Ninachokijua kuhusu Miradi ya DMDP na Ujenzi wa Miundombinu Mkoani Dar

Huko nyuma niliwahi kusoma kwamba barabara ya Mvuti - Dondwe imo DMDP phase two. Ila sasa sijaiona hapo juu. Jee iliondolewa?
Mkuu, hii Dondwe si ipo Mkuranga? Mkuranga ni Wilaya ya Pwani sio Dar es Salaam. Kule Chanika maeneo ya Homboza mpaka Masaki mbele ndo kuna hiyo barabara au nimechanganya madesa?
 
Magufili BT to Mpiji Magohe tumekosa!

Inauma sana.
 
Hawa jamaa wanatelekeza maeneo mengi sana. Barabara za Malamba-Kwembe, Luguruni-Kwembe-Kisopwa hadi Kisarawe? Mbona wamebase sana upande wa kulia wa barabara ya Morogoro?
 
Mkuu, hii Dondwe si ipo Mkuranga? Mkuranga ni Wilaya ya Pwani sio Dar es Salaam. Kule Chanika maeneo ya Homboza mpaka Masaki mbele ndo kuna hiyo barabara au nimechanganya madesa?
Mkuu barabara inapoanzia Mvuti ni wilaya ya Ilala na barabara ilipotakiwa kuishia ni gereza la Mvuti (mwanzo wa Dondwe). Gereza hilo liko mpakani Ilala na Mkuranga. Hiyo Dondwe ni kijiji kilicho Mkuranga, lakini mpakani na Ilala.

Hivyo barabara hiyo yote iko Ilala.
 
Nahisi ni kwakuwa huko ni pembezoni. Hata Saranga yenye watu wengi naona hawajapata. Naamini awatu ya tatu wote watafikiwa.
 
Hawa jamaa wanatelekeza maeneo mengi sana. Barabara za Malamba-Kwembe, Luguruni-Kwembe-Kisopwa hadi Kisarawe? Mbona wamebase sana upande wa kulia wa barabara ya Morogoro?
Sidhani kama wote wanaweza kufikiwa kwa wakati mmoja. Nchi ya Tanzania bado Masikini. Hata hapo panapojengwa na hela za Mikopp nahisi.
 
Wilaya ya ubungo hamna hata barabara 1 upande wa jimbo la kibamba!kwa dar hamna sehemu korofi yenye barabara mbovu kama jimbo la kibamba na limepewa za uso huku mbunge wake mtemvu hana habari!
 
Kwa wilaya ya Ubungo, jumla ya kilomita 36.11 zitajengwa kwenye maeneo zaidi ya 20 kwa umbali tofauti.
Wilaya ya ubungo ina majimbo 2,ubungo kwa kitila mkumbo na kibamba kwa mtemvu,mradi haujagusa jimbo la kibamba hata kidogo,barabara zote zitajengwa jimbo la ubungo
 
Changamoto kubwa kwa jiji la Dar es salaam ni ujenzi holela kwa asilimia kubwa.
Pamoja na ujenzi wa barabara tajwa, tatizo la msingi la idara ya mipango miji kushindwa kuwasaidia wananchi kupanga na kuboresha majengo na miundombinu, hakuna tija inayotakiwa.
 
Kwa upande wa Temeke (Mbagala), mungeongeza juhudi ya kutanua Barabara ya kuanzia Kituo kikuu cha mabasi ya mwendo kasi Mbagala mpaka Vikindu pia lijengwe daraja linaloeleweka pale Kokoto.
 
Hawa watu wanachezea watu tu, sehemu kubwa ya barabara za mitaa ni mbovu mno, hazina mitaro, afadhali wangeweka hata mitaro. Kilomita kidogo sana hizo. Wanapiga promo kana kwamba wana kilometa nyingi, kumbe hakuna kitu. Tunajua wanaofaidi huu mradi ni temeke na ilala. Kinondoni na ubungo hakuna kitu.
 
Asante kwa ufafanuzi ILA mbona kinondoni zipo chache hasa jimbo la kawe ambalo halijawahi guswa na dmdp phase za nyuma????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…