Ninachokijua kuhusu Miradi ya DMDP na Ujenzi wa Miundombinu Mkoani Dar

Ninachokijua kuhusu Miradi ya DMDP na Ujenzi wa Miundombinu Mkoani Dar

Wajitahidi waweke lami zinazoeleweka halafu mambo ya matuta hayana maana dunia ya leonjia km 4 matuta elfu moja kweli.
Jimbo la mpiga kelele mtandaoni gwajima lina hali mbaya sana ya barabara sijui ccm wakimpitisha watapanda watakachovuna.

Mtandaoni kawalipa walokole feki wenzie akiwaaminisha yeye ndio raisi ajaye gwajiboy alias kibwetere ana mambo sana
 
Kwa wilaya ya Ubungo, jumla ya kilomita 36.11 zitajengwa kwenye maeneo zaidi ya 20 kwa umbali tofauti.
Nyingine ni Hondogo Shija (4.16)
Hii barabara sijui kama itajengwa, maana hata ujenzi wa chuo cha Veta ambapo ndio barabara inaishia umesimama kwa karibu miezi 9 sasa!! Bajeti ilipitishwa toka mwezi Julai, sijui kama hata mkandarasi ameshapatikana
 
Inaweza kujengwa hata kama haipo kwenye mradi. Sababu sio kila barabara inayojengwa na Tarura ipo DMDP. Ila watu wa Viwege kazi mnayo. Upite ile Barabara hadi Utoboe kwa Muhaya, lazima utubu🤣🤣🤣
Tuombe Mungu
 
Kinondoni mbona mlipata awamu ya kwanza? Hiyo Manyanya hadi kwa Mtogole Manzese pote mitaa imejaaa lami. Bora ungesema upo Mbezi Maramba mawili ningeelewa. Mnataka mpate nyinyi tu. Kinondoni ni kubwa na Sungura ni mdogo. Ila mnaweza kuwauliza Viongozi wenu. Tatizo mnafanya uchaguzi kwa mihemuko na ushabiki matokeo yake mnakosa Watetezi mnabaki kulilia mitandaoni.
Malamba mawili,king'azi,kwembe na kibamba kuna lile dongo mfinyazi,kipindi cha mvua si binadamu wala vyombo vya moto,ni kuteleza tu!
 
Jimbo la kawe , nimeshangaa kuona ni kilometa chache sana. Ni aibu kwa mbunge wa kawe. Barabara za jimbo la kawe kuanzia mbezi beach mpaka bunju ni matope tupu.
Ndio maana mwakani ntachukua form kugombea jimbo la kawe kwa ticketi ya ccm.
Gwajima kashindwa ku-deliver.
 
Kinondoni mbona mlipata awamu ya kwanza? Hiyo Manyanya hadi kwa Mtogole Manzese pote mitaa imejaaa lami. Bora ungesema upo Mbezi Maramba mawili ningeelewa. Mnataka mpate nyinyi tu. Kinondoni ni kubwa na Sungura ni mdogo. Ila mnaweza kuwauliza Viongozi wenu. Tatizo mnafanya uchaguzi kwa mihemuko na ushabiki matokeo yake mnakosa Watetezi mnabaki kulilia mitandaoni.
Nazungumzia jimbo la kawe.
Hapo kwenye uchaguzi mbunge wetu aliletwa na magufuli.
Nileteeeeni Gwajima, Nileteeeeni Gwajima!!!
 
Mwaka 2021 Zilitengwa pesa Kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutokea mbezi kwenda misumi na mpigi magoe je zilienda wapi?maana wameanza kutenga fungu la hizo barabara kuanzia 2021,2022 na 2023 lakini watu wa huko Kila siku Wanakula vumbi
Hii utekelezaji wake sijui utaanza lini!
 
Sidhani kama wote wanaweza kufikiwa kwa wakati mmoja. Nchi ya Tanzania bado Masikini. Hata hapo panapojengwa na hela za Mikopp nahisi.
Lazima kuww na balance, jimbo la Kibamba linakuwa isolated siku zote na sijui shida iko wapi.
 
