Ninachokijua kuhusu Miradi ya DMDP na Ujenzi wa Miundombinu Mkoani Dar

Asante kwa ufafanuzi ILA mbona kinondoni zipo chache hasa jimbo la kawe ambalo halijawahi guswa na dmdp phase za nyuma????
Kinondoni mbona mlipata awamu ya kwanza? Hiyo Manyanya hadi kwa Mtogole Manzese pote mitaa imejaaa lami. Bora ungesema upo Mbezi Maramba mawili ningeelewa. Mnataka mpate nyinyi tu. Kinondoni ni kubwa na Sungura ni mdogo. Ila mnaweza kuwauliza Viongozi wenu. Tatizo mnafanya uchaguzi kwa mihemuko na ushabiki matokeo yake mnakosa Watetezi mnabaki kulilia mitandaoni.
 
Asante kwa ufafanuzi ILA mbona kinondoni zipo chache hasa jimbo la kawe ambalo halijawahi guswa na dmdp phase za nyuma????
Nakalekwa -Bwawani (7.32), hii barabara ipo Kawe na imekula km nyingi. Wengine unaona barabara nyingi lakini zina umbali mdogo. Mfano ni Temeke. Barabara ni nyingi Temeke lakini km chache. Barabara za Temeke baadhi ni Markas (0.48), Majimaji (0.32), Keko Machungwa (0.57), Magorofani (0.31), Igome (Yemen) kilomita 0.85, Diwani (0.67), Basri (0.9), Konisaga 1 (0.29), Konisaga (3.4), Kurasini (1.12), Taningira (0.42), Uhasibu (0.44), Kizota (0.91) na Lushoto (0.3).
 
Oohh, swali hapa JF, lile daraja la Jangwani ni la bilioni 300 au 97?

Kwa nini Kigamboni kama inatengwa hivi?

Hiyo mifumo mnaiingizaje katika bajeti zenu za kila siku, hata kwa kiwango kidogo?

So far, so good.
Ustaarabu ilikuwa ni kwenda kuuliza kwenye mjadala husika wa daraja. Usiwe kama unavuta bangi.
 
Safi sana Hatimae Msumi inapata Lami...
Njooni Msumi Viwanja bado vipo bei nzuri tuu
 
Huko nyuma niliwahi kusoma kwamba barabara ya Mvuti - Dondwe imo DMDP phase two. Ila sasa sijaiona hapo juu. Jee iliondolewa?
Ni kweli Mkuu, nimeangalia nikakuta ilitengewa fedha na tenda ilishatangazwa kwenye bajeti ya 2021/22 kwenye awamu ya kwanza ya DMDP. Sijajua kwanini haijaanza kujengwa hadi sasa.

Ila kwa uzoefu unakuta watu wanagoma kupisha miundombinu ya Barabara na kwenda Mahakamani hasa waliojenga katibu na barabara. Miradi mingine inachelewa kutokana na uzembe wa Mkandarasi. Wengine wanachelewesha miradi kutokana na Serikali kutokutoa hela. Unakuta fungu la hela linahamishwa kutoka mradi A kwenda B. Mfano hela za Barabara ya Bonyokwa huko Kimara zilihamishwa zikaenda kujenga barabara lililobomoka kipindi cha mvua za el nino.

Nyie wakazi wa huko muwe mnahudhuria Mikutano ya Serikali ili kuwauliza maswali kama haya.

Tenda ya hiyo barabara hii hapa
 

Attachments

Ungefupisha haya maelezo kwa maneno machache sana. CCM ime fail kwa hali zote na bila mabadiliko ya mfumo na viongozi hakutakuwa na ufanisi.
 
Majohe Viwege sijaiona. Kuna mpuuzi kaninunulisha kiwanja huko kwa kuniaminisha soon lami inapita kupitia DMDP.
Inaweza kujengwa hata kama haipo kwenye mradi. Sababu sio kila barabara inayojengwa na Tarura ipo DMDP. Ila watu wa Viwege kazi mnayo. Upite ile Barabara hadi Utoboe kwa Muhaya, lazima utubu🤣🤣🤣
 
Asante kwa ufafanuzi ILA mbona kinondoni zipo chache hasa jimbo la kawe ambalo halijawahi guswa na dmdp phase za nyuma????


Jimbo la kawe , nimeshangaa kuona ni kilometa chache sana. Ni aibu kwa mbunge wa kawe. Barabara za jimbo la kawe kuanzia mbezi beach mpaka bunju ni matope tupu.
 

Hii ina maana vyanzo vya mapato vya jiji kuweka miundombinu ya barabara lami hadi tupate mikopo na ufadhili.

Lini majiji yetu yataweza kukusanya kodi ili kuweza kukarabati na kutengeneza miundo-mbinu bila kutegemea mikopo na ufadhili

Maendeleo endelevu ya majiji inatakiwa itokane na mapato ya ndani, mwaka 2050 itakuwa imechakaa je tutakwenda tena kuomba mkopo nafauu World Bank n.k

Hili jambo la kujitegemea na majiji kujiendesha kwa mapato ya ndani liangaliwe kwa uzito unaostahili.
 
Togo ilijengwa lami ya kihuni iliisha kati tu haikumaliza Togo Street yote
Hapo naona kama wakijenga kuanzia bwawani kuelelekea nyakakalekwa hiyo barabara ntafaidika nayo

Ova
 
Tanzania sio Dar pekee kwamba Kila kitu ni huko huko
 
Mtoa mada Kwa utaalamu wako, Na Kwa kuwa hii ni nchi ya wapigaji unadhani tumepigwa kiasi Gani? Ukizingatia awamu hii ni ya fungulia mbwa we chukua Kwa urefu wa kamba na hakuna wa kukubugudhi.

Nikiri kwetu walijenga rami zege kama nusu kilometer na walipoishia Mimi ndio nachepuka Kuelekea kwangu umbali usiozidi mita 200, Imekuwa faraja. Kwa Sasa naona mkandarasi amerudi site anafukua kipande kingine Cha kama nusu kilomita.
Sema taa hawajaweka labda wakifika mwisho.

Mwisho hizi taa za Solar ambazo kwangu naona ni sihihi kabisa, kuna njia napita nakuta baadhi hazifanyi kazi nani anawajibika katika maintenance, maana tusijenge tu, bali tujue kutunza ili Value for Money ionekane.
 
DMDP awamu ya kwanza ilifanyika wakati wa Mwendazake na hakuna mradi wowote wa DMDP mwaka ulioutaja wewe
 
Mwaka 2021 Zilitengwa pesa Kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutokea mbezi kwenda misumi na mpigi magoe je zilienda wapi?maana wameanza kutenga fungu la hizo barabara kuanzia 2021,2022 na 2023 lakini watu wa huko Kila siku Wanakula vumbi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…