Ukweli ni kwamba hatoshi kwenye hiyo nafasi ,na hata hao waliomzunguka wanajua kama hatoshi kwenye hiyo nafasi na HAKUBALIKI ndio maana wanaogopa kumshindanisha na mtu yeyote mana wanajua hatapita wanataka kumpa URAISI WA VITI MAALUMU...wa FOMU MOJA.
Kama kweli wanaamini anakubalika waruhusu watu wachukue fomu,halafu atoke nje ya ukumbi aruhusu kamati kuu imjadili na ipitishe majina 40 kati ya hayo majina 40-60 apite tano bora apite na tatu bora..GHAFLA TU mtu mmoja anaibuka kusemea kamati kuu imeshaamua anaisemea kamati kuu ,wanamkingia kifua wanambeba,wanaogopa nini kama anakubalika ndani ya chama.??
2)KIKUNDI CHA WAHUNI WACHACHE mapapa ya mafisadi,mapiga dili ja majizi ,mabilionea ,wana mtandao SYNDICATE,MACARTEL ndiyo wanamtaka APITE KWA AJILI YA KULINDA MASLAHI YAO BINAFSI..dili zao na nafasi za watoto wao wake zao,biashara zao nakadhalika..
3) PIA wanamshauri vibaya mfano mikataba mibovu kama KUUZA BANDARI..ilikuwepi mezani toka awamu zilizopita lakini mbona wao walipokuwwpo madarakani hawakuisaini ..mana walijua ingewachafua wakaiacha magufuli alipoikuta mezani kwake akaikataa AKASEMA NI KICHAA TU ndiye anaweza kusaini mikataba mibovu kama hii ya Kuuza rasilimali za taifa ...lakini wao wanamshauri vibaya kwa sababu wanajua wao hawatachafuka wao na watafaidika nayo wao binafsi na si Taifa.
4)Haya mambo ya KUTEKANA na kuuana pia wanamshauri vibaya,mbona MKAPA alikuwa anasemwa sana ,anachorwa kwenye vibonzo,hata JK alisemwa sana kukosolewa sana lakini mbona wao hawakuteka na kuua watu,mbona walivumilia kukosolewa,katika maisha huwezi hata ya kawaida tu huwezi kupendwa na watu wote ..isikosolewe WEWE SIO MUNGU wewe sio malaika ..nabii Musa aliwatoa wana israeli utumwani MISRI walikokuwa wanateswa na farao,ila walipofika njiani wakaanza kimpinga nabii Musa wakasema bora ungetuacha utumwani Misri tulikuwa tunakula vizuri, kuliko ulivyotuleta jangwani,yani kuna watu wanampinga hata Mungu aliewaumba.,wengine wanamkosoa Mungu alivyowaumba kwa kunikarabati kurekebisha asili ya maumbile yaa wqlivyoumbwa wanamkosoa Mungu.WEWE ni nani usiotaka KUKOSOLEWA na KUPINGWA..
Yule KIJANA kachoma picha tu aliyechora mwenyewe amekamatwa ..watu wanatekwa kwa sababu ya KUKOSOA ...tunachafua taswira ya nchi..wanaoshauri wanashauri vibaya na hata kipindi cha uongozi wao pia hawakufanya hivyo wao,
RAFIKI anyekushauru vibaya huyo ndiyo HAKUTAKII MEMA na hakupendi.
Ila hawa akina GWAJIMA,POLE POLE na wanashauri vizuri..
5)Kufungia vyama vya UPINZANI haina haja chama tawala si huwa kinashinda miaka yote toka uhuru,sasa kuna haja gani ya kuwafunga wapinzani ,na kufungia wapinzani wakati wa kipindi cha kampeni...ILA HALI UHAKIKA WA KUSHINDA UPO NA MIAKA YOTE HUWA MNASHINDA..sasaa hii si ni kujichafua...
Vyombo vya dola ni vyenu,tume ya uchaguzi ni yenu,UHAKIKA wa kushinda kwa asilimia zaidi 100% upo sasa kwa nini kufungia upinzani??
Hii inachafua na kubomoa zaidi ya kujenga,na inazidi kuipa nguvu upinzani na ymaarufu mpaka nje ya mipaka ya kimataifa ,unaweza kufikiri unaidhoofisha au una ua upinzani kumbe ndio unaipa nguvu na umaarufu,na kuipa kukubalika na wananchi na puplic sympathy.na jamii za kimatifa zinazopenda DEMOKRASIA.
Yani huwezi ukashindana mbio na moinzani wako huku UMEMFUNGA KWA KAMBA MIKONO NA MIGUU,halafu useme nimemshinda mbio.
CHAUMA au ACT haviwezi vikawa VYAMA VIKUU VYA UPINZANI mbadala wa CHADEMA haiwezekani.CHADEMA HAIWEZI KUFA KWA STAILI HII.
Mimi siamini kama kwenye chama cha kijani hakuna mtu mwenye Akili mbona wakati wa JK hakukuwa na ujinga kama huu,nahisi wanamdanganya afanye vitu ambavyo hata wao hawawezi kuvifanya HUKU WANAMCHEKA..
Wana CCM wenzangu tufuate ushauru wa POLE⁷ POLE NA GWAJIMA.
6)WATANZANIA WA LEO ni tofauti sana na watanzania wa miaka 10 iliyopita..wameelimika utandawazi umekuwa sana,wanaelewa sana kuliko tulivyowazoea UJINGA umepungua sana..
sio wa kuwanunulia kofia na tisheti kuwapa baiskeli na piki piki...WANATAKA MATOKEO..na huko tunakoenda 2030 ndio UELEWA WA WATANZANIA utaongezeka ,watadai MAENDELEO sio kuhongwa ili wakuchague.
View: https://youtu.be/5HiTEZ2P-kQ?si=Cin32ialzNYuPWhR