Jimbo la.kawe ccm msituletee gwajima tena hana faida.na.wapiga.kura tunaishi. Kwenye matope barabara.hazijengwi.

Ukienda nae.kampeni anawalisha mihogo. Tupeni.hata.Yusufu mwenda japo kwa nguvu.aliyonayo mama kizigha najua anaweza kuteuliwa na chama ila.nae hana maajabu
 
Katika Mwaka wa fedha 2012/13 Serikali ilibuni Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project – DMDP), Madhumuni makubwa ya mradi wa DMDP ni kukabili changamoto zinazolikabili Jiji la Dar es Salaam kwa kutilia mkazo uboreshaji wa huduma za jamii kama miundombinu na kujenga uwezo wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam katika utoaji huduma, kuchangia katika kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na kusaidia katika kukabili matukio makubwa ya dharura kama majanga ambayo yanaweza kulikabili Jiji la Dar es Salaam.

Vipaumbele muhimu vilianishwa kwa kufuata vigezo muhimu bila kuangalia umaarufu wa maeneo au itikadi mbalimbali. Vigezo muhimu vilivyoanishwa ni pamoja na Miradi iwe inayounganisha maeneo ya watu wenye kipato kidogo na yaliyojengwa holela, Miradi iwe inayounganisha Wilaya na Mkoa na Miradi iwe inayounganisha maeneo mbalimbali na ukanda wa mabasi yaendayo haraka (BRT) ili kurahisisha usafirishaji.

Ikaibuliwa miradi ya Ujenzi barabara za mlisho (feeder roads) zenye urefu wa kilometa 65.6 katika Manispaa zote za Jiji ili kupunguza changamoto za msongamano. Mradi Mwingine ukawa ni Ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya mvua yenye urefu wa kilometa 31.8 katika maeneo ya mto Ng’ombe, Msimbazi, Gerezani Creek, Yombo na Kwashego ili kutatua changamoto za mafuriko.

Kupandisha hadhi makazi yaliyopangwa kiholela katika Kata 14 za Tandale, Mburahati, Mwananyamala, Gongo la Mboto, Kiwalani, Ukonga, Keko, Kilakala, Mbagalakuu, Mbagala, Mtoni, Yombo Vituka, Kijichi na Makangarawe kwa kujenga kilometa 145 kwa kiwango cha lami, kuweka nyenzo za ukusanyaji wa taka ngumu, kujenga mitaro ya kutiririsha maji ya mvua, kuweka taa za barabarani, kujenga njia za watembea kwa miguu, ujenzi wa maeneo ya mapumziko na vituo vya mabasi, ujenzi wa vyoo vya umma na ujenzi wa maeneo ya michezo.

Kuandaa Mpango kabambe wa Mfumo wa Maji ya Mvua na Maji Taka (Storm Drainage and Sewerage Master plan) kwa kushirikiana na DAWASA/DAWASCO ambao utasaidia kupanua wigo wa mifumo kwa asilimia 100% kufikia 2030. Kufunga mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa mapato katika Manispaa zote na kuepuka mianya ya kuvuja na ukwepaji wa kulipa kodi. Na Kujenga uwezo wa mwitikio wa haraka katika kukabiliana na majanga.

UTEKELEZAJI

Katika mwaka wa fedha 2015/16 Serikali iliingia Mkataba na Benki ya Dunia wenye thamani ya dola za Kimarekani 300 milioni za utekelezaji wa mradi wa DMDP kwa kipindi cha miaka mitano. Aidha, mfuko wa maendeleo ya nchi za Nordic (NDF) umechangia dola za Kimarekani 5 milioni kwa ajili ya kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia Nchi na Serikali ya Tanzania ina changia dola za Kimarekani 25.3 milioni katika mradi huu.

