Synthesizer Hili jambo unatakiwa uwahoji madereva kwa nini wanagoma kwenda hizo nchi na pia usidhani serikali haiko makini kwenye hili.
Binafsi nadili sana na transportation najua madhila wanayopata madereva kwa sasa na kwenye hili serikali inaenda vizuri na update ya madereva.
Hakuna wanaokataa kupimwa ila shida hata ukionekana negative unaenda kwa kunyanyapaliwa na vilevile hawaruhusiwi kufanya chochote kushuka kwenye gari kwenda maliwatoni,kuoga kupata mahitaji ya chakula nk.
Hivi wewe kwa akili yako hilo unaona ni sawa?
Nini maana ya kumpima mtu na kukubali aingie kwako ili umtese?
Hivi huu ugonjwa ulianzia Tanzania? na hapo Rwanda,Zambia na Kenya ndio ulipelekwa na watanzania?
Kama unakumbukumbu fatilia vizuri visa vya mwanzoni vya hizo nchi walipeleka watu gani halafu ndio uone hizi nchi zina maana gani na jirani zao.
Kwa nini Uganda watu hawalalamiki sana, kama nchi hizo nilizotaja hapo japo najua kwa sasa nao wanataka kubadilika ila si kwa kiwango cha hizo nchi tajwa hapo juu.
Kuna vitu wakati mwingine tujitahidi kuufatilia ukweli tukaujua kuliko kutoa tu lawama moja kwa moja kwa serikali.
Balozi wa Tanzania upande wa Zambia najua anapata malalamiko sana kwa siku kama mbili hizi najua kapokea kesi nyingi za watanzania kuteseka.
Hivi unamoima mtu hapo mpakani kwa nini usimrudishe kwao halafu umpeleke zaidi ya kilomita 180 na kisha kwenda kumuweka bila matibabu yoyote na huku chakula pia ni cha tabu?.
Kwenye hili jaribuni kuweka siasa na uvyama pembeni wanaoumia ni madereva wetu watanzania wenzetu na walipa kodi na wazalisha uchumi wetu tusibeze hatua zinazofanywa serikali iko macho kwenye hili.