amekuwa mwalim, sasa kweli mdogo wangu unauliza kama inalipa wakikuambia inalipa ukaenda ukafika mwaka wa pili ukaona walichokushauri sio utabadilisha tena course? Ushauri wangu soma unachokipenda uje ufurahie kazi na utimitize target za mwajiri wako maana ukiipenda kazi ni mojawapo ya motivation, asikuambie mtu mshahara sio njia ya kukufanya ufurahie kazi, kuna vitu vingi vinavyoendana navyo, wanajf waelezeni wadogo zenu please hii ni sumu mbaya sana kwa wadogo zetu kila mtu anakuja anauliza mshahara, mara inalipa mara kazi gani hiyo? kumbuka hata mpishi ni muhimu sana kwako.
 
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata Div One ya point 11...PHY-A, CHEM-A, MATH-A, BIO-C, Additional MATH-B....ningpenda kujua kati ya A level na DIT (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama DIT ni kuzuri zaidi, je Mining Engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
Asenteni.

nakushauri nenda techinical college..ila chukuwa electrical au civil nadhani ina ajira nyingi na mishahara mikubwq..mm mwenyewe nilisoma Mbeya diploma sasa nachukuwa degree D.I.T..
 
diploma ni nzuri maana utasoma miaka miwili then kama ukipenda kusoma degree itakua poa pia....ukimaliza diploma utakua tofauti na wa form6 maana tayari utakua na ujuzi na hata degree haitokusumbua kivile....ila sijajua maswala ya loan(kama utahitaji) itakuaje??? na kusoma form6 kiasi flani ina kaugum tofauti na diploma....

diploma ni miaka 3..loan pia unapata mpk asilimia mia..mm nimepita huko now nachukuwa degree dit
 
Mimi nafikiri akasome A' Level. Elimu ya diploma ni nzuri lakini unaweza kuishia kuwa technician usipate kwenda chuo kikuu ukasome na kuwa engineer. Lakini tii hisia zako. Chagua kile ukipendacho zaidi.

bora awe technician ..kuliko upate zero form6 uishie mitaani..
 
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata Div One ya point 11...PHY-A, CHEM-A, MATH-A, BIO-C, Additional MATH-B....ningpenda kujua kati ya A level na DIT (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama DIT ni kuzuri zaidi, je Mining Engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
Asenteni.

diploma DIT miaka mitatu, say degree ni miaka 4, jumla nimiaka 7.
A-level ni 2yrs, degree 4yrs jumla ni miaka 6

Assume utachukua loan kwa ajili ya diploma, halafu utachukua loan kwa ajili ya degree, nadhani utakuwa na deni kubwa zaidi, unless kuwe na njia ya kukwepa kulipa.

Ukimaliza diploma(ukashindwa kuendelea mbele) unaweza kujiajiri au kuajiriwa kama mtaalam.
Ukimaliza form6 unaweza kujiajiri lakini huwezi kuajiriwa kama mtaalam.

Unapochagua kozi ya kusoma(assuming unaimudu) usiangalie market ya sasa, forecast market kuanzia mwaka ambao utakuwa unamaliza hiyo kozi. Kwa mfano kama kozi ni miaka mitatu, na unataka uwe kwenye fani ya kuchimba madini na sasa hivi watu wanaendelea kuchimba madini na migodi mingine labda inafungwa, je mpaka miaka mitatu ya shule yako iishe hayo madini yatakuwa bado yapo au?

Soma comments nyingine mbalimbali humu, natumaini utafanya uamuzi wenye manufaa.
 
kinachoonekana leo kinafaa kwamaana ya soko la ajira kesho kinaweza kikawa chini, cha msingi fanya ki2 roho inapenda na ambacho kinaweza kukufaa hata kujiajiri, dogo UJUZI KWANZA TAMAA YA MSHAHARA MKUBWA BAADAE
 
huwa sikubaliani na idea ya kuwa kuna elimu nzuri ama mbaya. its about how you sale yourself in the market. know your stuff well, be flexible and believe you can soar high. kuna watu wana mivyeti na migpa ila interview hata kwa macho tu huwezi muamini!
 
Leo ni jumapili na huu ni mda wa kujiandaa na Ibada.

Babu, kijana alinikosoa kwenye uandishi ila ni kweli, pale kuna Bacherol of Eng in field flani au Diploma of Eng in field flani, Diploma au Bacherol za pale mfumo wanao tumia ni tofauti kidogo na vyuo vingine.
Hehehehe Nyani haoni kundule LOL
 
Watu wanafikiri hata hiyo Diploma ataimaliza kwa urahisi hivi hivi, sijui siku hizi, lakini enzi za FTC, mnaweza mkapata vyeti watu nane darasa la watu 25
 
Leo ni jumapili na huu ni mda wa kujiandaa na Ibada.

Babu, kijana alinikosoa kwenye uandishi ila ni kweli, pale kuna Bacherol of Engineering in field flani au Diploma of Engineering in field flani, Diploma au Bacherol za pale mfumo wanao tumia ni tofauti kidogo na vyuo vingine.
Angalia na kaedit haraka kabla jamaa LORDVILLE hajaja kukukosoa tena
 
Last edited by a moderator:
ah ah! toka ameingia pale Prof: Nyaumwa chuo kimeanza kurudi kama zamani, yule Prof: Kondolo alikua kama kaelemewa na majuku ivi so hata chuo kikaanza kupoteana..
Watu wanafikiri hata hiyo Diploma ataimaliza kwa urahisi hivi hivi, sijui siku hizi, lakini enzi za FTC, mnaweza mkapata vyeti watu nane darasa la watu 25
 
Mimi nafikiri akasome A' Level. Elimu ya diploma ni nzuri lakini unaweza kuishia kuwa technician usipate kwenda chuo kikuu ukasome na kuwa engineer. Lakini tii hisia zako. Chagua kile ukipendacho zaidi.

Mimi namshauri akasome hiyo diploma hakuna shida. Mimi nilisoma hapo DIT wakati hii diploma ikiitwa FTC nilipomaliza nikaenda mlimani nikabadili nikasoma BBA na Masters pia sasa ni mhadhiri wa masomo ya biashara na hapo hapo najivunia ujuzi wangu niliopata DIT. Kwa kweli nilipoenda UDSM nilitesa sana mbele ya wale waliokuwa wametoka form six.
 
Ulimaliza mwaka gani DIT?
 
Back
Top Bottom