Katika mwaka fedha 2016/17 utekelezaji wa miradi ya DMDP Awamu ya kwanza ulianza.

ManispaaBajeti kwa Mwaka 2016/17 (Sh.)Kazi zilizoanza kutekelezwa
Temeke72,804,468,467.00
  • Kujenga barabara za mlisho 14.51km
  • Ujenzi wa mitaro mikubwa 8.9km
  • Ujenzi wa barabara za mitaa 55km
Ilala43,242,117,826.00
  • Kujenga barabara za mlisho 2.84km
  • Ujenzi wa mitaro mikubwa
  • Ujenzi wa barabara za mitaa 55km
Kinondoni63,938,175,211.00
  • Kujenga barabara za mlisho 14.51km
  • Ujenzi wa mitaro mikubwa 8.9km
  • Ujenzi wa barabara za Mitaa 55km
Sekretarieti ya Mkoa ndo ilikuwa na jukumu la ushiriki wa pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Manispaa katika maandalizi ya usimamizi wa utekelezaji wa mradi. Kwa sasa Mchakato ya Kuunda Mamlaka ya Jiji la Dar Es Salaam kusimamia miradi huu unaendelea.

Kutekelezwa kwa miradi hii kumeibadilisha sura ya Jiji la Dar es Salaam na kuwa na muonekano. Sasa hivi Ukienda Mbagala, Kijichi, Temeke, Ilala, Tandika nk, Unakuta lami hadi vichochochoroni. Yote hayo ni Matunda ya Miradi ya DMDP.

MIRADI YA DMDP II INAYOJENGWA KUANZIA 2024

Mwaka 2024, Miradi ya DMDP II inaanza tena ambapo, Mkoa wa Dar es Salaam, barabara za awali zitakazoanza kujengwa kwenye awamu ya kwanza ya utekelezaji na zimeshafanyiwa usanifu zitakuwa zina urefu wa kilomita 150.74.

Kwa wilaya ya Ubungo, jumla ya kilomita 36.11 zitajengwa kwenye maeneo zaidi ya 20 kwa umbali tofauti.

Katika maeneo yote barabara ndefu zaidi ni kilomita 9.83 ya Msumi, na Goba Wakorea kilomita 7.76, huku barabara fupi ni ile ya kilomita 0.28 ya Tiptop na barabara ya Shule.

Nyingine ni Hondogo Shija (4.16), Makoka (4.04), Posta Matembe (0.82), Sheikh Bofu (1.13), Msikitini (0.37), Sinza KKKT (0.27), Segesera (0.77), Lion (0.84), Juma Ikangaa (0.97), Mbegani (0.28), Namnani (0.66), Chimwaga (0.34) na Mikindani (0.45)

Zimo barabara za Ubungo NHC (0.6), Midizini (0.99) na Binti Kayenga (1.27). Jumla ni kilomita 36.11.

Manispaa ya Kinondoni

Kilomita 20.34 zitajengwa katika manispaa hii. Zipo barabara za Nakalekwa -Bwawani (7.32), Umoja (3.86), Mivumoni (4.79), Tegeta Polisi - Silver- Binti Matola (0.77), na Amiri/Leni Tatu (Dawasa) kilomita 0.68.

Nyingine ni Togo (0.36), Togo 2 (0.36) na Togo 3 (0.2).

Jiji la Dar es Salaam(Wilaya ya Ilala)

Jumla ya kilomita 29.8 zitajengwa zikijumuisha barabara ya Banana Kitunda- Kivule -Msongola kilomita (16.31), Barakuda- Changombe -Majichumvi (3.27), Majumba Sita - Segerea (3.31), Migombani (1.57), Tabata Mawenzi - Kisiwani 2.12 na Bombom Market (0.12).

Barabara nyingine ni Community Park 2 (0.38), Community Park 2 Road 2 (0.56), Community Park 2 Road 3 (0.11), Community Park 2 Road 4 (0.11), Community Park 1 (0.35), Community Park 2 (0.11), Kigilagila Market 2 (0.28), Kigilagila Market (0.76), Kigilagila Market 3 (0.44).

Temeke

Kilomita 32.09 zitajengwa zikigusa barabara ya Ndunguru (1.64), Masaki (3.91) Masuliza (4.04) Kipati (0.72), Agape (1.07), Kilimahewa -Toangoma (6.17), Msikitini (0.45), Mwembeni (Nyika) (0.44), Malawi (0.28), Songambele (0.32), Mwakalinga Road 1.07.

Nyingine ni Markas (0.48), Majimaji (0.32), Keko Machungwa (0.57), Magorofani (0.31), Igome (Yemen) kilomita 0.85, Diwani (0.67), Basri (0.9), Konisaga 1 (0.29), Konisaga (3 0.4), Kurasini (1.12), Taningira (0.42), Uhasibu (0.44), Kizota (0.91) na Lushoto (0.3).

Pia zimo barabara za Pendamoyo (0.56), Pendamoyo 1 (0.2), Mandera (0.85), Mkumba - Miburani (0.39).

Kigamboni

Kwa upande wa Manispaa ya Kigamboni, zitaboreshwa barabara za kilomita 32.4.

Hizi zitajumuisha MC Full Shangwe (1.38), Gofingo - Shangwe (1.77), Kibada Plot (2.91), Lingia - Nyakwale (3.75), Gezaulole (Mivumoni) (7.05), Geza Juu - Eddah Avenue (2.92), Muongozo P/S (2.85), Pengo Simba (2.47), Dege Mbutu (1.6) na Atani Dege (1.76).

Nyingine ni Machava Njama (0.7), Mtaa wa Maji - Posta (1.28), Orasa (0.89), Mzee Msomi (0.65) na Polisi Pikori.

ujio wa DMDP awamu ya pili ni kicheko na furaha kwa Wananchi ambao hawakufikiwa na awamu ya kwanza.

Je, Umenufaikaje na miradi hii Sehemu unayoishi? Nini maoni yako?

Asanteni sana. Mjadala upo wazi karibuni
"Sasa hivi Ukienda Mbagala, Kijichi, Temeke, Ilala, Tandika nk, Unakuta lami hadi vichochochoroni"! Hiyo Mbagala yenye lami mpaka vichochoroni ni Mbagala ya nchi gani? Mbagala ina barabara ya lami toka Rangitatu kwenda Kijichi, toka Rangitatu kwenda Mbande na barabara ya Kilwa kwenda Mtwara. Mitaa yote ya Rangitatu ni ya vumbi licha ya kuwepo viwanda na bandarikavu.
Unapoandika jambo jaribu kufafanua.
 
Ndio maana mwakani ntachukua form kugombea jimbo la kawe kwa ticketi ya ccm.
Gwajima kashindwa ku-deliver.
Mnachanganya mambo. Hizi barabara ni za DMDP sio za Mbunge wala CCM wala Mgawanyo wake hautokani na Majimbo bali Wilaya. Japo kwenye Kampeni wanasema wao ndo wamejenga.
 
Mbona Mbezi Beach hakuna linaloendelea? Ni lini barabara ya Ndafu itakarabatiwa na kuwekwa lami?
 
Hawa jamaa wanatelekeza maeneo mengi sana. Barabara za Malamba-Kwembe, Luguruni-Kwembe-Kisopwa hadi Kisarawe? Mbona wamebase sana upande wa kulia wa barabara ya Morogoro?
Hii barabara ya kwembe kisopwa unaingilia wap
 
Togo ilijengwa lami ya kihuni iliisha kati tu haikumaliza Togo Street yote
Hapo naona kama wakijenga kuanzia bwawani kuelelekea nyakakalekwa hiyo barabara ntafaidika nayo

Ova
Barabara ya bwawani nakalekwa unaingilia wap? Nataka nijue
 
Back
Top Bottom